04 October 2012
Upelelezi kesi ya Msofe haujakamilika
Na Rehema Mohamed
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Marijani Msofe (50), umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali Bi. Mwanaisha Komba, alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salam mbele ya Hakimu Agnes Mchome, wakati shauri hilo lilipoletwa kwa ajili ya kutajwa.
Bi. Komba alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo anaiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutajwa ambapo Hakimu Mchome alipanga Oktoba 17 mwaka huu.
Katika shauri hilo, mshtakiwa anadaiwa Novemba 6,2011, huko Magombeni anadaiwa kumuua Bw. Onesphory Kitoli.
Bw. Msofe anayetetewa na wakili Bw. Majula Magafu, anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Kwa mara ya kwanza mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo Agosti 10 mwaka huu, na kusomewa shtaka hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment