30 July 2012

NIDA yaongeza muda wa kujaza fomu vituoni

Stella Aron na Grace Ndossa

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imeongeza muda wa wiki moja ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kujiandikisha.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari, ilisema hivi sasa mchakato wa kujiandikisha utamalizika Agosti 6 mwaka huu na hakutakuwa na nyongeza ya muda.

“Naomba watu wengi zaidi wajitokeze kujaza fomu katika kipindi hiki ambacho tumeongeza siku na wageni wote wanatakiwa kujaza taarifa zao kwenye fomu za 2A, wakionyesha uraia wa nchi zao na hadhi ya ukaazi wao,” ilisema taarifa hiyo.

Imesema kwa mujibu wa Sheria ya Usajili na Utambuzi wa Watu kifungu cha 9 kidogo cha pili (2), waombaji wasiojua kusoma na kuandika watasaidiwa kujaza fomu na wale wanaojua kusoma na kuandika watapewa fomu ili wajaze wenyewe katika vituo vya usajili chini ya usimamizi wa wasajili waliopo kila kituo.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 20, kifungu kidogo cha kwanza (C) cha Sheria tajwa, ni kosa la jinai kutoa taarifa ambazo si sahihi zikiwemo za uraia.

“Wote ambao watabainika, watatozwa faini au kuhukumiwa kifungo kisichozidi miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja, tunawaomba watu wote wanaojaza fomu za maombi kutoa taarifa sahihi hasa za ura,” iliongeza taarifa hiyo.

Watu walio kwenye makundi maalumu kama wagonjwa, wazee na walemavu wapeleke mahitaji yao kwenye vituo vya usajili kupitia wajumbe wa mtaa au kitongoji ili waweze kupata huduma stahiki kwa utaratibu ulipangwa.

Wakati huo huo, kilio cha wananchi katika maeneo mengi ni kitendo cha baadhi ya wajumbe wa nyumba kumi, kutumia nafasi zao kutoza wananchi sh. 2,000 hadi 500 ili kuwapatia karatasi zinazothibitisha kuwatambua.

Waandishi wa gazeti hili, jana na juzi walizunguka katika baadhi ya vituo na kukuta misururu mikubwa ya watu ambao wengi wao walidai kuwa, wajumbe wao waliwataka watoe fedha ili waweze kupewa barua ya utambulisho wa ukazi katika eneo husika.

Baadhi ya wananchi hao, walisema kitendo cha kutakiwa watoe fedha kwa wajumbe hao, kinawapa wakati mgumu kwani awali Serikali ilipotangaza kuanza kwa mchakato huo, ilisema kila mtu atapata kitambulisho bila gharama yoyote ili mradi awe na sifa zinazostahili kama raia wa Tanzania.

“Mchakato mzima wa kujiandikisha ili kupata kitambulisho cha Taifa una utata mkubwa, baadhi ya wajumbe wa nyumba kumi wanatoza fedha wananchi ili waweze kupewa barua ya utambulisho,” alisema Bi. Fatuma Hamadi, mkazi wa Karakata, Kipawa, wilayani Ilala.

Kwa upande wao, baadhi ya wakazi wa Gongolamboto na Ukonga walilalamikia kitendo cha baadhi ya wajumbe kuwatoza sh. 2,000 hadi 500 ili waweze kupewa barua za utambulisho.

“Kila mtu analipa kiasi chake, ukililia hali utalipa sh. 500 badala ya sh. 2,000 ili upate barua ya utambulisho wakati tunaambiwa hatutakiwi kulipa chochote,” alisema mkazi mmoja wa Ukonga ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Waandishi wetu walishuhudia umati mkubwa wa watu katika eneo la Kipawa Mtaa wa Karakata wakisubiri kujaza fomu za taarifa na kuongeza kuwa, mchakato huo umezungukwa na mizengwe.

“Katika vituo vingi wananchi wamepewa fomu ili wakajaze wenyewe kwa wale wanaojua kusoma na kuandika lakini katika kituo hiki, hali ni tofauti kama unavyoona vurugu tupu,” alidai mkazi huyo.

Alisema utaratibu uliowekwa na NIDA si mzuri kwani watu wanachukua muda mrefu kutafuta majina hivyo kusababisha wakae muda mrefu kituoni.

Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa wa Karakata, Kata ya Kipawa, Bw. Gersoni Mariki, alisema vitabu vya kuandikisha majina ya watu ambao hawakuandikishwa mara ya kwanza havipo hadi vitakapoletwa na kuwatangazia wananchi.

Wakati huo huo, taarifa zilizotufikia wakati tukienda mtamboni zinasema kuwa, NIDA imeongeza muda wa wiki moja ili kutoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kujiandikisha.

Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari, ilisema hivi sasa mchakato wa kujiandikisha utamalizika Agosti 6 mwaka huu na hakutakuwa na nyongeza ya muda.

“Naomba watu wengi zaidi wajitokeze kujaza fomu katika kipindi hiki ambacho tumeongeza siku na wageni wote wanatakiwa kujaza taarifa zao kwenye fomu za 2A, wakionyesha uraia wa nchi zao na hadhi ya ukaazi wao,” ilisema taarifa hiyo.

Imesema kwa mujibu wa Sheria ya Usajili na Utambuzi wa Watu kifungu cha 9 kidogo cha pili (2), waombaji wasiojua kusoma na kuandika watasaidiwa kujaza fomu na wale wanaojua kusoma na kuandika watapewa fomu ili wajaze wenyewe katika vituo vya usajili chini ya usimamizi wa wasajili waliopo kila kituo.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 20, kifungu kidogo cha kwanza (C) cha Sheria tajwa, ni kosa la jinai kutoa taarifa ambazo si sahihi zikiwemo za uraia.

“Wote ambao watabainika, watatozwa faini au kuhukumiwa kifungo kisichozidi miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja, tunawaomba watu wote wanaojaza fomu za maombi kutoa taarifa sahihi hasa za ura,” iliongeza taarifa hiyo.

Watu walio kwenye makundi maalumu kama wagonjwa, wazee na walemavu wapeleke mahitaji yao kwenye vituo vya usajili kupitia wajumbe wa mtaa au kitongoji ili waweze kupata huduma stahiki kwa utaratibu ulipangwa.

No comments:

Post a Comment