02 October 2012

Wabuni 60 kushiriki Swahili Fashion



Na Amina Athumani

ZAIDI ya wabunifu 60 wamejiandikisha kushiriki maonesho ya mavazi ya nguo za kiswahili 'Swahili Fashion Week', yaliopangwa kufanyika Desemba 6 hadi 8, mwaka huu Dar es Salaam.


Kabla ya maonesho hayo, baadhi ya wabunifu watakaoshiriki Swahili Fashion Week, watapata nafasi ya kushiriki Swahili Fashion Week Nairobi Oktoba 6, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana mwandaaji wa maonesho hayo, Mustapha Hasanali alisema wiki hiyo ya mavazi ya Kiswahili itajumuisha wabunifu wakongwe na chipukizi.

Alisema maonesho hayo yatashirikisha wabunifu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kwamba maonesho ya mwaka huu yatakuwa na tofauti kubwa ikilinganishwa na yaliyopita.

Hasanali alisema kati ya wabunifu 60 watakaoshiriki Swahili Fashion Week, 15 kati yao watawakilisha jukwaa la Swahili Fashion Week Nairob, Kenya.

Hasanali alisema tangu kuanzishwa kwa maonesho hayo mwaka 2008, yamekuwa yakiibua vipaji vingi vya wabunifu chipukizi.

Aliwataja baadhi ya wabunifu watakaoshiriki maonesho hayo kutoka Kenya ni Moo Cow na Patricia Mbela, Mohamed Bana, Morna Omondi, Shenu Hooda, Anna Adero, Vaishali Morjaria, Annesophie Achera na Wangechi Muriithi.

Kwa Tanzania ni Gabriel Mollel, Diana Magesa, Lucky Creations , Hameed Abdul na Sarah Masenga.

Hasanali  alisema onesho hilo limedhaminiwa na Precision Air, Phat Productions, Capital FM (Kenya) na 361 Degrees.

No comments:

Post a Comment