02 October 2012

Sekta binafsi zatakiwa kuwekeza katika jamii



Na Darlin Said

SERIKALI imezitaka sekta binafsi kuwekeza zaidi katika masuala ya kijamii ili iweze kufikia malengo mbalimbali.

Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Abdallah Chaulembo, aliyasema hayo jana wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya.

Alisema sekta binafsi zione umuhimu wa kuisaidia Serikali ambayo peke yake haiwezi kuboresha maisha ya Watanzania.

“NI vyema sekta hizi zikawekeza katika sekta ya afya, elimu ambayo ndio ufunguo wa maisha na maji kwa kuchimba visima ili kurahisisha upatikanaji wake,” alisema.

Alitoa wito kwa viongozi wa jumuiya hiyo kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanachochea maendeleo ya jamii na kuwasaidia wasiojiweza kama dini inavyotaka.

Aliwapongeza viongozi hao kwa kuwa mstari wa mbele kudumisha amani kwa kuzingatia mafundisho ya Uislamu.

Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Bw. Abdulrahmani Ame, aliwataka Waislamu nchini kuzingatia mafundisho ya dini yao.




No comments:

Post a Comment