03 October 2012
Rufaa ya Lema yasogezwa tena
Na Pamela Mollel, Arusha
HATIMAYE rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema (CHADEMA), jana imeshindwa kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, baada kuibuka hoja zaidi ya nne.
Umati mkubwa ulijitokeza katika mahakama hiyo wakiwemo wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wamekusanyika nje huku wengine wakiwa ndani ya mahakama.
Hoja hizo zilianza kutolewa na wakili wa mkatiwa rufaa, Bw. Mughwai, kudai rufaa iliyokatwa na Bw. Lema kupitia mawakili wake, Bw. Method Kimomogoro na Bw. Tundu Lissu, imekosewa kwa kukiuka kanuni za Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu.
Bw. Mughwai alihoji kwanini Bw. Lema akimbilie kukata rufaa ndani ya siku 29 badala ya siku 60, bila kuangalia kasoro zilizojitokeza. Mahakama iliahidi kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza kesi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Haki isogope mlundikano wa wafuasi wa chadema. huyu lema ni gaidi wa kichaga,ni mtu mwenye makundi ya kihalifu. ni hatari kuwa na kiongozi wa kitaifa kama huyu. ataandaa makundi ya kuuwa watu watakaompinga akiwa madarakani. dalili za madikteta anazo huyu kijana ni hatari sana wananchi tuchunge hii chama inaendeshwa na wafanya biashara na wanakifadhili,wewe mtanzania unategemea nini kwa hawa matajiri? wanajaribu kusoma nyakati,hivyi yuko tajiri anayeichukia ccm? ole wenu. HATARI HIYOOO
ReplyDelete