26 July 2012

Kizimbani kwa kutakatisha sh. milioni 776


Na Rehema Mohamed

MKAZI wa Ilala, Dar es Salaaam, Bw. Inock Kantelu, jana amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akituhumiwa kutakatisha fedha zaidi ya sh. milioni 776.

Mbele ya Hakimu Bi. Agnes Mchome, wakili wa Serikali Bi. Lilian Itemba, alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kati ya Februari 7 na 24 mwaka huu.

Alidai mshtakiwa alijipatia zaidi ya sh. milioni 776.2 na kuziweka katika akaunti yake namba 0852014743 ya NBC tawi la Masasi, mkoani Mtwara wakati akijua fedha hizo zimepatikana kwa uchimbaji haramu wa madini.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 9 mwaka huu, itakapoletwa kwa ajili ya kutajwa na amerudishwa rumande ambapo kosa hilo halina dhamana.



No comments:

Post a Comment