18 November 2010

Bilal kushughulikia mahakama ya kadhi.

Na Elisante Kitulo

WAUMINI wa dini ya kiislamu nchini jana waliungana na wenzao duniani kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj, ibada ambayo kitaifa iliswaliwa katika Msikiti wa
Simbambali, Temeke Maguruwe, Dar es Salaam, ambako Mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal aliahidi kushughulikia mahakama ya kadhi.

Ibada ya hiyo ya Hijja, ambayo ni nguzo ya tano ya kiislam, iliongozwa na Kaimu Mufti wa Tanzania, Shekhe Ismail Makusanya na kufuatiwa na Baraza Tukufu la Idd.

Akizungumza katika baraza hilo, Dkt. Bilal aliahidi kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi, na kuahidi kushughulikia suala la mahakama ya kadhi.

Dkt. Bilali alisema wananchi wanapaswa kuheshimu viongozi waliochaguliwa na kuahidi kutekeleza ahadi alizotoa kwa kuwa hilo ni agizo la Mwenyezi Mungu.

"Nawaomba muheshimu viongozi waliochaguliwa naahidi kutekeleza ahadi nilizotoa kama agizo la mwenyezi Mungu linavyotaka... kuhusu mahakama ya kadhi, kwa kuwa suala hilo limefika serikalini basi tutalishughulikia," alisema.

Dkt. Bilali amelitaka Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA kutilia mkazo suala la elimu, kuanzia elimu ya awali mpaka ya juu, kwa kuwa dini ya Kiislamu inasisitiza elimu.

Aidha, ameitaka BAKWATA kuratibu safari zote za Hijja ili kuondoa usumbufu waopata baadhi ya mahujaji ambao safari zao huratibiwa na taasisi nyingine.

Katika hatua nyingine, Dkt. Bilali amewata waislamu wasitekeleze ibada ya Hijja kwa kutumia pesa zilizopatikana kwa njia haramu kwa kuwa hijja yao haitakubaliwa.

Awali akisoma salamu za Baraza la Idd kwa niaba ya Katibu Mkuu BAKWATA, Sheikhe Abdalah Matumla alisema hadi sasa mahujaji wote walioko Mecca wako salama.

Kwa upande wake, Kaimu Mufti, Shekhe Makusanya alitoa wito kwa viongozi wa dini kutochanganya dini na siasa na badala yake wahubiri upendo na utulivu kwa waumini wao.

"Nawaasa viongozi wenzagu wa dini tusikubali kuchakachuliwa na kugeuza nyumba za ibada kuwa sehemu za siasa, kama kiongozi anaona siasa ni bora kuliko dini atumie majukwaa ya siasa kuhubiri siasa hizo," alisema.

Pia aliwata waislamu kuacha chuki baina yao na badala yake kuwa na umoja na upendo na kuheshimu viongozi na taratibu zilizowekwa.

Sheik Makusanya aliwata waisla wajiepushe na ulevi na maasi wakati huu wa sikuku ya Idd el Hajj.

"Nawaasa waislamu msitumie sikuku hii kujihusisha na ulevi na wala kutumia fukwe za bahari kufanya maasi kama ambavyo hampaswi kufanya siku nyingine yeyote" alisema.

21 comments:

  1. Bilali tunakutaka uwe makini na maamuzi na ahadi zako maana haya mambo yameshawahi kuleta mtafuku lazima uangalie na utoe uamuzi kwa umakini, na kuhusu Hijja hao Bakwata hawawezi kuratibu hizo safari pekeyao, maana wao pia wana mapungufu mengi sana,kiundwe kitengo maalumu cha kuratibu safari za taasisi zote. Hao Bakwata mwaka 2007/8 walishawahi kuandika barua ubalozi wa Saudia taasisi zingine zisipewe Visa mpk wao waidhinishe ni urasimu na ni kitu hakikubaliki maana sio Waislamu wote wanaikubali Bakwata utakuwa ni ukiritimba wa hali ya juu. Muhimu kitengo hicho maalumu kifatilie nyendo za taasis zote na zilizo kuwa na makosa yanayojirudia kama hao Taibah ni bora zikafungiwa-Kigmb

    ReplyDelete
  2. Hatari kweliweli. Suala la lenye utata lisilokubalika na wengi ndiyo la kuanzia. Sijui mikakati yenu itapeleka wapi nchi

    ReplyDelete
  3. ndio mjue walijidai hawana udini hapo tusemeje? mbona hawaanzi kushughulikia ufisadi unaonuka, na mlolongo wa vipau mbele? haya !!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Haya ndiyo waliyokuwa wanayatafuta watu! na wengine wakaingia kwa mkumbo eti sisiem wanafaa kuongoza inchi! sasa wote waliokuwa na kiherehere cha sisiem wangoje ujira wao maana watajutia uamuzi wao. Hawa sisiem walijulikana tangu mwanzo kuwa wameegemea upande wa waaisilam, hii mbaya sana. Ona sasa bilal anaanza na dini badala ya maslahi ya taifa!!! hii ni hatari sana, tena narudia, watu wote waliotia kura zao sisiem na wale wliosaidia kuchakachua watajutia uamuzi wao. Poleni sana, asiye sikia la mkuu huvunjika guu. CHAGUENI MAGEUZI achaneni na ufisadi wa sisiem.

    ReplyDelete
  5. Mahakama ya Kadhi tena!!!. Ama Kweli sikio la kufa halisikii Dawa.Huu si wakati wa CCM kutenga watanzania ni wakati wa kujenga kama hawalielewi hili watakuwa ni viumbe wa ajabu...

    ReplyDelete
  6. Hivi ili la mahakama ya Kadhi halikwisha,Mbona mnalirudiarudia,ebu wahusika waseme lilikuwaje,mbona linaibuka na kufifia na kuibuka tena,ni nini sababu yake??

    ReplyDelete
  7. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 18, 2010 at 10:26 AM

    Jamani, jamani, jamani,kidole na jicho jamani.Kwahiyo,Dr.Bilal ukimaliza hili utaelekea kwenye lile la Zanzibar ni nchi au la? Hapana vp wakati mambo haya yaliongozana.Usivyoogopa wala kuuheshimu umma basi Mheshimiwa wewe utaahidi kuhusu kama Tanzania ijiunge na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.Mambo haya yalishatolewa maelezo,iweje tena muyafufue? Hamwaamini Viongozi wenu waliotangulia kuyasemea? Kwanini? Hivi Mahakama ya Kadhi Mheshimiwa Bilal umeiona kwenye Ilani ya Chama gani kama 'Priority'? 'Nyinyiemu' mnayo? Anzeni na mambo muhimu,sio hili.Ahadi zenu hamjatekeleza halafu mnaanza kumwaga mpya...mmeshaanza usanii eeeh?

    ReplyDelete
  8. Huyo ndiye Bilal mvurugaji,ni nani asiyemjua alivyokuwa na upendeleo mkuu akiwa UDSM,Wizara ya elimu ya juu,au mmemsahau,alivyofanya?? wengi tunakumbuka.ebu waulizeni walikuwa wizara hiyo wakati akiwa katibu mkuu,ishu zake za udini,uzanzibar,bila shaka atazirejea kwani ni rais kinyonga kubadili rangi lakini si sumu.

    ReplyDelete
  9. Hongera Dk. Bilal kwa kukumbuka haki ya msingi ya waislam, ni wajibu kutimiza suala la mahakama ya kadhi.....!

    ReplyDelete
  10. Hivi hii serikali ni ya waislamu au ni ya dini zote, mbona kila kukucha waislamu tu hayo matatizo ya hayaishi. Halafu wanasema kuna udini na ukabila. Hawa viongozi wa kiislamu wanataka kuajiri serikali iwafanyie kazi ofisini kwao au. Viongozi waandae shughuli zao kwa wakati unao takiwa. Haya mambo ya kadhi mpeleke huko Zanzibar mtuachie Tanganyika yetu tunajua CCM wanataka vita vitokee tu. kila kukicha uislamu mbona hatuwasikii wakristo wakilalamika. Ina maana hawana matatizo au. Viongozi serikalini acheni kuwakumbatia hawa watu watatupeleka pabaya au kama mnataka kufanya shughuli zao muache shughuli serikali mkakae ofisini kwao kwa sabaabu nyinyi ndio mnaoweza.

    ReplyDelete
  11. wote mliompinga DR Bilal ni wanaafiki na wachonganishi wakubwa, ahadi ya kuanzisha mahakama ya kadhi ilikuwepo kwenye ilani ya C.C.M mwaka 2005, na ilishaanza kutekelezwa kwa serikali kuunda kamati ya wataalam wa kiislaam na serikali ili kujua muundo wa hiyo mahakama.

    kama mnaipinga mahakama ya kadhi, mnatakiwa mpinge pia kuwepo kwa ubalozi wa VATICAN hapa nchini, kwa kua unaendeshwa kwa kodi za watu wa dini zote!!!
    acheni chuki zenu nyie wakristo msiojua umuhimu wa amani!!

    ReplyDelete
  12. unajua hawa wenzetu wakristo wamejijengea imani kwamba wao ni first class na waislaam ni second class, hivyo kuona raisi wa TZ, makamu wa rais, Rais wa ZANZIBAR,makamu wote wawili, yaani TOP FIVE liders ni WAISLAAM, inawatafuna na kuwakereketa sana na wanatamani ardhi ipasuke wajichimbie ili wasione hii hali!!! poleni sana!!! itabidi mvumilie hayo maumivu kwa miaka mitano, na msipoangalia mtaendelea kuongozwa na waislaam kwa zaidi ya miaka 100 ijayo!! acheni chuki za kijinga!!! mahakama ya KADHI na nchi kujiunga na OIC ni lazima , MTAKE, MSITAKA!!

    ReplyDelete
  13. Kwa kweli serikali hii ya sasa ni serikali ya Kiisilamu. Hii sasa ni Islamic Republic of Tanzania. Unajua kwa sisi wakristo uchakachuaji ni dhambi kwa dini za wenzetu unaruhusiwa kuchakachua!
    Tunaomba neno moja tu. Msitulazimishe sisi wakristo kuunga mkono wizi.

    ReplyDelete
  14. to hell all christians....if u have nothing to view u better keep quite..!!i hates u as u hate me..

    ReplyDelete
  15. christians...shut your ass....whatever u can say kadhi is must whether for sword or grenade...do you hear me??big ass all!

    ReplyDelete
  16. In christianity cussing and profanity is a sin. I know in Islam its another matter altogether!

    ReplyDelete
  17. that z not a must u have to understand that..
    hao mnaojivunia kama ndo top 5 wenu hawataweza kuipitisha hiyo mahakama mpaka Bunge lipitishe, sasa hesabu wabunge ambao ni swala 5 na sisi wakristo ni pande ipi wengi.? hope jibu unalo

    udini mnauanzisha ninyi wenyewe mana rais mchakachuaji ndiye anayeteua viongozi kidini lkn hiyo haijalishi hope miaka 5 si mingi na bahati yenu mmechakachua tungewang'oa.

    hilo la ubalozi wa vatican kaka naomba uelewe kuwa ubalozi wowote uliopo bongo unajiendesha wenyewe ruzuku zote zinatoka nchi kwao HATA kwa maana uliyokuwa unakusudia vp kuhusu balozi za nchi za arabuni? hizo sio za kiisilamu?

    ReplyDelete
  18. Pale bungeni wakati baadhi ya wabunge kulalamikia kutopewa nafasi kwa kiongozi wa upinzani bungeni kuchangia uteusi wa raisi mintalafu waziri mkuu, spika Makinda alisema kuwa hoja hiyo haikuwa ya serikali kwa vile serikali haijakuwepo.
    Sasa kama serikali haijakuwepo Dr. Bilal amewezaje kutoa tamko rasmi la serikali? Ni baraza gani la mawaziri limekaa na kujadili hoja hiyo ya mahakama ya kadhi hadi ikatolewa rasmi jana? Kwanza Dr. Bilal hakuwa sehemu ya serikali iliyopita, amepata wapi jibu la serikali juu ya mahakama ya kadhi, au amekuwa akipata siri za vikao vya baraza la mawaziri lililopita? Mimi nadhani amewahi mno na hivyo kusababisha masuali mengi mno.

    ReplyDelete
  19. Bilal huna sera! We jikongoje tu umalize hii ngwe uliyofadhiliwa na mwislam mwenzio JK.Hujawahi kusikika hata.Na hapo hujaanza vizuri.Chunga mdomo wako.Sio waislam waliokuchagua- ni WATANZANIA.

    ReplyDelete
  20. SIKUJUA KAMA SERIKALI INGEFIKIA HAPA, WANANCHI WA TANZANIA POLENI SANA NA MUOMBE MUNGU HILI DARAJA LIWAVUSHE MSIJE MKAANGUKIA KATIKATI YA MTO MKALIWA NA MAMBA. KAMA SERIKALI ITAFANYA SHUGHULI ZA DINI HATUTAFIKA.
    KWA UFAHAMU TU VATICANI HAIITAJI HATA SENTI TANO SERIKALINI KAMA MNAVYOONGEA. HII KADHI SIJUI KADHI NI MPAKA IENDESHWE NA SERIKALI AU, KWA SABABU SERIKALI INAIHITAJI AU NI MTU AMEAMUA, SERIKALI INAKAZI ZAKE ZA KUFANYA HAIHITAJI HIYO MAHAKAMA. MAHAKAMA TULIZO NAZO ZINA TUTOSHA. MNATAKA MKAMFUNGE HUKO NANI WAFUNGWA WANAMAGEREZA YA KUTOSHA. AU NDIO CHINJA CHINJA INAKUJA KAMA KULE.........

    ReplyDelete
  21. Siku zote wanaovuruga amani duniani kote ni hawa hawa. Huwezi hata siku moja kusikia serikali ya kiisilamu inapatanisha watu wanaopigana au inasaidia watu wenye shida. Unachosikia ni kuwa wanaenda kupigana jihadi mara somalia mara afghanistan mara chechenya!

    Ni watu wasiopenda amani kabisa, angalia huyo jamaa hapo juu anatukana wakristo na kusema waende kuzimu yaani hell na anatukana matusiya nguoniwakristo.

    ReplyDelete