27 July 2012
Ajinyonga akidai wazazi wanamfuatilia
Na Theonestina Juma, Bukoba
MWANAFUNZI Mtanzania aliyekuwa akisoma Kidato cha Sita nchini Uganda, amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kamba akidai kuchoshwa na tabia ya wazazi wake kufuatilia maisha yake.
Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Phillip Kalangi, ambaye alisema limetokea katika Mtaa wa Kashenye, Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera.
Alimtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Remmy Mulima (17), ambaye baba yake mzazi yake, Bw. Sosithenes Mulima, alimpa sh. 500,000 kwa ajili ya ada lakini hakwenda shule na badala yake aliamua kumchukua rafiki yake wa kikena kwenda naye Bunazi, wilayani Missenyi.
Alisema wakiwa Bunazi, kijana huyo na rafiki yake wa kike (jina halikufahamika), walipanga chumba ili kufanya starehe ambapo baada ya baba yake kupata taarifa, alikwenda Bunazi kumfualia.
“Baada ya huyu kijana kujua mzazi wake amemfuatilia na kufahamu alikuwa amefanya kosa, alitaka kunywa sumu lakini baba alimzuia, kijana hakukata tamaa kwani waliporejea nyumbani, alichukua kamba, kuitundika kwenye muembe na kujinyonga,” alisema.
Alisema kijana huyo aliacha ujumbe kwenye nguo yake unaosema “Nimechoshwa na wazazi wangu kufutilia mambo yangu”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment