08 October 2012
Waandisi waandaa matembezi ya hisani
Neema Kalaliche na
Jane Hamalosi
Taasisi ya Waandisi imeandaa matembezi ya Hissani kwa ajili ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa lengo la kuwajengea uwezo.
Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Rais wa Taasisi ya Waandisi Bw.Malima Bundara wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, alisema fedha hizo zitasaidia kuwajengea uwezo wa wakufanya kazi kwa vitendo.
Bw.Bundara alisema kuwa suala la kuchangia fedha hizo litakuwa endelevu ili kuondokana na tatizo la ajira kwa waandisi ambapo wameamua kujitokeza hadharani kukabilia na matatizo mbalimbali ikiwemo ya kijamii na kiuchumi kwa kutumia taaluma yao.
"Tunayo matatizo ya miundombinu,nishati na ajari ambazo zinaonekana kuongezeka kila mwaka na Serikali inajitahidi kukabiliana na matatizo hayo ingawa ufumbuzi wa matatizo haya unategemea Waandisi na mafundi" alisema.
Pia alisema ili kuondokana na hali hiyo Taasisi kwa kushirikiana na serikali wameunda vikosi kazi vya wataalamu ambavyo vitajikita kwenye ubainishaji wa matatizo na kutengeneza mikakati ya kutatua matatizo hayo kitaalam.
Aidha alisema Taasisi hiyo ina mpango wa kukusanya takwimu za waandisi Tanzania kwa kuwatembelea sehemu zao za kazi nchi nzima ili kutambua kiasi cha ushiriki wa wahandisi katika soko la hapa nchini na nje.
Alisema kuwa Taasisi hiyo kuanzia mwaka 2013 watakuwa na taratibu ya kutoa zawadi na tuzo kwa waandisi wenye mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa kila mwaka ambapo zina lengo ya kuwapa changamoto waandisi ya kufanya kazi kwa bidii.
Matembezi hayo yanayotarajiwa kufanyika oktoba 7 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Bw.Mohamed Bilal na yataanzia karimjee hall mpaka na kuishia katika viwanja vya leaders.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment