26 July 2012
Musonye:Timu kongwe zinacheza kimazoea Kagame
Na Andrew Ignas
KATIBU Mkuu wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye amesema klabu nyingi kongwe zimetupwa nje ya mashindano ya Kagame kutokana na kucheza mpira wa kimazoea.
Akizungumza Dar es Salaam jana Katibu huyo wa CECAFA alisema michuano ya mwaka huu imekuwa migumu sana kwa klabu kongwe zikiwemo za Simba naTusker kwa kuondolewa mapema kutokana na mifumo ya kucheza soka la mazoea badala ya kujipanga vyema.
"Ni wazi kwamba mashindano ya mwaka huu yamekuwa na ushindani mkubwa ambao umeonyeshwa na klabu ndogo kutokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya kabla ya kuanza michuano hiyo,"alisema Musonye.
Alisema klabu kongwe kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati zinacheza soka kwa mfumo wa mazoea ambao ni kinyume na kandanda la sasa ambalo linahitaji ustadi mkubwa wa kujipanga.
Wakati huo huo Katibu huyo amesisitiza kuwa kamati yao ya utendaji itajadili kwa kina jinsi ya kubadilisha michuano hiyo ili yaweze kufanyika Januari badala ya Julai ili kuziandaa timu na michuano ya Klabu Bingwa na kombe la Shirikisho.
Pia amelaani vikali taarifa zinatolewa na Makocha, kuwa CECAFA wanaendesha michuano hiyo kama njia ya kujipatia fedha kwa kuzibeba timu za Simba na Yanga kutokana na kuwa na mashabiki wengi.
"Nimesikia taarifa ambazo zinadaiwa kuwa kuna baadhi ya makocha wanatutuhumu kuwa tunaendesha mashindano haya kimapato kwa kuzibeba Simba na Yanga, kwanini nisiibebe timu yangu ya Tusker kama ni hivyo, sisi tunacholenga ni kuziandaa timu zetu zote kabla ya kuanza kwa ligi kuu," alisema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment