01 October 2012

Serikali yaombwa kuboresha bajeti ya elimu Mwanza




Na Daud Magesa,
Mwanza


SERIKALI imetakiwa kuboresha bajeti ya elimu ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa vitabu,mabaara na vifaa vyake na miundombinu ya majengo na nyumba za kuishi walimu katika shule mbalimbali nchini.

Wito huo umetolewa jana na mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Mkolani, Wilayani Nyamagana, Mwanza, Bw.Noel Mtekateka, ambaye ni Mhasibu wa Jeshi la Polisi mkoani hapa akiomba serikali kuongeza bajeti katika wizara hiyo ya elimu.

Bw.Mtekateka alitoa wito huo jana baada ya Mkuu wa Shule hiyo,Bw.Asencio Mathias kudai kuwa shule inakabiliwa na upungufu wa walimu wa sayansi,nyumba za kuishi walimu,mabara na vifaa vyake,vitabu vya kiada na ziada,pamoja na vyumba vya madarasa ,wakati akitoa taarifa fupi ya shule.

Akizungumza na waandishi wa habari Bw.Mtekateka alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo serikali haina budi kuboresha na kuongeza bajeti ya elimu,lakini pia akaomba wadau kusaidia sekta ya elimu nchini sekta ambayo ni kitovu cha kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali.

Alisema kukosekana kwa maabara katika shule, ukosefu wa vitabu na uhaba wa walimu kunasababisha Taifa kuzalisha wataalamu wasio na uwezo kielimu.

Awali katika taarifa yake kwa mgeni rasmi, Mkuu wa shule hiyo, Bw.Mathias alisema shule inabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu, vyumba vya madarasa,uzio,uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi,upungufu wa vitabu vya sanaa,majengo ya maabara na vifaa vyake.

Alidai wanahitaji majengo matatu ya maabara,ambapo moja ya ujenzi wake umekwama,vyumba vitatuu vya madarasa,viwanja vya michezo,vifaa vya kujifunzia,maji ya bomba na nishati ya umeme.

Kuhusu mafanikio mkuu huyo wa shule alisema jamii imeweza kutunza mazingira ya shule ili kuzuia

No comments:

Post a Comment