01 October 2012

Ahmadiyya wakutanisha waumini kufahamina


Na Darlin Said

JUMUIYA ya Waislam wa Ahmadiyya umefanya Mkutano wa 43 ambao unafanyika kila mwaka duniani,lengo ikiwa ni kuwakutanisha waumini pamoja ili waweze kufahamina na kujifunza mambo ya kiroho.

Akifungua Mkutano huo Dar es Salaam jana Amiri Mkuu wa Jumuiya hiyo, Tanzania Bw.Amiri Chaudhry alisema watu wametakiwa kufuata Quran na mafundisho ya Mtume Muhhamad (SAW) ili waweze kukabiliana na changamoto zinazoikumba uislamu ulimwenguni badala ya kulipiza kisasi kwa kufanya mambo yanayoenda kinyume na mafundisho ya dini hiyo.

Pia alisema kwa kufanya hivyo wataweza kuondokana na mambo maovu kwa kuelimishana kuwepo kwa Mungu ili wawe waja wema.

Alisema tofali la msingi wa mambo mema limejengwa na Mwenyezimungu kupitia Quran tukufu, hivyo aliwahasa waumuni hao kuwa mfano mwema kwa kufuata mafundisho yaliyokuwemo katika kitabu hicho.

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bw.Seifu Nakuchima alitoa wito kwa vijana kuwa mfano wa raia wema kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.

Bw.Nakuchima alisema vijana wanatakiwa kuwa na maadili mazuri, kwani wao ndio Taifa linalotegemewa na wazee.

Pia waliwataka kuwa makini na mitandao na wajaribu kutumia akili kwa kile wanachokiona katika mitandao hiyo.

Katika Mkutano huo ambao mada mbalimbali zitatolewa ikiwemo umuhimu wa elimu kwa vijana wa kiislamu pamoja na kivipi uislamu ulivyomkomboa Mwanamke wa leo.

Zaidi ya  Waumini 3000 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambazo utafikia kilele chake leo.  


No comments:

Post a Comment