04 October 2012
Dkt. Mgimwa: Uchumi wetu unaendelea kukua
Leah Daud na Kassim Mahege
UCHUMI wa Tanzania unaendelea kuimarika licha ya kuwepo changamoto mbalimbali pamoja na mfumuko wa bei.
Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyasema hayo Dar es Salaam juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara iliyofanywa na ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IFM), ambao uliongozwa na Bw. Paolo Mauro.
Alisema wakati ujumbe huo ukijitimizsha ziara hiyo, Bw. Mauro, alisema uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika vizuri ambapo ukuaji wa pato la Taifa mwaka huu, unatarajiwa kukua kwa kati ya asilimia 6.5 na 7.0.
Alisema mfumuko wa bei umekuwa ukipungua taratibu kutoka kwenye kiwango cha juu ambacho kilifikiwa mwaka 2011.
Dkt. Mgimwa alisema Bw. Mauro aliisifu Tanzania kutokana na makusanyo mazuri wa mapato ambapo matumizi ya Serikali yalidhibitiwa ipasavyo na si madeni yote ambayo yalitokana na matumizi ya ndani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment