02 October 2012
Manispaa Ilala yaongeza ukusanyaji mapato 2012
Mwali Ibrahim na Amina Athumani
MANISPAA ya Ilala, Dar es Salaam, imefanikiwa kuongeza mapato yake kutoka asilimia 88 mwaka 2010/11, hadi 99 mwaka huu.
Meya wa manispaa hiyo Bw. Jerry Silaa, aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika uzinduzi wa bango la mapato na matumizi.
Alisema mapato hayo yameongezeka kutokana na ukusanyaji kodi ikiwemo ya mabango yaliyopo barabarani na leseni ya ujenzi na vyanzo vingine.
Akifafanua ongezeko hilo, Bw. Silaa mabango ya matangazo yameongeza mapato kwa asilimia 102, sawa na sh. bilioni 2.25 kutoka sh. bilioni 1.47.
Upande wa leseni ya ujenzi mapato yameongezeka kwa asilimia 205 sawa na sh. milioni 307 kutoka kwenye sh. milioni 154 mwaka jana.
Alisema licha ya mafanikio hayo, sehemu iliyofanya vibaya hasa mwaka huu ni ukusanyaji mapato ya leseni ya biashara.
Bw. Silaa alisema hali hiyo inasababisha mansipaa hiyo ishindwe kufikia malengo yake licha ya kuwa na wafanyabiashara wengi ambao wameonesha kushindwa kulipa kodi baada ya kazi ya ukusanyaji kufanya na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA).
Aliongeza kuwa, manispaa hiyo imeunda mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanafikia malengo yao na tayari wameunda kamati ambayo itakutana na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda ili kuzungumzia mikakati hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment