04 October 2012

Goba wazidi kulalamikia kero ya maji



Na Rose Itono

WAKAZI wa Goba, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, wamesema mradi wa maji uliokuwa ukisimamiwa na Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Bw. John Mnyika, umekufa na kusababisha wananchi wakose huduma ya maji safi na salama.

Wakizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, baadhi ya wakazi hao walisema hivi sasa wanalazimika kununua maji kwa bei kubwa.

Bi. Regina Maziku, mkazi wa Goba kwa Sanga, alisema wanalazimika kulipia sh. 40,000 kwa boza moja la maji
ili waweze kupata huduma hiyo.

Aliongeza kuwa, kutokana na ugumu wa maisha baadhi ya wananchi wanashindwa kumudu gharama hizo hivyo kukosa haki ya kupata huduma za msingi kama maji.

“Unakuta mwanamke anahangaika siku nzima kutafuta maji bila kufanya shughuli nyingine yeyote ya kumuingizia kipato, hii ni kuzidishiana umaskini,” alisema Bi. Maziku.

Alisema awali walikuwa wakipata maji kupitia mradi huo ambao ulikuwa ukisimamiwa na Bw. Mnyika kwa karibu ili kuwabana viongozi waliokuwa wakijinufaisha kwa masilahi binafsi.





No comments:

Post a Comment