30 July 2012
Majimarefu awataka wapiga kura kuwapuuza wapinzani Na Mashaka Mhando, Korogwe
MBUNGE wa Korogwe Vijijini, mkoani Tanga Bw. Stephen Ngonyani, maarufu 'Profesa Majimarefu', amewata wapiga kura jimboni humo kupuuza maneno ya wapinzani wake kisiasa wanaodai wamekosea kumpa mbunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwenye atika Kijiji cha Kwashemshi, Bw. Ngonyani alisema kuna watu wanapita katika jimbo hilo wakioshirikiana na baadhi ya madiwani kudai wannchi walikosea kumchagua ili kuwa mbunge wao.
“Tangu nimekuwa mbunge wa jimbo hili, tayari nimetumia zaidi ya sh. milioni 118 za Mfuko wa Jimbo kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, wenzangu walionitangulia hawajawahi kutumia fedha hizi kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Kama nimefanya makosa kwenu, nyie ndiyo mtakaoniadhibu, hawa wanaopita kwenu na kusema mmekosea kunichagua, wanapata wapi ujasiri huu, kwanini hawasemi mmekosea kwenye nini wakati nimekuwa nikisadia shughuli nyingi za maendeleo nyingi,” alisema.
Alisema katika kata hiyo pekee ameweza kutumia sh. milioni 6.2 ambapo kati ya hizo, sh. milioni 2.8 zimetumika kwa ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Mgila A, kwa kutoa mifuko 80 ya saruji 80 na gharama za fundi.
Aliongeza kuwa, sh. milioni 2 zimetumika kumalizia nyumba ya mwalimu wa Shule ya Msingi Miembeni kwa kutoa bati, saruji na gharama ya usafirishaji ambapo mwaka huu, tayari ametoa sh. milioni 2,230,000 ili kusaidia ujenzi wa madarsa na ofisi ya walimu Shule ya Msingi Mgila A.
Bw. Ngonyani aliongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Mrisho Gambo ambaye kabla ya mkutano huo, alimtembeza kuona uchafuzi wa maji katika mto uliopo kijijini hapo ambayo hutumika kwa mahitaji ya nyumbani lakini hivi sasa yamechafuliwa kutokana na shughuli za madini zinaoendelea juu ya milima.
“Mheshimiwa Mbunge, naamini ilani ya CCM unaitekeleza kwa vitendo, suala hili la maji tutahakikisha tunalifuatilia ili kuwabaini wachafuzi wachukuliwe hatua,” alisema Bw. Gambo.
Pia Bw. Gambo hakuridhishwa na maelezo yanayosema choo kilichopo katika Soko la Kwashemshi ambacho alioneshwa Bw. Ngonyani kimetumia mifuko 30 ya saruji wakati jengo lake ni dogo na kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wilayani humo ifanye uchunguzi kubaini gharama halisi za ujenzi wa choo hicho na nyumba ya mwalimu wa Shule ya Msingi Miembeni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment