01 October 2012

Wanafunzi 80 waliofanya vizuri wazawadiwa Ilala


Na Heri Shaaban

WANAFUNZI 80 wa shule za sekondari Mkoa wa Ilala wamezawadiwa kwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha tatu na tano.

Tuzo hizo zilitolewa Dar es Salaama jana, na Wakuu wa Shule Tanzania (TAHOSSA)katika afla iliyofanyika sekondari ya Tambaza.

Akitoa taarifa ya uendeshaji wa mitihani Mwenyekiti wa Kamati ya Mitihani Ilala, Bw.Hussein Zuberi alisema kuwa umoja huo lengo lake kuunga jitihada za serikali katika kukuza taaluma katika shule zote za serikali hapa nchini.

Bw.Zuberi alisema kuwa mitihani hiyo huendeshwa katika ngazi ya Kanda na mikoa ,kama ilivyo katika mkoa huo wa Ilala na hiyo ni mara ya kwanza kwa kamati hiyo kuendesha mitihani kwenye ngazi ya mkoa.

"Kamati ya mitihani Mkoa Ilala TAHOSSA huendesha mitihani uendesha mitihani ya kumaliza mwaka wa masomo kwa kidato cha tatu na kidato cha tano kila mwaka na washindi upewa zawadi,kidato cha tatu wanafunzi 41, kidato cha tano wanafunzi 39,"alisema Bw.Zuberi.

Madhumuni ya mitihani hiyo kuwajengea wanafunzi hali ya ushindani,kuwasaidia walimu kupata uzoefu katika utungaji,kuhariri, kusahihisha mitihani,kusaidia walimu kujua uwezo wa wanafunzi wao.

Kwa upande wake Mbunge wa Tarime Bw.Nyambari Chacha alisema kuwa wamebaini kitu kizuri kwa wanafunzi wa shule hizo ili waweze kujihamini huko mbele,na kuwataka wazazi kushirikiana na kamati za shule katika kufatilia maendeleo ya watoto wao.

Bw.Chacha aliwapongeza mpango huo na kusema kuwa mtaala wa elimu uwe unabadilika kila wakati kutokana na mabadiriko tuliyonayo,pia kabla kubadirisha kwa mtala huo tuwandae walimuwatakaofundisha.

Aliutaka umoja huo wa TAHOSSA kusimamia vizuri shule za kata hili ziweze kutoa wanafunzi bora watakaojenga Tanzania ya baadae.


No comments:

Post a Comment