31 July 2012
Lissu awalipua wabunge saba *Adai ndio wanahusika na kashfa ya rushwa *Yumo Ole Sendeka, Vicky Kamata, Nassir
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Bw. Tundu Lissu, jana amewataja kwa majina wabunge saba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anodai kuhusika na kashfa za rushwa ambayo inalihusu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Mgomo wa walimu watikisa nchi *Mikoa mbalimbali yaunga mkono, serikali yatoa tamko
Na Waandishi Wetu
WAKATI mgomo wa walimu ukiwa umeanza jana katika baadhi ya shule za msingi na sekondari nchini, Serikali imesisitiza mgomo huo ni batili na kutoa onyo kwa walimu ambao wanawatisha, kuwapiga na kuharibu mali za wenzao wasiogoma, waache mara moja.
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, amesema chanzo cha migogoro na migomo katika vyuo vikuu nchini ni Wenyeviti wa Mitaa na vijiji kupitisha fomu za watoto wa vigogo ili kuomba mikopo na kuwaacha watoto wanaotoka katika familia zisizojiweza kukosa mikopo hiyo.
MAZUNGUMZO
Ofisa wa Jeshi la Polisi Kituo cha Mbezi Luis (jina halikufahamika), akiwatuliza wanafunzi wenye hasira waliovamia kituo hicho ili kuwataka wawashinikize walimu kuwafundisha baada ya kuanza kwa mgomo, Dar es Salaam jana.(Picha na Aloyce Lukwaro)
Siri hujuma mitambo ya TANESCO yafichuka
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Mwibara Bw. Kangi Lugola (CCM), jana amefichua siri ya kuwepo mkakati unaoratibiwa na vigogo wa Shirika la Umeem Tanzania (TANESCO), ili kuharibu mitambo ya umeme kwa lengo la kumuumbua Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kutokana na msimamo alioweka kuhakikisha hakuna mgao wa umeme.
Wizara yajipanga kuzuia ugonjwa wa Ebora
Na Grace Ndossa
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imesema tayari imejipanga kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka nchini Uganda na kuua watu 14.
Akizungumza na Majira, Msemaji wa Wizara hiyo, Bw. Nsachriss Mwamwaja, alisema tayari wamefanya mawasiliano na mikoa yote nchini pamoja na Wilaya ili wajipange kukabilina na ugonjwa huo.
Mshtakiwa amtaja Bilal kesi ya EPA
Na Rehema Mohamed
MSHTAKIWA wanne katika kesi ya wizi wa zaidi ya sh. bilioni 3.9 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Bw. Imani Mwakosya (54), ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Bw. Daudi Balali, alipitisha fedha hizo zilipwe kwa Kampuni ya Mibare Farm kwa kuwa ilionekana ni deni halali.
TUCTA kupinga Sheria Mpya ya Mifuko kwa maandamano
Na Darlin Said
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Mkoa wa Dar es Salaam, limetangaza maandamao ya amani ili kupinga sheria inayowazuia wanachama wanaojitoa kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii, kutopata mafao hadi watakapofikisha umri wa miaka 50 au 60.
Wanawake Goba washauri kujiunga kwenye vikundi
Na Rose Itono
WANAWAKE waishio kwenye Kata ya Goba, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, wameshauriwa kujenga utamaduni wa kujiunga kwenye vikundi ili kujiletea maendeleo endelevu.
Wakizumgumza Majira Dar es Salaam, juzi baadhi ya wanachama wa Kikundi cha Kusaidiana cha Wanawake wa kata hiyo (KIWAKUKI), walisema umaskini kwa wanawake hauwezi kupungua kama hawatajiunga na vikundi vya kusaidiana.
Abiria afariki katika ajali ya pikipiki Dar
Neema Kalaliche na Jane Hamalosi
ABIRIA wa pikipiki yenye namba za usajili T668 BXL, aina ya Jinghen, Mwanaidi Saidi (25), amefariki dunia baada ya pikipiki hiyo kugongwa na gari ambalo halijafahamika.
Ajali hiyo imetokea eneo la Santiago, Barabara ya Msongola, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.
AMKO ALAT
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mstahiki Dkt. Didas Masaburi, akisoma tamko la Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) mwishoni mwa wiki, linalokemea vitendo vya mabaraza ya madiwani kuwaondoa madarakani Wenyeviti wa Halamashauri mbalimbali nchini bila kufuata utaratibu. (Picha na Charles Lucas)
Wafanyakazi mgodi wa Ruby wakimbia makazi
Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAFANYAKAZI wote waliokuwa wakiishi ndani ya mgodi wa madini unaomilikiwa na Kampuni ya Mundarara Ruby Mining Company Ltd, uliopo Kijiji cha Mundarara, Wilaya ya Longido, mkoani Arusha, wameondoka mgodini hapo baada ya vijana wa kimasai (morani), kuwatangazia vita isiyo na kikomo.
Manispaa K/ndoni kuanzisha wodi za matibabu ya kulipia
Na Darlin Said
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, imejipanga kuazisha wodi za kisasa za kulipia 'Fast track', katika Hospitali ya Mwananyamala ambazo zitatoa huduma bora kwa wananchi.
Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Songoro Mnyonge, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akitoa ufafanuzi juu ya hatua walizo zichukuwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za matibabu katika hospitali hiyo.
Sabodo: Wanaotaka kuchimbiwa visima vya maji leteni maombi
Na Mwandishi Wetu
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Mustafa Sabodo, amewata wananchi na taasisi mbalimbali zikiwemo za dini ambazo zinahitaji msaada wa kuchimbiwa visima vya maji, wampelekee maombi.
Watumishi Pori la Akiba wadaiwa kuchoma moto bendera ya CCM
Na Said Njuki, aliyekuwa Kondoa
MGOGORO uliodumu muda mrefu kati ya wakazi wa Vijiji vya Ikengwa, Keikei na Idindiri, Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma na watumishi wa pori la Akiba la Mkungunero, lililopo katika vijiji hivyo, umechukua sura mpya.
Gari la kanisa laua watoto wawili, wanakwaya sita
Na Bryceson Mathias, Mvomero
GARI la Parokia ya Mt. Theresia Maskati, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, limepinduka na kuua wanakwaya sita, watoto wawili papo hapo na kujeruhi wengine 13 wakati wakienda kutoa huduma ya ekaristi na ubatizo kwenye Kigango cha Chaginali.
Azam yamuweka sokoni Ngassa
Na Zahoro Mlanzi
HATIMAYE Klabu ya Azam FC, imekubali kumruhusu kiungo wao, Mrisho Ngassa kujiunga na timu yoyote kwa dau la dola 50,000 baada ya kuonekana kiungo huyo kutokuwa na mapenzi na timu hiyo.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Ngassa kuonesha dhahiri mapenzi yake kwa mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga kwa kuibusu jezi ya timu hiyo baada ya kuifungia Azam bao la pili lililoipeleka fainali ya michuano hiyo.
Migogoro ya ardhi inakwamisha maendeleo
Na Grace Ndossa
MIGOGORO ya ardhi ambayo inaibuka mara kwa mara inachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo na kuendelea kuangamiza zaidi ya asilimia 70 ya watanzania ambao huishi kwa kutegemea kilimo.
MIGOGORO ya ardhi ambayo inaibuka mara kwa mara inachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya sekta ya kilimo na kuendelea kuangamiza zaidi ya asilimia 70 ya watanzania ambao huishi kwa kutegemea kilimo.
Jamii iwajibike kuwasaidia watoto wa mitaani, yatima
KITANDA usichokilalia, huwezi kujua kunguni wake, shida na mateso wanayopata watoto waishio katika mazingira hatarishi na wale wa mitaani ni vigumu kuelezea.
Watoto hawa hawajui leo au kesho watakula nini, hakuna anayehangaika kuwatafutia chakula, wanapolala na njaa hakuna wa kumlilia na wakiumwa hakuna wa kumweleza hivyo huendelea na maisha yao hadi wanapopata nafuu au kupona kabisa.
TAFF wapewa changamoto
Na Elizabeth Mayemba
SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF), limetakiwa liendelezwe na watu wa tasnia
hiyo, ili serikali iweze kutia mkono wake.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na TAFF, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Utamaduni na Michezo ambaye alikuwa ni
mmoja wa wakufunzi wa semina hiyo, Profesa Eliasante Gabriel alisema maendeleo ya
tasnia ya filamu lazima yaanzishwe na wenyewe, ili serikali iweze kutia mkono wake.
BFT yahuzunishwa Kidunda kudundwa
Na Mwali Ibrahim
SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) limehuzunishwa na bondia wake, Selemani Kidunda aliyepigwa katika mashindano ya Olimpiki yanayoendelea London, Uingereza.
Bondia huyo pekee wa Tanzania, juzi alichezea kichapo kwa kupigwa kwa pointi 20-7 na bondia kutoka Moldova Belous Vasilii,.
MAJAJI EBSS
Mjaji wa EBSS 2012 Ritha Paulsen (katikati) Master Jay (kushoto),
wakimsikiliza jaji Salama Jabir kulia aliyekuwa akifafanua jambo juzi katika Ukumbi wa La Casa Chika jijini Tanga wakati wa usaili wa kuwatafuta nyota EBSS Tanga. Na Mpigapicha Wetu
wakimsikiliza jaji Salama Jabir kulia aliyekuwa akifafanua jambo juzi katika Ukumbi wa La Casa Chika jijini Tanga wakati wa usaili wa kuwatafuta nyota EBSS Tanga. Na Mpigapicha Wetu
Nyota 6 wa Airtel kupigwa msasa
Na Amina Athumani
NYOTA sita wa Airtel Rising Star, wanatarajia kushiriki kliniki ya kimataifa itakayoendeshwa na makocha wa Klabu ya Manchester Uneted.
Kliniki hiyo inatarajia kufanyika Oktoba mwaka huu, ambapo nyota hao wataambatana na kikosi cha timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, watakaoshiriki michezo ya Afrika itakayofanyika Nirobi, Kenya.
30 July 2012
Kashfa nyingine yaibuka bungeni *Mbatia adai Kamati ya Maadili imekosa sifa *Awalipua wajumbe wake kuhusika na rushwa
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, amekosoa uadilifu wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyopewa jukumu la kuwachunguza wabunge waliohusika na kashfa za rushwa katika Wizara ya Nishati na Madini na kutaka wajumbe wa kamati hiyo, wajitakase kwanza kabla hawajaanza kazi hiyo kwani baadhi yao wananuka rushwa.
NIDA yaongeza muda wa kujaza fomu vituoni
Stella Aron na Grace Ndossa
MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeongeza muda wa wiki moja ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kujiandikisha.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari, ilisema hivi sasa mchakato wa kujiandikisha utamalizika Agosti 6 mwaka huu na hakutakuwa na nyongeza ya muda.
CUF waivaa CCM, CHADEMA *Wataka itamke kuwavua ubunge wabunge wake
Na Peter Mwenda
CHAMA cha Wananchi (CUF), kimetoa tamko la kuutaka uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), utamke kuwavua madaraka ya ubunge wabunge wote wa vyama hivyo waliotuhumiwa kuhusishwa na vitendo vya rushwa.
Mnyika: Nipo tayari kutoa ushahidi wa Nchimba
Na Stella Aron
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo Bw. John Mnyika, amesema yupo tayari kutoa ushahidi wa tuhuma alizotoa dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Bw. Mwigulu Nchimba (CCM).
Alisema anachosubilia kwa sasa ni kuitishwa kikao cha Kamati ya Kanuni ya Bunge ili aweze kuwasilisha ushahidi unaomuhusu Bw. Nchemba, kuhusika na ufisadi wa Fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Serikali yaombwa kuchangia mfuko wa tiba mbadala
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI na wadau mbalimbali, wameombwa kuchangia mfuko wa utoaji elimu kuhusu matibabu ya tiba mbadala.
Ombi hilo limetolewa Dar es Salaam jaana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili na Utafiti cha Boresa, Bw. Boniventura, wakati akizungumza na Majira kuhusu maadhimisho ya dawa za asili yanayotarajiwa kufanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia Agosti 27-30 mwaka huu.
MAONESHO
TIPF yawataka Waislamu kushiriki sensa ya watu, makazi
Na Anneth Kagenda
TAASISI ya Tanzania Islamic Peace Foundation (TIPF), imewataka Waislamu nchini kuwapuuza watu wanaotaka kukwamisha ushiriki wao katika Sensa ya Watu na Makazi badala yake washiriki kikamilifu kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
TAMWA: Waliokufa Mv Skagit wengi wao ni wanawake, watoto
Na Stella Aron
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA), kimeitaka Serikali kuweka mikakati ya kuimarisha usalama wa vyombo vya usafiri baharini ili kuepusha vifo visivyo vya lazima kwani waathirika wakubwa wa ajali zinazotokea ni wanawake na watoto.
UHUSIANO
Sakata bei ya pamba kutua kwa Pinda
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
SAKATA la kushuka kwa bei ya pamba, limechukua sura mpya baada ya viongozi wa Halmashauri za Wilaya saba katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Geita, kuunda timu maalumu ya watu saba ambayo itakwenda kuonana na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda.
TAPOA wapata uongozi mpya
Na Frank Geofray, Jeshi la Polisi
CHAMA cha Askari Wastaafu wa Jeshi la Polisi (TAPOA), kimefanya uchaguzi wa viongozi wake ambao watakiongoza ili kufikia malengo ya kuchochea maendeleo ya wanachama.
Nafasi zilizogombewa katika uchaguzi huo ni Mwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mwanasheria wa chama, wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na wadhamini.
MAFUNZO SENSA
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo, akifungua mafunzo ya sensa ya watu na makazi juzi kwa waandishi wa habari kutika yombo mbalimbali kutoka mikoa kumi ya kanda ya ziwa na kanda ya kati, semina iliyofanyika jijini Mwanza, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo ili waweze kutumia taaluma yao kuelimisha jamii juu ya zoezi hilo. (Picha na Patrick Mabula)
Majimarefu awataka wapiga kura kuwapuuza wapinzani Na Mashaka Mhando, Korogwe
MBUNGE wa Korogwe Vijijini, mkoani Tanga Bw. Stephen Ngonyani, maarufu 'Profesa Majimarefu', amewata wapiga kura jimboni humo kupuuza maneno ya wapinzani wake kisiasa wanaodai wamekosea kumpa mbunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Madiwani Shy wamtema Mwenyekiti halmashauri
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
WIMBI la kukataliwa kwa wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya na Majiji limeendelea kupamba moto baada ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Malmashauri hiyo Bw. Amos Mshandete.
100% tz Flava yakuna mashabiki wa burudani
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Lager, ni miongoni mwa kampuni ambazo hushirikiana na jamii katika mambo mbalimbali.
Ukiangalia kwa haraka bia hiyo, imekuwa ikiiweka jamii pamoja kupitia michezo kwa kuandaa tuzo za wanamuziki (Kili Music Awards) pamoja na udhamini kwa timu kongwe nchi za Simba na Yanga.
Flying Eagles yaiduwaza Ngorongoro
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Nigeria (Flying Eagles), imeishangaza timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania wenye umri huo (Ngorongoro Heroes) kwa kuichapa mabao 2-1.
Mchezo huo ulipigwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ukiwa na wa kwanza hatua ya pili ya kuwania kucheza fainali za 18 za Afrika.
Saintfiet aanza tambo Jangwani *Apania kuivua ubingwa Simba
Na Speciroza Joseph
BAADA ya kutwaa Kombe la Kagame kwa mara ya kwanza, Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet amewapongeza wachezaji wake na kutamba huo ni mwanzo bado Ligi Kuu Bara na mashindano mengine.
Yanga juzi ilitwaa kombe lake la tano la Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) ikiwa chini ya kocha huyo aliyeanza kuifundisha timu hiyo wiki tatu zilizopita akichukua mikoba ya Kostadin Papic aliyetimuliwa.
Sakata la mgomo lawagawa walimu *CWT: Hatujali vitisho, Dar, Pwani waupinga Na Waandishi Wetu Tumaini Maduhu na Masau Bwire RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Gratian Mukoba, amesema chama hicho hakijali vitisho na propaganda zitakazotolewa na wajiri wao (serikali), na wananchi kutokana na mgomo uliopangwa kuanza Jumatatu asubuhi. Akizungumza na waandishi wa habari Daresalaam jana, Bw. Mukoba alisema mgomo huo umezingatia taratibu na sheria za utumishi wa umma ambapo suala la vitisho ni jambo la kawaida. Alisema propaganda zilizotolewa hadi sasa ni pamoja na tamko Serikali likiwataka walimu wapuuzie mgomo huo kwa madai ni batili kutokana na shauri lao kuwa mahakamani. “Sisi kama CWT tunasema kuwa, mgomo upo pale pale, hatuogopi vitisho vyovyote kwa sababu wanachama wenyewe ndio wameafiki kwa asilimia 95.7 ambao ni walimu wa shusle za awali, msingi, sekondari, maofisa walioko kwenye ukaguzi wa shule pamoja na wakufunzi wa Vyuo na Ualimu na Maendeleo ya Jamii,” alisema. Bw. Mukoba aliwataka walimu kushiriki mgomo huo akidai ni halali na umeitishwa na CWT kwa mujibu wa sheria na hauna uhusiano wowote na ushiriki wao katika sensa ya watu na makazi. Hata hivyo, alisema walimu wanapaswa kutambua kuwa madai kuwa shauri lao lipo mahakamani, hakiwaondolei utararatibu wa kuendelea na mgomo kwani hadi sasa, mahakama haijatoa amri yoyote ya kusitisha mgomo huo. “Kutokana na hoja hiyo, tunaisishi Serikali isitake kutumia kivuli cha mahakama kugandamiza haki za walimu ambao wamezingatia taratibu na sheria zote za nchi kufanikisha mgomo. “CWT tunatoa wito kwa walimu wote nchini, kuunganisha nguvu zao ili tupate haki zetu tunazoidai Serikali bila kujali vitisho ambavyo vinaendelea kutolewa,” alisema Bw. Muhoba. Wakatu huo huo, Mwandishi Wetu kutoka Ruvuma anaripoti kuwa, CWT mkoani humo, kimesisitiza kuwa, suala la mgomo lipo pale pale kama ulivyopangwa. Msisitizo huo umetokana na ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms), uliotumwa na Bw. Mukoba kwa viongozi wa chama hicho ukiwataka wanachama wa CWT kutoenda kazini Jumatatu. Walisisitiza chombo kinachotakiwa kutoa tamko la kusitisha mgomo huo ni mahakama pekee si wapinzani wao ambao ni Serikali. Katika Mkoa huo, walimu asilimia 97 wameunga mkono mgomo uliotangazwa na CWT ambapo kundi dogo la walimu hao ndilo halijapiga kura ya kuunga mkono. Taarifa kutoka ndani ya chama hicho mkoani hapa zinasema kuwa, pamoja na Serikali kuwa na utamaduni wa kukimbilia mahakama, kifungu cha 84/ (1) (e) cha sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004, kinairuhusu Mahakama ya Kazi kuweka zuio baada ya kujiridhisha wahusika wameshiriki katika mgomo batili. Kifungu cha 84/(2) kinaizuia mahakama kutoa amri hiyo hadi zipite saa 48 baada ya maombi ya zuio kufikishwa kwa aliyeitisha mgomo ambaye ni CWT. Mwenyekiti wa CWT, mkoani hapa, Bw. Castory Ngonyani na Katibu wa chama hicho Bw. Luya Ngonyani, waliwataka walimu kusikiliza kauli za chama na sio ya Serikali. Katika hatua nyingine, wakati CWT kikitangaza mgomo huo nchi nzima kuanzia Jumatatu, baadhi ya walimu wamegawanyika hasa mkoani Dar es Salaam na Pwani, wakidai hawako tayari kugoma bali wataingia kazini na kuchapa kazi kama kawaida. Wakizungumza na Majira jana kwa sharti la kutotajwa majina yao gazetini, baadhi ya walimu wa shule mbalimbali, walisema mgomo uliotangazwa na CWT kupitia Rais wake Bw. Mukoba, hauna manufaa kwao bali unalenga masilahi yake na viongozi wa kitaifa. Walidai viongozi CWT ngazi ya Taifa, wamewageuza walimu kuwa mradi wao kwa kutangaza migomo ya msimu ili upande wa pili uwaone, kuwapoza chochote na kutangaza mgomo hakuna. “Kimsingi tumechoshwa na mchezo wanaotufanyia, kama ni suala la kugoma, agome yeye na kamati yake, mwaka 2008 Bw. Mukoba alitangaza mgomo lakini siku moja kabla haujaanza, tulikusanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, akatangaza mgomo hakuna. “Katika mkutano ule kulikuwa na wawakilishi kutoka mikoani tukiamini tunatangaziwa taratibu za kufanya ili kufanikisha mgomo, alivyotangaza mgomo hakuna tulikasirika na kumpiga kwa chupa za maji kwani tulijua tayari amehongwa,” walisema na kuongeza kuwa, hivi sasa hawauungi mkono kwani wamechoka kudanganywa. Walisema ndani ya uongozi wa CWT wenyewe hawaelewani kwa sababu ya fedha wanazokatwa walimu ambapo hadi sasa, mgogoro huo umeshindwa kutatuliwa. “Walimu wote nchini tunakatwa kila mwezi asilimia mbili ya mshahara wetu, hatujawahi kuambiwa fedha hizi zinatumika vipi, hatuoni faida yoyote zaidi ya viongozi CWT kula fedha zetu. “Kama CWT haitutendei haki, moyo wa huruma wameutoa wapi hadi kuishinikiza Serikali ipandishe mshahara kwa asilimia 100 kama si kutaka kujikosha kwetu, hatugomi hadi tuambiwe fedha zinazokatwa zinatumika vipi vinginevyo tutawafikisha mahakamani kwa ufisadi wanaotufanyia,” walisema walimu hao. Alisema hivi sasa, walimu wanajipanga ili kuandaa maandamano makubwa ya kupinga uongozi wa CWT kwani chama hicho mbali ya kuchukua ada ya uanachama, kimeshindwa kugharamia sare za walimu hasa wanapoadhimisha siku yao kitaifa. “Kila siku tuaambiwa chama hakina fedha wakati michango yetu kwa mwezi mmoja inatosha kununua fulana kwa walimu wote, wao wana fedha zetu wanashindwa kutuhudumia iweje waishutumu Serikali hadi kuitisha mgomo, kwanza watutendee haki kabla ya kuomba nguvu yetu,” walisema. Majira lilipomtafuta Bw. Mukoba ili kuzungumzia madai hayo, alimwambia mwandishi wetu amtafute baada ya saa mbili kwani yupo kwenye kikao na muda huo ulipofika, simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani. Waandishi wa haabari hii ni Tumaini Maduhu, Masau Bwire na Steven Augustino.Sakata la mgomo lawagawa walimu *CWT: Hatujali vitisho, Dar, Pwani waupinga
Na Waandishi Wetu Tumaini Maduhu na Masau Bwire
RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Gratian Mukoba, amesema chama hicho hakijali vitisho na propaganda zitakazotolewa na wajiri wao (serikali), na wananchi kutokana na mgomo uliopangwa kuanza Jumatatu asubuhi.
Askofu Songea aonya viongozi
Na Joseph Mwambije, Mbinga
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Kanisa Katoliki, mkoani Ruvuma, Mhashamu Norbert Mtega, amewataka viongozi nchini kuheshimu miiko ya uongozi tofauti na ilivyo sasa.
Mhashamu Mtenga aliyasema hayo jana katika katika Jubilei ya miaka 25 ya Jimbo la Mbinga na Jubilei ya miaka 25 ya utumishi wa Askofu mstaafu wa jimbo hilo Emanuel Mapunda.
Vitambulisho vya Taifa sasa vurugu tupu
Na Stella Aron
MCHAKATO wa ujazaji fomu za vitambulisho vya Taifa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, umegubikwa na utata mkubwa kutokana na fujo zinazotokea katika baadhi ya vituo.
Fojo hizo zinasababishwa na mrundikano wa watu ambapo hali hiyo ilijitokeza jana kwenye Kituo cha Mbezi Temboni.
'Mikataba mizuri ya kazi itamaliza migogoro kazini'
Na Gift Mongi
APRIL 23, mwaka huu kampuni ya sukari ya TPC iliyopo wilayani Moshi
mkoani Kilimanjaro, itatimiza miaka miwili tangu iliposaini mkataba wa
hali bora za wafanyakazi na chama cha wafanyakazi wa huduma za jamii
Tanzania (TASIWU), ikiwa ni hatua kubwa ya kumaliza mgogoro wa wafanyakazi uliodumu kwa zaidi ya miaka sita kiwandani hapo.
Matonya:Msanii wa bongo fleva aliyegeukia biashara *Ajenga hoteli ya Kifahari Tanga
Na Victor Mkumbo
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Seif Shaban 'Matonya', ni mmoja wa wasanii wachache wenye mafanikio ambayo kwa njia moja au nyingine ni mfano wa kuigwa kwa wengine walioko kwenye tasnia hiyo.
Kumekuwa na wasanii mbalimbali ambao wanapata umaarufu mkubwa, lakini hawana maendeleo.
Kizimbani kwa ubakaji
Mohamed Mohamed na
Happy Julius.
MKAZI wa Mbagala Kingugi Dar es Salaam Bw. Salum Ramadhani (42) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma ya ubakaji.
Mbele ya Hakimu Bw. Karim Mushi ilidaiwa na mwendesha mashtaka Bi.Honorina Munishi kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya mwaka 2009 na Julai mwaka huu katika maeneo ya Kariakoo.
Selasini awalipua wabunge mafisadi *Adai wamehongwa pesa na kampuni za mafuta *Wapo wa CCM, CHADEMA, Mnyika alipuka
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Rombo, mkoani Kilimanjaro Bw. Joseph Selasini (CHADEMA), jana alikuchua makucha na kuwalipua baadhi ya wabunge kwa madai ya kura rushwa kutoka kwa wamiliki wa kampuni binafsi za mafuta.
Zanzibar kununua meli ya kisasa *Itabeba abiria 1,000, mizigo tani 100
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, ameiagiza Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, kuandaa utaratibu wa kupata fedha ndani ya wiki moja ili kununua meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 1,000 na mizigo tani 100.
Wateja wa TANESCO wasikilizwa
Na Benedict Kaguo, Dodoma
SERIKALI imepunguza gharama za kuunganisha umeme ambapo kuanzia Januari 2013, wateja ambao watataka kuvutiwa umeme na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), watalipia sh. 177,000, badala ya sh. 455,000 wanazolipia sasa.
John Komba afanyiwa upasuaji
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Mbinga Magharibi, mkoani Ruvuma, Bw. John Komba amefanyiwa upasuaji wa nyonga nchini India ambayo ilikuwa ikimsumbua katika mguu wa kulia.
Bw. Komba ambaye amerejea nchini jana, amedai kusikitishwa na taarifa zinazodai alikuwa mahututi.
WALIMU
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw. Ezekiel O'luoch, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam juzi, kuhusu msimamo wa walimu kufanya mgomo baada ya kutoafikiana na Serikali katika madai ya malimbikizo ya mishahara yao. Kushoto ni Mwekahazina, Bw. Mohamed Utaly na Rais wa Chama hicho, Bw. Gratian Mukoba. (Picha na Charles Lucas)
CWT yatoa notisi saa 48 za mgomo serikalini
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, jana imepokea notisi ya saa 48 inayohusu kusudio la walimu ambao ni wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kugoma kuanzia Julai 30 mwaka huu, saa moja na nusu asubuhi.
Diamond kuibukia kwenye taarab
BAADA ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, msanii nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond’ amesema anafikiria kujitosa katika muziki wa taarab.
Diamond alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, amefikia uamuzi huo kutokana na kuvutiwa na muziki huo wa taarab.
Shindano la Maisha Plus 2012 kuja na sura mpya *Kipanya aomba sapoti kwa Watanzania kulifanikisha
Na Amina Athumani
KATI ya mashindano mbalimbali yanayoendeshwa hapa nchini shindano la Maisha Plus ambalo huendeshwa kwa kuoneshwa katika televisheni, limekuwa likiteka hisia mbalimbali za Watanzania hasa jinsi lilivyo na muonekano tofauti na mashindano mengine.
Wanne washinda vuta mkwanja Moshi
Na Mwandishi Wetu, Moshi
KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca-Cola ya Bonite leo imewazawadia washindi nane wa promosheni ya Vuta Mkwanja ambao wemeweza kushinda zawadi na fedha taslimu.
Tukio la kukabidhi zawadi hizo limefanyika jana katika kiwanda cha Bonite Bottlers mjini Moshi.
Washindi hao ni Joseph Gerald ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha SAUT na Diana Thadeo, muuza duka mjini Moshi, ambao wote kila mmoja amejishindia zawadi ya sh.milioni moja.
Wanamichezo kupewa ofa Quality Centre
Na Amina Athumani
WANAMICHEZO watakaofika katika maduka ya Fun Sport yaliyopo Quality Centre iliyopo barabara ya Nyerere, Dar es Salaam watapewa ofa ya kununua vitu mbalimbali kwa punguzo la asilimia 50.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Meneja Habari kwa Umma, Atuphy Mwaijengo ilieleza kwamba ofa ni maalumu kwa ajili ya mwezi huu wa mfungo wa Ramadhan.
Azam FC: Haituumizi Ngassa kushangilia Yanga
Na Mwali Ibrahim
KLABU ya Azam imedai kutokushtushwa na kitendo cha mchezaji wao Mrisho Ngassa kushangilia bao la timu yake ya awali ya Yanga lilowapeleka fainali.
Ngassa alionekana kushangilia goli walilofunga Yanga na pia alivaa jezi ya timu hiyo na kuwashangilia ikiwa ni kuonesha mapenzi yake na timu hiyo na hata kuripotiwa kutaka kurudi katika timu hiyo.
MASHABIKI WA YANGA
Mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yao wakati wa mechi ya nusu fainali, ambapo Yanga walicheza na APR ya Rwanda na kuifunga bao 1-0. (Picha na Imma Mbuguni)
Yanga kutwaa taji la tano, Azam la kwanza *Bahanuzi, Bocco, Kiiza mvutano
Na Zahoro Mlanzi
KATIKA siku ambazo mashabiki na wadau wa soka hawatotulia sehemu moja wakisubiri muda ufike basi ni leo, ambapo mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame, timu ya Yanga itaumana na Azam FC katika fainali ya aina yake itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
27 July 2012
Mbatia afichua ufisadi Tanesco *Aeleza madudu ya Mhando, aonesha mkataba wake *Siri wabunge CCM kumng'oa Waziri sasa yafichuka
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, jana ameibua ufisadi wa kutisha wa ununuzi mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL na kudai baadhi ya wabunge walihongwa ili kumtetea aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. William Mhando.
Sheria mifuko ya hifadhi sasa mwiba mkali
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MBUNGE wa Mwibara, mkoani Mara, Bw. Kangi Lugola (CCM), amewalipua wabunge waliopitisha sheria kandamizi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kurejea kauli yake kuwa, chombo hicho hakiko makini kwenye kutunga na kupitisha sheria.
Mgomo wa walimu sasa wanukia *Unaratibiwa na CWT, kura zaanza kupigwa
Na Reuben Kagaruki, Kagera
SERIKALI imeshindwa kufikia muafaka na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), juu ya madai yao kupitia Tume ya Usuluhishi ambapo hivi sasa wanachama wa chama hicho wameanza kupewa barua ili wajiandae kwa mgomo baada ya taratibu kukamilika.
SMZ yafungia meli 3 ikiwemo Seagull, Sepideh
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imezifutia usajili meli tatu kutofanya shughuli za usafiri ndani ya Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), Bw. Abdallah Hussein Kombo, aliyasema hayo Malindi jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Ajinyonga akidai wazazi wanamfuatilia
Na Theonestina Juma, Bukoba
MWANAFUNZI Mtanzania aliyekuwa akisoma Kidato cha Sita nchini Uganda, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba akidai kuchoshwa na tabia ya wazazi wake kufuatilia maisha yake.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Phillip Kalangi, ambaye alisema limetokea katika Mtaa wa Kashenye, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera.
HUNDI
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Bw. Charles Singili (Kulia) akimkabidhi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, hundi ya sh. milioni 65, za kuboresha nyumba za Kata ya Mazense Mvuleni, wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam hivi karibuni. (Picha na Heri Shaaban)
Uturuki sasa kumaliza kero ya mgawo
Na Stella Aron
MGAWO wa umeme nchini, unaweza kusahaulika na kubaki historia baada ya wajumbe wa kampuni kubwa 16 kutoka nchini Uturuki ambazo zinahusika na uzalishaji nishati hiyo, kuwasili nchini ili kubadilishana mawazo na sekta nyingine.
Mgomo wa daladala batili-SUMATRA
Na Agnes Mwaijega
BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (SUMATRA-CCC), limesema mgomo wa daladala uliotangazwa na Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa (DARCOBOA) ni batili.
Tamko hilo limekuja siku moja baaada ya DARCOBOA, kutangaza mgomo wa kutosafirisha abiria kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa madai ya kupinga manyanyaso wanayofanyiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA).
HAKI
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu, Dkt. Hellen Kijo Bisimba, akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam juzi, wakati wa uzinduzi wa ripoti ya nusu mwaka ya hali ya haki za binadamu nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo na Uwezeshaji, Bi. Imelda Urio.(Picha na Dorin Mchau)
Ugumu wa maisha kuongezeka nchini
Na Mwandishi Wetu, Mashirika ya habari
HALI ngumu ya maisha inayowakabili Watanzania wengi nchini, huenda ikaongezeka zaidi ya ilivyo sasa.
Hali hiyo inadaiwa kuchangiwa na tofauti kubwa ya pato la Taifa nchini hadi kufikia asilimia 15 ya pato la jumla mwaka 2011/12 kutokana na kupanda kwa uagizaji mafuta na gesi kutoka nje.
Kizimbani kwa kutoa vyeti vya uuguzi, ukunga
Na Rehema Mohamed
MKAZI wa Tabata Bi. Veronica Danford (44), jana amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa makosa mawili ambayo ni kujivika utu na kutoa vyeti vya uuguzi na ukunga vyenye majina ya mtu mwingine.
Morani wadaiwa kumuua Meneja Mgodi wa Ruby Longindo.
Na Mwandishi Wetu, Longido
VIJANA wa Kimasai (Morani) zaidi ya 500 kwenye kata ya Engerenaibor, iliyopo Wilaya ya Longido, mkoani Arusha, wanadaiwa kumuua Meneja wa Mgodi wa Madini aina ya Ruby, uliopo Mundarara Ruby Mining Company Ltd, Bw. Omary Shengovi (49), kwa kumchoma moto.
VIJANA wa Kimasai (Morani) zaidi ya 500 kwenye kata ya Engerenaibor, iliyopo Wilaya ya Longido, mkoani Arusha, wanadaiwa kumuua Meneja wa Mgodi wa Madini aina ya Ruby, uliopo Mundarara Ruby Mining Company Ltd, Bw. Omary Shengovi (49), kwa kumchoma moto.
Uhaba wa vifaa wachangia taka kuzagaa Dar
Na Rehema Maigala
TATIZO la uhaba wa vifaa vya kuzolea taka katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam, unachangia jiji hilo kuwa chafu.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, katika warsha ya kupata mawazo ya wadau mbalimbali wa mazingira ili kuwezesha jiji hilo kuwa safi, Kaimu Mkuu wa Udhibiti Taka mkoani humo, Bw. Protus Membe, alisema jiji hilo lina uhaba wa vifaa vya kuzolea taka kwa asilimia 94, pamoja na magari 42 ya kuminya taka.
UWEZESHAJI
Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Nicholas Brooks (kushoto), akizungumza na mawakala wa mauzo ya bidhaa za kampuni hiyo, kutoka mikoa ya wenyeji Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Morogoro, Lindi, Pwani na Mtwara, wakati wa mkutano wa kuwajengea uwezo, uliofanyika Dar es Salaam juzi. (Picha na Anna Titus)
Wakulima Kondoa wapewa matrekta na diwani wao
Na Darlin Said
WAKULIMA wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma, wamekabidhiwa matrekta manne yenye thamani ya sh. millioni 80 kutoka kwa Diwani wa kata hiyo, Alhaji Omari Kariati.
Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salaam jana, katika ofisi za Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT), ikiwa ni mkakati wa kuendeleza sera ya Kilimo Kwanza.
Iundwe mamlaka ya usimamizi vyombo vya majini -Mwaibula
Na Rose Itono
WITO umetolewa kwa Serikali kuunda mamlaka maalumu ya kusimamia masuala yote yanayohusu vyombo vya majini ili kupunguza tatizo la majanga yanayotokea mara kwa mara na kupoteza nguvu kazi kubwa ya Taifa.
Mdau wa sekta ya usafiri Bw. David Mwaibula aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati mada inayosema “Watanzania tumekubali kuwa Taifa la majanga”, katika kipindi cha Five Connection kinachorushwa na televisheni ya EATV.
Halmashauri kutegemea wakala kukusanya kodi kikwazo serikali kuendesha shughuli kwa kujitegemea.
Na Willbroad Mathias
SERIKALI ya Tanzania ni kati ya serikali za kiafrika ambazo kwa kiasi kikubwa zinategemea kuendesha shughuli zake za maendeleo kutoka kwa wafadhili mbalimbali wa nchi za Magharibi.
Hali hii inatokana na kasumba iliyojengeka kwamba nchi nyingi za kiafrika bado hazina uwezo wa kujiendesha zenyewe bila kupata msaada kutoka nje ya nchi.
MKATABA
Mkurugenzi wa Masoko na Matukio wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jimmy Kabwe akisaini mkataba wa makubaliano ya udhamini wa michuano ya Super 8, inayodhaminiwa na benki ya ABC (kulia) ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah, Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Boni Nyoni na Mkuu wa Idara ya fedha ya benki hiyo, Mwalimu Zubery. Picha na blogu ya dinaismail
Simba kufanya usajili upya
Na Elizabeth Mayemba
BAADA ya timu ya Simba kuondolewa katika michuano ya Kombe la Kagame na Azam FC hatua ya robo fainali, uongozi wa klabu hiyo umepanga kuongeza wachezaji wengine katika kikosi hicho.
Akizungumza na gazeti hili mmoja wa viongozi wa Simba ambaye yumo katika Kamati ya Usajili, alisema timu ina upungufu katika nafasi ya beki wa kulia, kushoto na wa kati kwa kuwa waliopo sasa nafasi ya kati aina yao ya uchezaji unafanana.
Uzalendo unahitajika kusimamia uchimbaji gesi- Killagane
Na Cornel Antony
MATUMIZI mabaya ya rasilimali ni moja ya kikwazo cha maendeleo katika nchi zinazoendelea.
Licha ya kuwa kipimo cha utajili wa Taifa ambao husaidia kuongeza fedha za kigeni, usimamizi wake umekuwa ukisuasua huku wachache wakinufaika nazo.
TFF kuzichonganisha Simba, Yanga, Azam
Na Amina Athumani
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeanza michuano mingine ya Super 8 kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza, ambayo itazikutanisha timu za Simba, Azam FC na Yanga ambazo zilishika nafasi tatu za juu katika ligi.
Yanga, Azam FC patachimbika kesho *Kiiza aipeleka fainali *Mtoto hatumwi sokoni
Na Speciroza Joseph
MABINGWA watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga jana ilipenya hatua ya fainali baada ya kuifunga APR ya Rwanda bao 1-0 katika mechi ya nusu ya fainali ya michuano hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
26 July 2012
SIKU YA MASHUJAA
Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita ya ukombozi dhidi ya wakoloni, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
Daladala Dar kugoma rasmi wiki ijayo
Na Heri Shaaban
CHAMA cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA), kimetangaza kuanza mgomo kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayofanyiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) wa kuzikamata bila utaratibu.
Upelelezi kesi kesi ya Dkt. Ulimboka bado
Na Rehema Mohamed
UPANDE wa Mashtaka katika kesi ya kumteka na kutaka kumuua Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Dkt. Steven Ulimboka, umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Kesi hiyo ambayo inamkabili raia wa Kenya Bw. Joshua Mulundi (21) jana ililetwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dar es Salaam kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Agnes Mchome.
MAADHIMISHO
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Bw. Pandu Ameir Kificho, akifurahia na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mstahiki, Dkt. Didas Masaburi (kushoto), mara baada ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jana. (Picha na Charles Lucas)
JK aongoza mamia Dar Siku ya Mashujaa
Na Goodluck Hongo
RAIS Jakaya Kikwete, jana aliongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.
Maadhimisho hayo hufanyika Julai 25 kila mwakakila mwaka ambapo watu mbalimbali walihudhuria wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini.
Muuza nyama ajisaidia chupa 12 za mikojo buchani
Na Patrick Mabula, Kahama
MFANYABIASHARA anayeuza nyama katika bucha iliyopo mjini Kahama, mkoani Shinyanga, Bw. Said Mayala, amekamatwa baada kukutwa na mkojo chupa 12, iliyowekwa kwenye chupa za ujazo wa lita 1.5,.
Tukio hilo limetokea juzi baada ya kukutwa na Maofisa Afya wa Halmashauri ya mji huo katika Soko Kuu akiwa na chupa hizo ambazo alizitumia kujisaidia haja ndogo ndani ya bucha.
Kizimbani kwa kutakatisha sh. milioni 776
Na Rehema Mohamed
MKAZI wa Ilala, Dar es Salaaam, Bw. Inock Kantelu, jana amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kutakatisha fedha zaidi ya sh. milioni 776.
Wana Tanga waandaa mkutano Dar kujadili mambo mbalimbali
Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa Dar es Salaam waliozaliwa mkoani Tanga, wanatarajia kukutana wiki ijayo kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Mkoa huo likiwemo suala la kushuka kwa maendeleo ya sekta mbalimbali hivyo kukwamisha maendeleo.
USHIRIKIANO
TRA kutoa mafunzo ya ukusanyaji kodi
Na Salim Nyomolelo
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), inatarajia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake ili waweze kukabiliana na mabadiliko ya ukusanyaji kodi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Harry Kitillya mafunzo hayo yatatolewa kwa ushirikiano wa mamlaka hiyo na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA).
Kesi wizi wa nyara Kibiti kusikilizwa Agosti 22
Na Rose Itono, Pwani
MAHAKAMA ya Kibiti, iliyopo Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani, Agosti 22 mwaka huu, itaanza kusikiliza kesi ya kupatikana na nyara za Serikali inayomkabili mwendesha pikipiki 'bodaboda', Bw. Jumanne Ligenge na wenzake watano.
KIVUTIO
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw.Harry Kitillya, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana, kuhusu kuanzishwa kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), katika Mradi wa Kuboresha Ukusanyaji Kodi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni. (Picha na Angelina Mganga)
SUMATRA yaigomea TPA kupandisha tozo
Na Anneth Kagenda
BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA-CCC), limeigomea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kuhusu ombi lao la kuongeza tozo mbalimbali za kuhudumia meli.
Mradi wa uboreshaji makazi Manzese wamgusa Tibaijuka
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amesema miradi ya uboreshaji makazi nchini haiwezi kufanikiwa bila kushirikisha sekta za kibenki kwani wananchi hawawezi kununua kwa fedha kutoka mifukoni mwao.
Ukataji tiketi kwa njia ya simu utapunguza ulanguzi kwa abiria
Na Salim Nyomolelo
MAENDELEO ya Teknolojia yamerahisisha huduma za jamii ikiwemo mawasiliano ya simu yanayounganisha watu sehemu mbalimbali nchini.
Awali mawasiliano yalitumia barua ambayo ilichukua muda mrefu kumfikia mlengwa na kupata mrejesho.
Uchimbaji madini unufaishe wazawa
HIVI karibuni, washiriki wa mkutano wa 16 uliohusisha wataalamu wa masuala ya uchumi na madini, walijadili kwa kina umuhimu wa sekta hiyo kunufaisha wazawa.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini, uliandaliwa na Umoja wa Umoja wa Mataifa (UN), ili kupitia kanuni za uchimbaji madini yasitumike kibiashara pekee na kusafirishwa nje ya nchi bali yanufaishe wananchi.
UZINDUZI
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi. Eugen Mwaiposa na Mratibu wa Mfuko wa Urafiki na Mshikamano (REHEMA), Bw. Mohamed Potea wakimtwisha ndoo yenye maji Bi.Eshe Mohamed, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima kirefu kilichochimbwa na mfuko huo eneo la Pugu Mpakani. (Picha na Peter Mwenda)
Hukumu kesi ya Mtikila Agosti 27
Na Rehema Mohamed
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kutoa hukumu ya kesi ya kuchapisha na kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila Agosti 27 mwaka huu.
ALAT yasikitishwa na ung'olewaji wa viongozi halmashauri
Na Mwandishi Wetu
JUMUIYA ya Tawala za Mitaa na Tanzania (ALAT),imesikitishwa na mtindo unaotumika kuwang'oa viongozi wa Halmashauri kwa kuwatuhumu kwa kutumia utaratibu ambao ni kinyume cha sheria.
Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Dkt.Didas Masaburi alisema wamepokea taarifa za vurugu katika Halmashauri mbalimbali nchini hivyo ingependa kuona zinaendeshwa kwa kuzingatia utawala bora na utawala wa sheria na haki.
Musonye:Timu kongwe zinacheza kimazoea Kagame
Na Andrew Ignas
KATIBU Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye amesema klabu nyingi kongwe zimetupwa nje ya mashindano ya Kagame kutokana na kucheza mpira wa kimazoea.
Flying Eagles wawasili kuivaa Ngorongoro J.pili
Na Janath Abdulahim
TIMU ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Nigeria (Flying Eagles) imewasili nchini jana kwa ajili ya mechi yao ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za 18 za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazochezwa mwakani nchini Algeria.
Wadau: Uwanja wa Majimaji unatia kichefuchefu
Na Mhaiki Andrew, Songea
WAPENZI na mashabiki wa soka mkoani Ruvuma wamelalamikia ubovu wa uwanja wa Majimaji kutokana na wamiliki wake ambao ni Chama chaMapinduzi(CCM), kushindwa kuufanyia matengenezo huku wakiendelea kuchukua ushuru wa uwanja huo na pango la vyumba vya uwanja kila mwezi.
Mchumiatumbo kuzichapa na Zola D Idd El Fitri
Na Peter Mwenda
MABONDIA Alphonce Joseph (Mchumiatumbo) na David Michael Mlope (Zola D – King) watapambana katika Tamasha la Watani wa Jadi litakalofanyika katika Sikukuu ya Idd El Fitri kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari Temeke.
BONDIA AKISAINI MKATABA
Bondia David Mlope maarufu kama Zola D King (kushoto) akisaini mkataba wa pambano lake na mpinzani wake Alphonce Mchumiatumbo (kulia)litakalofanyika Sikukuu ya Eid El Fitri katika uwanja wa Bandari Temeke anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib. (Picha Peter Mwenda)
Yanga, APR gharika leo Kagame
Na Elizabeth Mayemba
MABINGWA watetezi wa Kombe la Kagame Yanga leo wanashuka uwanjani kumenyana na APR ya Rwanda katika nusu fainali ya michuano hiyo ya Kagame, mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa kuanzia saa 10 jioni.
Mkutano Mkuu Simba Agosti 5 *TBL yawapa sh.milioni 20
Na Zahoro Mlanzi
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Lager jana ilikabidhi hundi ya sh.milioni 20 kwa klabu ya Simba kwa ajili ya Mkutano wake Mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 5, mwaka huu.
MKURUGENZI WA BIA (TBL) AKIKABIDHI HUNDI.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Masuala ya Sheria wa Kampuni ya Bia (TBL), Bw. Stephen Kilindo (kulia) akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange (kushoto) hundi ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Agosti 5, mwaka huu. Wanaoshuhudia ni George Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wadhamini wakuu wa klabu hiyo na Katibu wa Simba, Evodius Mtawala.
Chakula chenye sumu chaua mmoja, wengine mahututi
Na Eliasa Ally, Iringa
MKAZI wa Kijiji cha Ibofye, Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa Bw. Faruni Nyaupumbwe (65), amefariki dunia na wengine zaidi ya 10 wamelazwa katika Hospitali za Mkoa wa Iringa na Kituo cha Afya Ihambo baada ya kula chakula chenye sumu katika sherehe.
Waislamu kuweni wanyenyekevu'
Na David John
MKURUGENZI wa Kituo cha Utamaduni cha Irani, Bw. Morteza Sabouri, amewataka waumini wa Kiislamu kujenga tabia ya kuwa karibu na Mwenyezi Mungu kila wakati badala ya kusubiri mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
JK atuma zsalamu za pongezi India
Na Willbroad Mathias
RAIS wa Jakaya Kikwete, amemtumia salamu za pongezi Rais wa India, Bw. Prunab Murkjee, kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi wa 13 wa Taifa hilo.
Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo habari Dar es Salaam jana, ilisema Rais Kikwete amempongeza kwa dhati Bw. Murkjee baada ya kuibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu nchini humo.
Maliasili: Hatujakalia ripoti yoyote
Na Stella Aron
WIZARA ya Maliasili na Utalii, imesema hakuna ripoti ya wanyama ambayo imekaliwa na Wizara hiyo kuhusu suala la uchunguzi wa tuhuma za watumishi wanaodaiwa kuhusika na utoroshaji wanyama kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Makalla: Wizara kukamilisha sera maendeleo ya michezo
SERIKALI katika mwaka wa fedha 2012/13, inatarajia kukamilisha Marekebisho yanayohusu Sera ya Maendeleo ya Michezo toleo la mwaka 1995.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. Amos Makalla, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Bw. Idd Azzan (CCM).
Mbunge ataka ufafanuzi madini yanayochimba, kufanyiwa tafiti
MBUNGE wa Muhambwe, Bw. Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), ameitaka Serikali kueleza kiasi cha madini yaliyochimbwa katika tafiti mbalimbali, baada ya kuchimbwa yamepelekwa wapi na Serikali imechukua hatua gani kuhakikisha hayaibiwi.
Japan imetoa msaada kubwa wa mchele nchini - Serikali
SERIKALI ya Japan, imekuwa ikitoa msaada wa mchele kwa Tanzania tangu mwaka 1979.
Kwa mjibu wa takwimu zilizopo toka mwaka 1992 hadi 2011, mchele uliotolewa na Japani ni tani 183,366.92, sawa na fedha za Kijapan bilioni 7.770.
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Adam Malima, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde, Bw. Katib Said Haji (CUF).
Mil. 56.3/- zatengwa kukamilisha miundombinu shule za sekondari
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imesema mwaka wa fedha 2012/13, Serikali kupitia Mpango wa Elimu ya Sekondari (MMES II), imetenga sh. bilioni 56.3, kwa ajili ya kukamilisha miundombinu ya shule 264.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Bw. Philipo Mulugo, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Bi. Susan Lyimo (CHADEMA).
Walimu wadanganyifu katika mitihani kuchukuliwa hatua
SERIKALI imetangaza kuchukua hatua za kisheria kwa walimu ambao wanajihusisha na vitendo vya udanganyifu wa matokeo ya mitihani ya darasa la saba.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Ngara, Bw. Deogratiaa Ntukamazina (CCM).
Tunakwama wapi kukomesha mimba kwa wanafunzi
TATIZO la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini, linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu.
Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinathibitisha kuwa tatizo hili limekuwa likiongezeka siku hadi siku hasa baada ya kuanzishwa kwa shule za kata.
Pamoja na shule hizo kupunguza tatizo la wanafunzi kukosa nafasi za masomo, bado zinakabiliwa na changamoto.
Wazazi watakiwa kuziheshimu, kuzithamini shule za kawaida
Na Anneth Kagenda
WITO umetolewa kwa wazazi nchini kutozidharau shule zinazotoa elimu ya kawaida na kukimbilia shule za kimataifa badala yake wanapaswa kuziheshimu kutokana na juhudi zinazofanyika kuhakikisha zinapata vifaa vyote vya muhimu vikiwamo vitabu.
VITABU
Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Business Printers Limited (BPL), Idara ya Uchapishaji Vitabu, Bw.Christian Gaya (wa tatu kushoto), akikabidhi vitabu 903 vilivyochapwa na kampuni hiyo kwa Rais wa Taasisi ya Kilimanjaro Education Outreach (KILEO), Bw. Waltel Miya (kulia), ambaye aliongozana na mwanzilishi wa taasisi hiyo Bi. Shawn Miya (wa pili kulia), ambavyo vitapelekwa katika Shule ya Msingi Kotela, iliyopo Marangu, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. (Picha na Prona Mumwi)
Serikali yashirikisha asasi binafsi kuboresha huduma
Darlin Said na Angelina Mganga
SERIKALI imeanza mchakato wa kushirikisha asasi zisizo za kiserikali kuboresha huduma kwa umma na kusaidia kuelimisha wananchi ili wadai haki zao na huduma bora.
Naibu Katibu Mkuu Utumishi, Bw. Hab Mkwizu, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano ulioshirikisha Serikali na asasi zisizo za kiserikali na kusisitiza kuwa, lengo ni kuimarisha uwajibikaji katika sekta za umma.
CHADEMA yavuna 256 Kilomero
Na Rehema Maigala
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro, kimevuna wanachama wapya 256, waliohamia chama hicho kutoka vyama vingine vya siasa.
Wanachama hao wametoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), na Tanzania Labour Party (TLP), ambao walirudisha kadi zao kwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (BAVICHA), Bw. John Heche, alipokuwa jimboni humo kwenye ziara ya muendelezo wa vuguvugu la mabadiliko M4C.
Wassira kufungua kituo cha kimataifa kupunguza umaskini
Na Grace Ndossa
WAZIRI wa Nchi Mahusiano na Utaratibu Bw. Stephen Wassira, leo anatarajia kuzindua Kituo cha Kimataifa cha Kupunguza Umaskini nchini ambacho kimejengwa na Serikali ya China.
Katika uzinduzi huo, Bw. Wassira atakuwa na Waziri Ofisi wa Serikali ya Jamhuri ya china Bw. Fan Xiaojian ambapo taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema Mawaziri hao watatilian saini kama ishara ya ushirikiano.
Mgombea ubunge apeleka malalamiko kwa Kikwete
Na Agnes Mwaijega
ALIYEKUWA mgombea wa ubunge katika Uhaguzi Mkuu 2010, Jimbo la Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro, kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. Faustime Sungura, amewaandikia barua ya malalamiko viongozi wa Serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete.
24 July 2012
Kukamilika awamu ya pili mkongo wa Taifa kutasaidia mawasilino-Prof Mbarawa
Na Darlin Said
UWAJIBIKAJI ni majukumu yanayotakiwa kufanywa na watawala na wataliwa ili kuwa na maendeleo endelevu.
Viongozi wana wajibu wao kama watawala na wananchi wana wajibu wao kama watawaliwa ambayo hutegemeana ili kufanikisha malengo yaliyowekwa.
Soko la uhakika changamoto kilimo cha matunda nchini
Na Daniel Samson
SHAMBA darasa ni mbinu ya kuandaa utaalamu katika kata na kijiji, miongoni mwa wakulima kwa kutumia ujuzi unaopatikana kupitia mafunzo shirikishi ili kuongeza uzalishaji.
Pia, imesaidia kuwapatia wakulima mbinu za kilimo bora kwa kufuata mfano wa wataalamu wa kilimo wakitumia zao maalumu.
Wanunuzi wadogo walivyosaidia kuinua kipato cha wakulima wa pareto nchini
Na Rashid Mkwinda
MKAKATI wa kumkomboa mkulima kunufaika na kilimo kwa kujikita na kilimo cha kisasa utasaidia kupunguza umaskini.
Pia imepania kukuza uchumi na kusaidia ongezeko la kipato kwa wakulima kwa nia ya kufuta umaskini kuegemea katika kilimo cha kibiashara hatimaye kuelekeza nguvu kwenye sekta ya viwanda inayohudumia kilimo.
Mbato Cup kuanza kutimua vumbi Agosti
Na Omary Mngindo, Bagamoyo
MICHUANO ya kuwania kombe la Diwani Shukuru Mbato (Mbato Cup) Kata ya Pera Bagamoyo, Pwani inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Diwani Mbato kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Pingo ambapo alisema michuano hiyo itafanyika mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Tukuyu Stars sasa imeanza kukamilika
Na Janath Abdulrahimu
JUHUDI za kuifufua Tukuyu stars zimeendelea katika kata na tarafa mbalimbali za jiji la Mbeya na mpaka sasa wapo katika hatua ya nusu fainali kwa ajili ya kupata wachezaji wa kuunda timu hiyo.
Akizungumza Dar es salaam jana Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo Peter Mwambuja alisema lengo la kuifufua timu hiyo ni kubadilisha mpira wa Tanzania uwe katika sura ya mpira wa zamani, kwa kuzalisha wachezaji wenye nidhamu na uwezo mkubwa wawapo uwanjani.
Pugu mabingwa kombe la Stakishari
Na Heri Shaaban
TIMU ya soka ya Kata Pugu imeibuka mabingwa wa mashindano ya Polisi Jamii katika fainali ya kugombea kombe la Stakishari Ukonga, Wilayani Ilala.
Katika fainali hiyo mshindi wa pili ni timu ya Kata Chanika na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Segerea.
ZAWADI
Upendo yaizaba Ambassadors mabao 7-0
Na Damiano Mkumbo, Singida
TIMU ya soka ya watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Upendo mjini hapa imewachapa wenzao wa Shirika la Youth Ambassadors mabao 7-1.
Mechi hiyo iliyopigwa juzi katika Uwanja wa Chuo cha VETA, ilikuwa na msisimko kutokana na kandanda walilokuwa wakicheza wachezaji wa timu hizo.
23 July 2012
Padri alishukia Bunge, serikali *Adai nchi inaelekea kubaya kutokana na ubinafsi *Alalamikia Bunge kupendelea wabunge wa CCM *Asema yeye ni nabii, yupo tayari kupigwa mawe
Na Anneth Kagenda
MKURUGENZI wa Shirika la Familia la Farijika Afrika Mashariki, Padri Baptisti Mapunda, ameishukia Serikali na kudai Tanzania inaelekea kubaya kutokana na viongozi wake kufanya uozo bila kuchukuliwa hatua.
Mmiliki Mv Skagit, nahodha mbaroni *Maiti nyingine tano zaopolewa, sasa zafikia 73
Na Mohammed Mhina, Jeshi la Polisi-Zanzibar
JESHI la Polisi Zanzibar, linawashikilia wafanyakazi sita wa meli ya Mv Skagit akiwemo mmiliki wake Bw. Said Abdulrahman pamoja na Nahodha wa meli hiyo, Bw. Mussa Makame Mussa.
SWALAA
Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa tatu kushoto), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein (wa nne kushoto) na baadhi ya Viongozi Serikali wakishiriki Swala ya kuwaombea Dua Abiria waliopoteza maisha wakati wa ajali ya Meli Mv. Skagit, iliyozama hivi karibuni. Swala hiyo iliongozwa na Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabi, kwenye Msikiti wa Mwembeshauri, Mjini Unguja jana. (Picha na Muhidin Sufian OMR)
Subscribe to:
Posts (Atom)
