31 July 2012

Nyota 6 wa Airtel kupigwa msasa


Na Amina Athumani

NYOTA sita wa Airtel Rising Star, wanatarajia kushiriki kliniki ya kimataifa itakayoendeshwa na makocha wa Klabu ya Manchester Uneted.

Kliniki hiyo inatarajia kufanyika Oktoba mwaka huu, ambapo nyota hao wataambatana na kikosi cha timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, watakaoshiriki michezo ya Afrika itakayofanyika Nirobi, Kenya.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusianao wa wa Kampuni ya Airtel Jane Matinde, alisema vijana wote waliopatikana katika programu ya Airtel ya kuendeleza soka kwa vijana ndiyo watakaoshiriki kliniki hiyo.

"Mchakato huu uliwapata wachezaji nyota sita kupitia Airtel Rising Star, ambao ndiyo watakaoshiriki kliniki itakayoendeshwa na makocha wa Manchester United kama ilivyokuwa mwaka jana.

Pia tunao vijana 16 waliounda timu ya vijana kwa ajili ya michuano ya Afrika ambayo pia itafanyika Nairobi, Kenya," alisema Jane.

Alisema mashindano hayo na kliniki hiyo, itashirikisha vijana kutoka nchi 16 za bara la Afrika ambazo Airtel zina matawi yake katika nchi hizo.

Ofisa huyo alisema tarehe rasmi na utaratibu mzima kuhusu safari ya nyota hao, itatangazwa mara baada ya utaratibu mzima kukamilika.

Alisema Airtel itaendelea kusapoti vipaji vya vijana wa Tanzania kupitia mashindano ya Airtel Rising Star, ambayo yanatoa fursa kwa vijana wadogo kutangaza vipaji vyao na Tanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment