02 October 2012
Vyombo vya majini vithaminiwe-Abbas
Na Anneth Kagenda
WITO umetolewa kwa Watanzania kuvitunza na kuvithamini vyombo vya usafiri majini ili ubora wake uendelee kuwepo sambamba na kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.
Mtaalam wa Vifaa vya Meli, Bw. Hussein Abbas aliyasema hayo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika Maonesho ya Bahari Dunia ambayo yaliandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti, Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATA).
Maonesho hayo yalifungwa mwishoni mwa wiki ambapo Bw. Abbas aliongeza kuwa, upo umuhimu wa kila Mtanzania anayetumia usafiri huo kutunza vifaa vyake ili kuokoa maisha ya wananchi wengi hasa inapotokea ajali wakati chombo husika kikiwa safarini.
“Hivi sasa tumejipanga, tuna mpango wa kuingiza meli mpya iitwayo Azam Searink 1, kutoka Uturuki ambayo itakuwa ikibeba abiria 1,500 na magari 200,” alisema.
Alisema lengo la kuleta meli hiyo ni kutokana na kampuni ya Azam kuwa na mikakati ya kuboresha ubora wa huduma zake kwa abiria.
Alipngeza kuwa, hivi sasa kampuni hiyo ipo katika mchakato wa kuingiza meli nyingine Kilimanjaro 4, yenye uwezo wa kuchukua abiria 700, ambayo itatembea kwa saa moja kutoka Dar es Salaam hadi Unguja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment