01 October 2012
Migiro kukomesha unyanyapaa, ubaguzi kwa waathirika
Na Mwandishi Wetu
MJUMBE Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi barani Afrika Dkt.Asha-Rose Migiro ameanza majukumu kwa kuitembelea Tume ya Taifa ya UKIMWI (TACAIDS) na kuwataka wadau katika vita kutilia mkazo katika masuala yanayochangia maambukizi mapya kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza na wafanyakazi wa tume hiyo juzi, Dkt.Migiro alisema kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni kufahamiana na wadau katika vita dhidi ya ugonjwa huo.
Alisema kuwa ugonjwa wa UKIMWI umeathiri kila familia barani Afrika, hana budi kutia mkazo zaidi katika masuala yanayochangia maambukizo mapya kwa kiwango kikubwa na kusema kuwa unyanyapaa na ubaguzi wa kijinsia kuwa miongoni mwa mambo atakayoyapa kipaumbele katika kutekeleza majukumu yake ya kutokomeza ugonjwa huo barani Afrika.
“Suala la unyanyapaa, suala la unyanyasaji wa kijinsia, na mengine kama hayo lazima yapigwe vita kwa nguvu zote kama kweli tunaka kulilinda bara letu na UKIMWI,” alisema na kuongeza kuwa, yuko imara kutekeleza majukumu hayo kwa kuwa anajua fika kuwa kuna watu nyuma yake wanaounga mkono jitihada za mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
Alisema kuwa kama hali isingekuwa hivyo, asingekubali majukumu haya,
hata hivyo, Dkt. Migiro alitoa changamoto kwa TACAIDS na wadau wengine kuihusisha jamii katika kila hatua na mikakati ya kuutokomeza ugonjwa huo.
“Kule chini ndani ya jamii ndipo kuna kila kitu…habari nyingi ziko huko, si vema basi kama tutawatenga wana jamii katika kupanga mikakati yetu, alisema Dkt. Migiro.
Wakati wa kipindi chake cha u-Naibu Katibu Mkuu kuanzia 2007 had 2012, Dtk. Migiro alijihusisha na masuala ya kupambana na UKIMWI duniani na pia barani Afrika, huku akitia msisitizo wa kupunguza hatari ya maambukizo kwa wasichana na wanawake na pia kuhakikisha haki za WAVIU zinaheshimika kwa mujibu wa UNAIDS.
Akitoa mwelekeo wa mapambano dhidi ya VVU na UKiMWI nchini, Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Fatma Mrisho alibainisha kuwa moja wapo ya changamoto ambazo zinafaanyiwa kazi na tume ilikuwa ni ubadili wa tabia ambao unatokea lakini sio kwa kasi iliyotarajiwa.
Akasema, Tanzania inaelekea kuzuri kwenye malengo matatu ambayo ni kutokuwa na maabukizi mapya ifikapo 2015, kutokomeza ubaguzi na unyanyapaa unaohusiana na UKIMWI na UKIMWI kutokuwa ni chanzo cha vifo tena ifikapo 2015.
Maambukizo baina ya 2003/2004 na 2007/2008 yalipungua kutoka asilimia 7 kwenda asilimia 5.7.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Dkt. Mrisho, takwimu zinaonyesha kuwa maambukizi kwa wasichana wa chini ya umri wa miaka 24 yameongezeka, jambo ambalo linafanyiwa kazi kupitia mkakati wa UKIMWI wa Taifa 2013-2017 ambao utakamilika ifikapo mwisho wa mwaka huu (2012).
Kama njia ya kukabiliana nna hali hiyo, Dkt. Mrisho alisema tume ilikuwa imejipanga kuanza kuwalenga vijana hasa wasichana kwa vile maambukizo yanawapata zaiddi. “Tunaendelea kufanya hivyo kupitia shule, njee ya shule, michezo, sana na mitandao ya kileo (social media).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment