23 July 2012
Padri alishukia Bunge, serikali *Adai nchi inaelekea kubaya kutokana na ubinafsi *Alalamikia Bunge kupendelea wabunge wa CCM *Asema yeye ni nabii, yupo tayari kupigwa mawe
Na Anneth Kagenda
MKURUGENZI wa Shirika la Familia la Farijika Afrika Mashariki, Padri Baptisti Mapunda, ameishukia Serikali na kudai Tanzania inaelekea kubaya kutokana na viongozi wake kufanya uozo bila kuchukuliwa hatua.
Alisema hali hiyo inachangia idadi kubwa ya watu kuwa wabinafsi na wengine kuchuma mali ambazo huzitumia na familia zao.
Padri Mapunda aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika mahubiri aliyotoa kwenye Kanisa Katoriki Manzese na kumtaka Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, Naibu wake Bw. Job Ndugai pamoja na Wenyewiti wa mijadala ndani ya bunge, kuacha kuwapendelea wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Wabunge wa vyama vyote wanatoa lugha chafu bungeni lakini Spika wa Bunge (Bi. Makinda), na Naibu wake (Bw. Ndugai), wanaangalia upande mmoja wa CHADEMA, kwa kuwatoa nje wabunge wake wakati hata CCM wanafanya makosa.
Alisema Watanzania wamechoka na mambo yanayofanywa na viongozi serikalini ambapo yeye kama kiongozi na nabii anayefanya kazi ya Mungu kwa miaka 23, ataendelea kukemea maovu hayo.
Aliongeza kuwa, viongozi serikalini wamekuwa wakifanya makosa mbalimbali lakini hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi yao hivyo kuacha majonzi kwa Watanzania kutokana na Rais Jakaya Kikwete kuyafumbia macho.
“Lazima viongozi wazembe tuwaseme, sisi ni mwanga wa kuwasha watu wanaofanya ufisadi na ukandamizaji haki za binadamu japo utasikia baadhi ya watu na magazeti wakisema Padri Mapunda aliutoa wapi unabii...mimi nimepewa na Mungu kupitia Baba Askofu, sitaacha kusema hata wakinipiga mawe,” alisema.
Padri Mapunda aliongeza kuwa, wabunge wa CCM wanapofanya makosa bungeni hawatolewi na kama atatolewa ni gelesha ili kuficha aibu kutokana na makosa wanayofanya.
Alisema hakuna mbunge aliyetumwa na wapiga kura kwenda bungeni kutoa lugha chafu zaidi ya kwenda kupanga mipango endelevu ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Sakata la Dkt. Ulimboka
Akizungumzia sakata la kutekwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dkt. Steven Ulimboka, Padri Mapunda alisema iweje raia wa Kenya amteke kiongozi huyo na kufikishwa mahakamani kimya kimya.
“Nasikia mtekaji alienda kwenye kanisa fulani kutubu na badaye akakamatwa na kupelekwa mahakamani, wameshatuona wajinga kiasi hiki wakidhani hakuna tunalojua, kwanini asiende nchini kwao Kenya kutubu madhambi yake,” alihoji Padri Mapunda.
Alisema Watanzania wataendelea kuhoji hadi ukweli ujulikane na kulitaka Jeshi la Polisi lieleze mtekaji ni dhehebu gani, alitumia usafiri gani kuja nchini, alipita mpaka upi na kwanini afanye maungamo kwenye kanisa lililopo Tanzania.
Padri Mapunda alihoji kwanini Ukristo unadharirishwa na kuonekana sehemu ya maovu kwa baadhi ya watu wanaosema uongo kupitia imani za watu hivyo ataendelea kufanya maombi Dkt. Ulimboka ili apone haraka na kusema ukweli.
Ajali ya Mv Skagit
Alisema kuzama kwa meli ya Mv. Skagit, haukuwa mpango wa Mungu badala yake ni utendaji mbovu na uzembe unaofanywa na Serikali iliyopo madarakani.
“Iweje chombo kinacho beba abiria na kinapita kwenye maji kisifanyiwe ukaguzi wa kina badala yake kinaruhusiwa kufanya safari matokeo yake watu wanakufa, huu ni uzembe uliofanywa na Serikali hivyo wahusika wachukuliwe hatua za kisheria, hatuwezi kukaa kimya katika hili,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
PADRI BAPITIST MAPUNDA NAKUOMBA UGOMBEE UBUNGE NA UINGIE BUNGENI KWANI NI VIONGOZI WANGAPI WA DINI WAKO BUNGENI YUKO MCHUNGAJI MSIGWA, YUKO MCHUNGAJI RWAKATARE NAWENGINEO UMETUUDHI SANA WAUMINI KUTULAZIMISHA TUFUATE MATAKWA YAKO NINGEKUWA POPE NINGEKUFUKUZA KANISANI UKISHAKOSA MAUBIRI HUKO KANISANI UNAFUATA NINI KAWAULIZE VIONGOZI WA DINI WALIOKO BUNGENI WANAHUBIRIJE TUMECHOKA MUNATUBOA
ReplyDeletenabii vua kanzu njoo ktk usanii yaani siasa acha kufanya kazi 2 unabii na usanii baki na kanzu au vua vaa gamba au gwanda
ReplyDeletefreedom of speech
Deletewewe ni chadema mia kwa mia siasa na dini wapi na wapi.hubiri dini huoni kwamba mahudhurio kwenye nyumba za ibada yamepungua na hii ni kwa sababu ninyi wahubiri wenye sura mbili mmekuwa wengi
ReplyDeletewe pumbafu, unaangalia mtu au alichosema kwamba ni cha ukweli? hiyo tunaita ad hominem yaani kumshambulia mtu binafsi badala ya kuangalia hoja yake. hoja ya huyo padri ni ya msingi, yeye kama kiongozi anapaswa pia kukemea ufisadi, kwani dini na siasa zote zinamhusu binadamu huyo huyo mmoja huwezi kumgawa binadamu ukasema hii ni sehemu ya siasa na hii ya dini. rudi darasani kasome tena
ReplyDelete