01 October 2012

Vyombo vya habari vyatakiwa kutumia lugha ya alama



Na Agnes Mwaijega

VYOMBO vya habari nchini vimesahuriwa kujitahidi kuanza kutumia lugha ya alama ili viziwi nao waweze kupata taarifa mbalimbalina kutoa maoni.


Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw.Assah Mwambene (MAELEZO) katika maadhimisho ya wiki ya viziwi yaliyoandaliwa na Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA).

Alisema mfumo wa sasa hivi wa vyombo vingi vya habari nchini unawatenga viziwi kwa sababu hawawezi kuelewa chochote.

"Mkakati wa kuendeleza huduma ya habari kwa viziwi ni muhimu na utawasaisdia hata kujona nao ni sehemu ya jamii," alisema.

Mhadhiri Mwandamizi wa Lugha za kigeni na Isimu Chuo Kikuu Dar es Salaam Dkt.Henry Mzale alisema upo umuhimu wa televisheni kujitaidi kutumia wakalimani watakaowawezesha viziwi kupata taarifa .

Alisema changamoto kubwa inayowakabili viziwi nchini ni kutokuwepo na wakalimani hali ambayo inasababisha mambao yao mengi kukwama.

Hata hivyo alishauri serikali kuona umuhimu wa kuwawezesha viziwi kupata taarifa kwa kuhakikishan wanaliingiza suala hilo katika katiba mpya.



No comments:

Post a Comment