08 October 2012
Madereva wa daladala waponda ujio wa Treni
Mariam Said na
Zena Mohamed
MADEREVA wa daladala jijini Dar es Salaam wamesema ujio wa usafiri wa treni hautapunguza foleni bali utaongeza foleni mara dufu.
Wakizungumza na waandishi wa gazeti hili baadhi ya madereva walisema ujio huo utaongeza foleni katika barabara ambazo zitakatiza njia ya treni(reli).
Dereva anayefanya safari za Temeke/Kariakoo kupitia barabara ya Kilwa,Rafiji alisema kuwa pindi treni inapokatiza barabara magari yote lazima yasimame ili kuipisha hivyo itasababisha msongamano na kuifanya foleni iendelee.
Dereva mwingine Bw. Ismail Abajani anayefanya safari za Temeke-Kariakoo kupitia barabara ya Kilwa alisema kuwa serikali ipunguze magari mabovu na kubadilisha miundombinu ilikuweza kukabiliana na foleni na siyo kuleta treni.
Naye dereva anayefanya safari za Ubungo-Kariakoo Bw.Said Mudy alisema biashara itakuwa ngumu kwa upande wa daladala kwasababu treni inachukuwa watu wengi hivyo wengi wao watakimbilia kwenye treni na kufanya wao wakose abiria.
"Hii itakuwa hasara kwetu kwasababu waajiri wetu watakuwa hawatuelewi juu ya viwango walivyotupangia vikipungua kutokana na ugumu wa biashara,"alisema.
Pia dereva anayefanya safari za Mabibo-Kariakoo Bw.Rajab Salum alisema pamoja na treni kuletwa kwajili ya kupunguza foleni lakini itakuwa inaharibu biashara ya daladala kwasababu abiria wengi watakimbilia treni na kuacha daladala.
"Treni inachukuwa watu wengi hivyo itatufanya hata sisi kutubadilishia ruti kama tulikuwa tunaenda Kariakoo mara nane basi tutaenda mara mbili na foleni itaendelea kama kawaida,"alisema.
Bw. Haroon Juma dereva wa Ubungo -Kariakoo aliipongeza serikali kwa uwamuzi huo kwasababu watu wengi wataacha magari yao na kutumia usafiri wa treni na kufanya foleni kupungua baada ya magari mengine ya binafsi kupakiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment