27 July 2012
Mbatia afichua ufisadi Tanesco *Aeleza madudu ya Mhando, aonesha mkataba wake *Siri wabunge CCM kumng'oa Waziri sasa yafichuka
Na Benedict Kaguo, Dodoma
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, jana ameibua ufisadi wa kutisha wa ununuzi mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL na kudai baadhi ya wabunge walihongwa ili kumtetea aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. William Mhando.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Bw Mbatia ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa, alisema kipindi cha wiki moja sasa, kumekuwa na vikao vya chini chini ambavyo vinafanyika ndani ya Bunge, nje ili kutoa mapendekezo ya Bw. Mhando kuonewa juu ya tuhuma zinazomkabili.
Alisema Waziri Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, wamefanikiwa kuziba mianya ya watu wachache kunufaika na miradi ya TANESCO.
“Hali hii ndiyo imechangia kuundwa timu inayohusisha baadhi ya wabunge ili kuonesha wenye matatizo ni viongozi wa Wizara sio Maofisa wa TANESCO,” alisema Bw. Mbatia.
Alisema inasikitisha kuona wabunge wameingia katika ufisadi wa kutisha, kuweka masilahi yao kwanza na kusababisha Taifa liingie katika matatizo ya umeme.
Bw. Mbatia alidai hadi June mwaka huu, TANESCO walipewa sh. bilioni 222.1 na Serikali kama ruzuku ili kuendeshea shirika hilo kukabiliana na tatizo la mgawo lakini walikuwa wakizima mitambo ya umeme kwa makusudi ili waweze kunufaika na mgawo kwa kununua mafuta kutoka katika kampuni yao.
“Kampuni ya Puma ambayo zamani ilikuwa iliitwa BP ambayo sehemu kubwa inamilikiwa na Serikali, ilisema katika mradi huo wa mafuta ya mitambo itauza sh. 1,460 kwa lita, baadhi ya kampuni zilizoingia katika ushindani kwenye kandarasi ya kusambaza mafuta, wenyewe walikuwa wauze sh. 1,800 kwa lita.
“Katibu Mkuu wa Wizara hii alitumia mamlaka yake kwa mujibu wa sheria na kutengua maamuzi ya kununua mafuta kutoka kampuni binafsi hivyo kuokoa sh. bilioni 6 kwa mwezi, ambapo Serikali ingeingia hasara kama ingenunua mafuta katika kampuni binafsi,” alisema Bw. Mbatia.
Aliongeza kuwa, TANESCO haikuwa na sababu ya kupewa ruzuku kwani makusanyo ya mwezi katika shirika hilo ni makubwa ambapo Julai mwaka huu, wamefanikiwa kukusanya sh. bilioni 85, hivyo kulikuwa na haja gani kutoa ruzuku kwa shirika ambalo linajiendesha kwa faida.
Bw. Mbatia alisema kutokana na kashfa hiyo, Kamati ya Nishati na Madini imekosa uhalali na baadhi ya wabunge ambao ni wajumbe wa bodi kwani ndio wamechangia kutokea wizi huo.
Alitaka Menejimenti ya TANESCO na Bodi ya Wakurugenzi, wote hawafai, wanapaswa kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola kwa kutaka kuliua shirika la umma.
Alitoa waraka wa mkataba aliosaini Bw. Mhando na mkewe wa sh. milioni 800 (kwa waandishi wa habari), ili kusambaza vifaa vya ofisini ambapo kampuni hiyo ilikuwa na mtaji wa sh. milioni 10 tu, na kueleza kuwa hayo ni matumizi mabaya ya madaraka.
Mkakati wa kumngo’a Waziri
Wakati Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo akitarajiwa kuwasilisha Bajeti ya Wizara yake leo, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), usiku wa kuamkia jana walikutana kwa udharura kujadili suala la baadhi ya wabunge wa chama hicho kutaka kuwasilisha hoja ya watendaji wakuu wa Wizara hiyo wang’olewe.
Kkikao hicho ambacho kilifanyika kwenye ukumbi wa Msekwa kilikuwa na ajenda kuu ya kujadili hoja ya baadhi ya wabunge waliotaka kuwasilisha hoja binafsi.
Hoja hiyo ni kutaka Prof. Muhongo na Katibu Mkuu waondelewe kwa madai ya kukiuka sheria ya manunuzi kwenye ununuzi wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL.
Hata hivyo, kikao hicho ambacho kilitawaliwa na mvutano mkali ambapo wabunge wengi waliwalaumu wenzao kwa kuendesha kampeni hiyo baada ya kuhongwa na TANESCO ili watetee uamuzi wa kutaka mafuta hayo yanunuliwe na kampuni binafsi.
Kampuni hizo zinataka kuizia TANESCO lita moja ya mafuta sh. 1,800 badala ya sh.1,460 inayonunuliwa na Kampuni ya Puma ambayo zamani ilikuwa ikiitwa BP.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zilisema wabunge waliochangia waliwanyooshea kidole baadhi ya wabunge wachache
wanaodaiwa kununuliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tanzania na watanzania tutafika wapi kama watu tuliowaamini tukawapa thamana ndio hao kila siku kuizamisha taifa kwa kujineemeasha wenyewe.Hii ni laana iliyoikumba nchi na watawala,siwaiti viongozi katu,kilichobaki sasa ni watu wafunge na kuiombea taifa ili MUNGU ashushe ghadhabu yake juu ya wezi hawa.
ReplyDeletetuwajue tu hao wabunge waliohongwa na majimbo wanayotoka 2015 tumalizane nao mungu awalani kwa ufisadi wao
ReplyDeleteuzalendo wa watanzania umepotea kwa kujali maslahi binafsi badala ya maslahi ya waliowengi.Watanzania tuamke tusichague vyama tuchague viongoziwaadilifu,wachapakazi bila kuangalia rangi,kabila na kulaani mfumo wowote wa kupata viongozi kwa misingi ya rushwa,kujuana na kurithishana.
ReplyDeleteMwandishi huyu ajitahidi kuhakiki uandishi wake. Hawezi hata kujieleza. Aibu
ReplyDeleteSio kweli kwamba mwandishi ameshindwa kujieleza. Hapa ni message sent and delivered. Ukweli ni kwamba ukitupa jiwe kwenye mbwa wengi, atakaebweka huyo ndiye aliyepigwa.
DeleteHuna jipya,ingawa unaona.
Deletelabda angetusaidia mwandishi ameshindwa vipi kujieleza,kwa sababu tunajua aliyekuwa anajieleza ni mbatia sio mwandishi hao ndio wote mafisadi wanaomtetea muhando,huyo ameshalipuliwa kwa ufisadi haponi tena
ReplyDeleteWatanzania na serikali yetu tunatakiwa kuwa na utamaduni wa uwajibikaji: Ukituhumiwa na/au kutiliwa mashaka ktk wadhifa ws umma, achia ngazi.. PERIOD. Hao Waheshimiwa watakapotajwa, huo 'Waheshimiwa' utakuwa ndio umeyeyuka - waachie ngazi immediately, tusisubiri 2015.
ReplyDeleteMimi kwa upande wangu naamini wabunge wengi wa CCM hawakupewa ridaa na wananchi bali walipewa ridhaa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.Matokeo yake ni hayo hawana wanachofanya bungeni ni kujipendekeza kwa serikari yao na kuunga mkono hoja,ziwe hoja za kifisadi au za rushwa wao kwao si tatizo.Kwa hili tunaomba watajwe hadharani tuwajue.
ReplyDeleteHUYU ALIYEANDIKA HAPO JUU NI KICHAA KWA KUZUNGUMZIA WABUNGE WA CCM TU. HAWA NDIO MAMLUKI WA VYAMA VYA SIASA WALIOKODIWA KUTETEA UOZO. KASHFA HII YA TANESCO INAMHUSU HATA ZITTO KABWE WA CHADEMA NA UKIENDA MBALI ZAIDI HATA FREEMAN MBOWE YUKO KWA ALIPANGA DEAL NA JIMBO LAKE LA UCHAGUZI KUNUNUA JENERETA TANESCO KISHA WALITENGENEZE KWA KISINGIZIO KUTUMA KWA JIMBO LAO NA ZIADA IUZWE KWA TANESCO. SIO CCM TU HATA CHADEMA WAMO AU HUJUI CHAMA HIKI KILIANZISHWA NA WAFANYABMAARUFU MJINI MOSHI? TAIFA LINAIBIWA NA WANASIASA KWA KUMUUA MLALAHOI. HII DEAL YA TANESCO NI YA SIKU NYINGI,HUMUONI ZITTO KABWE YUKO KIMYA SIKU HIZI KESHAFUNGWA MDOMO NA ALIKUWA MSTARI WA MBELE ATI KUITA BODI YA TANESCO IKAJIELEZE . SWINE TANZANIANS MNAOTETEA VYAMA HUKU MKIFA
ReplyDeleteuna point lakini punguza jazba. sisi wote wenye uchungu na nchi hii tuko tayari kuwanin'giniza mafisadi na wezi wa aina yoyote bila kujali rangi ya scarf wanazovaa shingoni
DeleteInauma sana hii. Nilisoma juzi juzi hapa kuwa mapato yameongezeka kutoka shs. billion 57 hadi billion 85 mara baada ya kusimamishwa mkurugenzi. Haijapita wiki tatu tangu hii itokee. Matumizi yote kwa mwezi ni karibu shs. Billion 11. Inamaanisha Tanesco ina-ziada ya shs billion 74. Hizi pesa nyingi kiasi hiki zinakwenda wapi na kwanini itoke ruzuku tena serikalini? Tumeambiwa mafuta ya PUMA yana-save kiasi cha shs billion 6 kwa mwezi na kama yangenunuliwa kwa watu binafsi basi hizi billion 6 zingeishia kwa wachache- ambayo ndio wanatusumbua hapa mjini na magari na majumba ya kifahari kwa wizi tu. Hivi kama kuna ziada kubwa kiasi hiki, kwanini umeme usiteremshwe bei hata kwa asilimia 60 ili watu waweze kununua umeme na kuacha kutegemea mikaa na pia kuacha kuiba umeme? Suala la kuiba umeme halijaanza siku nyingi, watu wameshindwa kabisa kununua umeme ambao kila siku unapanda bei na umekuwa bei ghali kuliko hata mishahara yao. Wachachwe wanatuibia mamia ya mabillion ya shilingi halafu wengi wanateseka kwa umeme kuwa ghali kuliko maelezo. Kumbe watu wengine wanazima mitambo wengine wanafanya makusudi kuua machine ili waweze kununua mafuta wapate mabillion ya pesa.Watu wanashindwa kununua umeme maana ni ghali mno. Tumekimbilia kununua gas amabyo mtungi wa kg 15 ulikuwa shs. 23,000 lakini leo ni shs 54,000 maana watu walimbilia kununua gas baada ya umeme kupanda bei kutokana na ufisadi wa viongozi wetu.Vishoka wa Tanesco wameelewa hili ndio maana nao wana kula kwa ujanja wao kwa kuwaunganishia watu umeme au kuchezea Luku maaana umeme haununuliki. Watu wanaiba umeme kutokana na gharama kubwa inayotokana na wizi wa mabillion ya pesa. Umeme uteremshwe bei tuone kama maisha hayatakuwa bora kwa watanzania. Tunajua hata gas kuna watu wanafaidi ndio maana hakuna mtu anayelalamika. Hii gas inayotoka kusini haiwezi kusaidia bei ya gas kushuka? Jamani hatutaki kutumia kuni na mkaa, umeme na gas ni bei rahisi kama ufisadi utapigwa vita. Tusamehane na tuanze ukurasa mpya, kila mwenye kosa ajirekebishe na kama ulishakula pesa zako- mabillion basi yanakutosha.Anza kuwekeza zitawatosheni na familia zenu. Mungu awabariki sana
ReplyDeleteJAMANI HATUONI NCHI ZA WENZETU?CHINA INAENDELEA KWA KASI KWA KUWAPRUNI WEZI WA AINA HII.HIVI HAWA WAKUBWA WETU KWELI WANA DINI?HAIWEZEKANI WATU WANALAZIMISHA MGAWO WA UMEME ILI WAPATE HELA HAWA NDO MASHUJAA WA BONGOLAND?????
DeleteKama kungekuwa na uwajibikaji wa kweli hawa wanaotuhumiwa kuhujumu taifa bora wanyongwe pindi itakaposibitika wamefanya makosa hayo.Tumechoka kusikia tuhuma tuu bila ADHABU YA KUKOMESHA UJINGA HUU WA MAKUSUDI.Jamani
ReplyDeleteNajua watu dini wanazo na huu ni mwezi wa toba lakini nashangaa hakuna hata anayejitokeza kutubu dhambi zake kwetu wananchi au wanafikiri MUNGU anafanyiwa unafiki kama mwanadamu?Ama UFISADI si DHAMBI,watu wanatuhumiwa lakini vyeo hawataki kuachia ndio kwanza wanaongoza kamati za bunge.Nawalaumu viongozi wa DINI maana hao watumiwa ni waumini wao hawawambii ukweli na wanadiriki kupokea zaka ambazo ni hela tumedhulumiwa walalahoi kutokana na nafasi walizonazo.
ReplyDeleteYaani, Waziri wetu na Naibu na Karibu walipotaka kuokoa shs billion 6 zilizokuwa zinalipwa kila mwezi kwa wasambazaji wa mafuta wa kampuni binafsi wameonekana ni wabaya hata kutaka kuundiwa tuhuma nzito. Kumbe watu waliteseka kwa umeme kutokuwepo kutokana na watu wachache kuhujumu mitambo? Hivi hizo ruzuku za shs billion 222 zilizokuwa zinatoka serikalini zilikuwa zinaenda wapi? Tumesikia ati kuwa mapato yameongezeka hadi billion 85 kwa mwezi kutoka billion 59. Je, kama matumizi kwa mwezi ni billion 11 , hizo pesa nyingine ni wakina nani hao wanazichukua? Hivi Utoah, walimdhibiti asifanye ukaguzi kwenye hili shirika? Vyombo vya usalama viko wapi? Saa nyingine tunasema China ni wababe, ila kwa kweli kama maendeleo yanahitaji ubabe kwa watu wanaotumia vibaya madaraka kiasi hiki ni heri na sisi tuwe kama chini, maana ingekuwa ni china basi tungewapoteza jamaa wetu wengi sana ktk hili suala. Wenzetu hawa hawana utani kabisa
DeleteANONYMOUS
DeleteHALI HII NI HATARI SANA. KULE ETHIOPIA WATU KAMA HAWA WALIKUWA WAKITANDIKWA RISASI HADHARANI NA SERIKALI YA MENGISTU HAILE MARIAM. ADHABU KAMA HIZO ZIMEIFANYA ETHIOPIA KUSONGA MBELE KWA KASI KWA SABABU WATENDAJI WOTE, PAMOJA NA WATAWALA AU VIONGOZI WALIINGIWA NA WOGA WA KUIBA MALI YA UMMA, TOFAUTI NA NCHI YETU HII ILIVYO SASA. MIAKA YA 70 TANZANIA ILISIFIWA KWA NIDHAMU YA UTENDAJI KAZI. SI SASA. MTANZANIA AFANYAYE KAZI KATIKA MASHIRIKA YA KIMATAIFA AU KWENYE BALOZI ZA NJE NCHINI ANASIFIWA KWA UHODARI, UADILIFU NA UZALENDO. SI SERIKALINI AMBAKO IMEKUWA SHAMBA LA BIBI. AIBU KUBWA SANA NA ATHARI ZAKE ZITATOKEA SIKU MOJA NA WATANZANIA NDO WATAJUA GHADHABU NA HASIRA ZA WALALA HOI NI KITU GANI.
PRT General Supliers LTD ndo walishinda tenda ya kusambaza vifaa vya ofisini mhando na mkewe akawapiga changa la macho kama kunmuandishi wa habari aende kampuni hio ina data zote naiko maeneo ya ubungo nhc karibu na kanisa la kianglikana na ishu iko mpaka PPRA bodi ya tenda tanzania
Delete