30 July 2012
Kizimbani kwa ubakaji
Mohamed Mohamed na
Happy Julius.
MKAZI wa Mbagala Kingugi Dar es Salaam Bw. Salum Ramadhani (42) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma ya ubakaji.
Mbele ya Hakimu Bw. Karim Mushi ilidaiwa na mwendesha mashtaka Bi.Honorina Munishi kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya mwaka 2009 na Julai mwaka huu katika maeneo ya Kariakoo.
Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alibaka mtoto mwenye umri wa miaka 14(jina tunalo),mshtakiwa alikana shtaka hilo na yuko nje kwa dhamana ya sh.5,000,00 kesi itatajwa tena Agosti 16 mwaka huu.
Wakati huohuo Mkazi wa Tabata Segerea Bw. Gabriel Edward (27) amefikishwa Mahakamani hapo kwa tuhuma ya ubakaji.
Mbele ya Hakimu Ester Mwakalinga ilidaiwa na mwendesha mashtaka Bi. Anuciata Leopard kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 15, mwaka huu katika maeneo ya Segerea.
Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alimbaka binti wa miaka 21(jina tunalo), mshtakiwa alikana kosa hilo na yuko nje kwa dhamana ya sh..4,000,000 kesi itatajwa tena Agosti 15,mwaka huu Mahakamani hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment