02 October 2012
Michuano ya Kifimbo kuzinduliwa leo
Na Daud Magesa, Mwanza
MASHINDANO ya kusaka vipaji na kuviendeleza kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, jijini hapa yanatarajia kuzinduliwa leo kwenye Uwanja wa Nyamagana.
Ligi hiyo ya kuwania Kombe la Dkt. Kifimbo, itashirikisha timu 14 za Wilaya za Nyamagana na Ilemela, ambayo itachezwa kwa mtindo wa mtoano hatua ya awali.
Washindi wa hatua hiyo wataingia robo fainali, ambayo itachezwa kwa mtindo wa ligi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa michuano hiyo ambaye ni mganga wa tiba asilia, Dkt Kifimbo, alisema lengo ni kuvumbua vipaji vya vijana na kuviendeleza.
Alisema wachezaji wenye vipaji watakaopatikana wataunda kombani, ambayo itafanya ziara ya michezo katika Mikoa ya Arusha, Kagera na Shinyanga.
“Mashindano haya yamelenga kuvumbua vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kuwajenga na kuwaendeleza kisoka.
"Likini pia kuhakikisha kunakuwa na mashindano mengi katika Wilaya hizi za Nyamagana na Ilemela, kwani hadi sasa kuna michuano ya Copa Coca-Cola pekee,” alisema.
Alisema bingwa wa ichuano hiyo atazwadiwa seti moja ya jezi na mpira mmoja, wa pili ataondoka na mipira miwili huku wa tatu akipata mpira mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment