24 July 2012
Upendo yaizaba Ambassadors mabao 7-0
Na Damiano Mkumbo, Singida
TIMU ya soka ya watoto waishio katika mazingira magumu wa kituo cha Upendo mjini hapa imewachapa wenzao wa Shirika la Youth Ambassadors mabao 7-1.
Mechi hiyo iliyopigwa juzi katika Uwanja wa Chuo cha VETA, ilikuwa na msisimko kutokana na kandanda walilokuwa wakicheza wachezaji wa timu hizo.
Katika mechi hiyo bao la kwanza la Upendo liliwekwa kimiani na Mulik Saidi dakika ya tano.
Washambuliaji wa Upendo ambao walionekana kuwa na uchu wa mabao walipata mabao mengine dakika za 14, 20 na 25 kupitia kwa Ayubu Jumanne, Hamisi Jumanne na Abdu Juma.
Upendo iliendelea kuinyanysa Ambassadors ambapo dakika ya 40, Hamis Jumanne aliipatia timu yake bao la tano.
Kipindi cha pili kilianza kwa nguvu kwa upande wa Upendo, ambapo Malik Said aliifungia timu hiyo bao la sita dakika ya 46 na lingine la saba dakika ya 56.
Bao la kufutia machozi la Ambassadors, lilifungwa dakika ya 27 kupitia kwa Frank Jumanne kwa shuti kali, baada ya kuwalamba chenga mabeki wa Upendo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Youth Ambassodor mjini hapa, Hossein Martin alisema lengo la mchezo huo ni kujenga urafiki miongoni mwa vijana hao, kuibua vipaji vya soka na kuimarisha ushirikiano wa taasisi hizo mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment