08 October 2012
Mkapa azindua tawi jipya DCB
Na Darlin Said
RAIS mstaafu Bw. Benjamini Mkapa amezindua Tawi la Benki ya Biashara (DCB)Magomeni na kuwataka Watanzania wanao kwenda kukopa warejeshe mkopo kwa kuwa benki hiyo siyo ya kisiasa.
Benki hiyo ambayo zamani ilikuwa ikiitwa benki ya wananchi DCB imebadilishwa jina na kupandishwa hadhi na kuwa benki ya kibiashara, ambayo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa uhamasishaji ununuzi wa hisa za haki za beki hiyo kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Bw. Mkapa aliyasema hayo jana Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika matukio hayo, ambapo alisema benki hiyo imeanzishwa baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kukosa mitaji ya kuboresha maisha yao enzi za uongozi wake.
Bw.Mkapa alisema mwaka 1990 kulikuwa na uzinduzi wa mpango wa uendeshaji wa sekta isiyo rasmi, ambapo katika mkutano huo alipata malalamiko hayo kwa wananchi na kulazimika Halmashsauri na serikali kuu kuanzisha benki itakayowasaidia wananchi.
Hivyo Bw.Mkapa aliwataka wananchi kuendelea kujiunga na DCB ili waweze kupata huduma zitakazowasaidia katika kujikwamua kiuchumi, kwani kilio chao kimepatiwa uvumbuzi.
Pia aliipongeza benki hiyo kwa kushika tano bora kati ya benki 15 katika soko la hisa Afrika na kuwa ya kwanza Afrika Mashariki.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Bw.Raymond Mkwawa aliiomba Serikali kuwa na imani na kujivunia mafanikio kwani lengo la DCB kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupunguza umaskini kwa wananchi.
Kw upande wa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Bw.Paul Rupia alisema benki hiyo imepata mafanikio makubwa, kwani mwaka 2002 walianza na wateja 12,141 wa kuweka na kukopa amana ya sh. Biilioni 1.8 na leo wanazaidi ya wateja 200,000 wenye amana ya sh.Bil 77.9.
Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam BW.Said Meck Sadik alisema DCB imekuwa rafiki wa wananchi wenye kipato cha chini kwa kuwakopesha akina mama hata kama hawana dhamana ya kupata mkopo hivyo inaongoza kwa kuwajali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment