02 October 2012
Rais ateua Kamishna Jenerali Magereza
Na Mwandishi Wetu
RAIS na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Kikwete, amefanya uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza na Makamishna wa idara mbaolimbali.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilisema Rais Kikwete amemteua Bw. John Minja kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza.
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peter Ilomo, ambaye ndiye amesaini taarifa hiyo, alisema maodisa wengine walioteuliwa ni
Dkt. Juma Malewa kuwa Kamishna, Divisheni ya Sheria na Uendelezaji wa Magereza, Bw. Deonice Chamulesile kuwa Kamishna, Huduma za Urekebishaji na Bw. Gaston Sanga kuwa Kamishna, Divisheni ya Utawala na Fedha.
Wengine ni Bw. Fidelis Mboya kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambapo kabla ya uteuzi huu, Bw. Mboya alikuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria na Uendeshaji wa Magereza.
Maofisa wengine ni Bw. James Celestine, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Jamii Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, sasa amekuwa Naibu Kamishna wa Magereza ambapo atarejea Magereza na kupangiwa kazi nyingine. Uteuzi huo umeanza Septemba 25 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment