30 July 2012

Selasini awalipua wabunge mafisadi *Adai wamehongwa pesa na kampuni za mafuta *Wapo wa CCM, CHADEMA, Mnyika alipuka



Na Benedict Kaguo, Dodoma

MBUNGE wa Rombo, mkoani Kilimanjaro Bw. Joseph Selasini (CHADEMA), jana alikuchua makucha na kuwalipua baadhi ya wabunge kwa madai ya kura rushwa kutoka kwa wamiliki wa kampuni binafsi za mafuta.


Alisema lengo kampuni hizo ni kuwataka wabunge hao wamshauri Rais Jakaya Kikwete ili awaondoe madarakani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw Eliakim Maswi, kwa kisingizio cha kukiuka kununi za manunuzi ya mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL.

Akichangia hotuba ya Wizara hiyo mjini Dodoma jana, Bw. Selasini alisema wamiliki wa kampuni hizo walikuwa mkoni humo kwa muda wa wiki moja wakitoa fedha kwa baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CHADEMA.

Alisema dhamira ya viongozi wa kampuni hizo kutaka watendaji wa Wizara hiyo waondolewe ni baada ya kuokoa sh. bilioni sita kila mwezi ambazo zingekwenda katika ununuzi wa mafuta hayo.

Bw. Selasini alisema kwa muda wa wiki moja, Prof. Muhongo na Bw. Saswi wamekuwa wakidharirishwa kwa hatua za kudhibiti upoteza wa fedha hizo.


“Mheshimiwa Mwenyekiti, rushwa haina chama, dini wala kabila, wamiliki wa kampuni binafsi za mafuta walikuwa hapa Dodoma wakimwaga fedha kwa wabunge wa CCM na CHADEMA...ndio maana wabunge wanazungumza kwa nguvu ya fedha,” alisema.

Aliongeza kuwa, baadhi ya wabunge wanakidharirisha chombo hicho na Taifa kwa kugawanyika ili kuwatetea mafisadi wachache ndani ya TANESCO.

Alisema Bw. Maswi alitumiwa hadi ujumbe mfupi wa vitisho katika simu yake yake ya mkononi ambapo kuna baadhi ya wabunge wanafanyabiashara na TANESCO ndio maana wanataka kuliyumbisha Bunge kwa kigezo cha kukiuka kanuni.

Baadhi ya (sms), alizotumiwa Bw. Maswi (Majira inazo), zinasomeka kuwa, “Maswi, sijawahi gombana na wewe kwa saababu nakuheshimu sana, tuhuma ambazo wewe na na Waziri wako mnatoa dhidi yangu ni uwongo, uzushi na za kupikwa”

“Mwambie Waziri wako na wewe binafsi, sijawahi kushindwa vita ya kulinda credibility yangu, sipendi ujinga hata kidogo, mimi nina uhuru wa kusema ninachoamini, sina bei tupambane ili tuone nani ataumia” ujumbe huo ulisomwa na Bw. Selasini bungeni.

Alisema baada ya kuingia Bw. Maswi katika Wizara hiyo, aligundua kuwa TANESCO wanakusanya sh. bilioni 60 kwa mwezi ambapo zaidi ya sh. bilioni 11 ndizo zilikuwa zinatumika kwa mishahara wakati kiasi kingine hakijulikani kinakokwenda.

Aliongeza kuwa, kuwepo pendekezo la sheria za wahujumu uchumi, umefika wakati mafisadi wote wahukumiwe kama wahujumu uchumi kwani wabunge wamezoea kuinyooshea kidole Serikali na Mawaziri kuwa ndio mafisadi kumbe wao ndio zaidi.

“Wabunge wenzetu wameshiba pesa, sisi tunapiga makofi kumbe wanatumia nguvu ya fedha kutetea mafisadi, leo watu wanakuja na hoja ya sheria za manunuzi zimekikukwa, wako wabunge ambao wanafanyabiashara na TANESCO na kutaka kuyumbisha bunge, washindwe kwa jina la Yesu na wameshindwa,” alisema.

Mbunge wa Mwibara (CCM), Bw. Kangi Lugola ni jambo la kutia moyo kuona Bunge limekuwa moja na limeamua kutotumika na mafisadi wanaotafuna nchi.

Alisema Bunge haliwezi kukubali kuchezewa na mafisadi kwa sababu wana fedha za kuhonga wabunge na kusisitiza kuwa, Bw. Maswi hakukiuka taratibu zozote kwani mkataba wa IPTL unaonesha Wizara pekee ndio itakayoiuzia mafuta sio TANESCO.

Alisema uamuzi huo umeokoa Bilioni 72 kwa mwaka ambazo zingweza kuondoa tatizo la vifaa vya Hospitalini ikiwemo ambayo ilisababisha mgomo wa madaktari ambao walitaka Mil.600 kwa ajili ya kununulia mashine ya t scan

Mbunge wa Same Mashariki, Bi Anna Kilango (CCM), alisema masIlahi ya Taifa kwanza na kupongeza maamuzi ya Bw. Swai pamoja na Prof. Muhongo kuzuia mpango huo akiwataka wasiogope kwa maamuzi waliyotoa.

Alimpongeza Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kupitia Wizara hiyo Bw. John Mnyika kutaka waliohusika na ufisadi TANESCO akiwemo Bw. William Mhando (Mkurugenzi Mkuu), wachukuliwe hatua kali.


No comments:

Post a Comment