27 July 2012
Ugumu wa maisha kuongezeka nchini
Na Mwandishi Wetu, Mashirika ya habari
HALI ngumu ya maisha inayowakabili Watanzania wengi nchini, huenda ikaongezeka zaidi ya ilivyo sasa.
Hali hiyo inadaiwa kuchangiwa na tofauti kubwa ya pato la Taifa nchini hadi kufikia asilimia 15 ya pato la jumla mwaka 2011/12 kutokana na kupanda kwa uagizaji mafuta na gesi kutoka nje.
Barua iliyotumwa na Serikali ya Tanzania kwenda Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Juni 21 mwaka huu, ilisema hazina kubwa ya gesi imegundulika nchini mwaka huu.
Pia barua hiyo ilisema Tanzania inakabiliana na matatizo mengi kutokana na mfumko wa bei unaosababisha kupanda kwa ghrama za maisha na udhaifu wa sarafu dhidi ya dola kwa kipindi kirefu cha mwaka 2011 ambapo hali hiyo pia inadaiwa kuzikumba nchi jirani za Kenya na Uganda.
Chanzo cha hali hiyo ni upungufu wa nishati katika kipindi hicho kutokana na uhaba wa maji ambayo ndio chanzo cha kuzalisha umeme ambapo viwanda vililazimika kutumia jenereta zinazotumia mafuta na gesi hivyo uagizaji mafuta na gesi kutoka nje uliongezeka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment