31 July 2012

Azam yamuweka sokoni Ngassa


Na Zahoro Mlanzi

HATIMAYE Klabu ya Azam FC, imekubali kumruhusu kiungo wao, Mrisho Ngassa kujiunga na timu yoyote kwa dau la dola 50,000 baada ya kuonekana kiungo huyo kutokuwa na mapenzi na timu hiyo.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Ngassa kuonesha dhahiri mapenzi yake kwa mabingwa wa Kombe la Kagame, Yanga kwa kuibusu jezi ya timu hiyo baada ya kuifungia Azam bao la pili lililoipeleka fainali ya michuano hiyo.


Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana Dar es Salaam jana na Mmoja wa viongozi wa timu hiyo, zilieleza kwamba Ngassa ana mapenzi tena na Azam na ndio maana wameamua kumuweka sokoni.

"Klabu ya Azam imechoka na na vitendo vya Ngassa, hivyo imeamua kufungua milango kwa timu yoyote inayomuhitaji kufanya nao mazungumzo kwa gharama zisizopungua dola 50,0000," kilisema chanzo hicho ambacho hakikupenda kutajwa jina lake.

Kingozi huyo alidai, timu yao ilitoa nafasi ya upendeleo kwa Yanga lakini hakuna ofa iliyoletwa ila walipokea ofa kutoka kwa Simba ikimuhitaji mchezaji huyo.

Alidai mbali na tukio hilo, Ngassa pia alikuwa haoneshi ushirikiano wa aina yoyote na wachezaji wenzake hususani wakati mazoezi.

Aliongeza na ndio maana Kocha Mkuu, Stewart Hall alikuwa hamchezeshi mpaka uongozi wa juu ulipoingilia kati na kuamuliwa ni bora abakie kumalizia mkataba wake.

No comments:

Post a Comment