08 October 2012
AY kuhamasisha mradi kusaidia watoto wenye mahitaji malum
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Airtel, kupitia kitengo chake cha huduma kwa jamii na Msanii wa Bongofleva, Ambwene Yesaya 'AY', wameanza mchakato wa kutembelea shule zitakazonufaika na mradi maalum wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum ili kujionea changamoto zinazowakabili na kuwahimiza Watanzania kuchangia mradi huo unaoendeshwa kwa ushirikiano na Baraza la Maendeleo ya Vitabu Tanzania (BAMVITA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Ofisa Mawasiliano na Matukio wa kampuni hiyo, Dangio Kaniki ilieleza kwamba kampuni hiyo ikiwa na Balozi wake, AY itatembelea shule zote zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubainisha matatizo wanaoyokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia.
Alisema shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum zinahitaji vitendea kazi vingi ili kuwafanya wanafunzi hao kuweza kupatiwa elimu inayostahili.
“Shule hizi zinamahitaji mengi sana, tumeona ni vyema kumtumia pia Balozi wetu huyu msanii maarufu nchini A Y kuendelea kuwafikishia jamiii ujumbe waendelee kuchangia katika mradi huu wenye lengo la kuendeleza jamii” alisema Dangio .
Akizungumza mara baada ya kutembelea shule ya msingi Sinza Maalum, Balozi AY, alisema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuongeza kiwango cha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum.
“Watoto hawa wenye uhitaji maalum nimejionea mwenyewe kuwa wakiwezeshwa wanaweza, ndio maana naona ni vyema zaidi kushirikiana na Airtel pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha tunawachangia vijana wetu hawa nao waweze kuendeleza hata vipaji vyao pamoja na elimu yao," alisema AY.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment