30 July 2012
Wanne washinda vuta mkwanja Moshi
Na Mwandishi Wetu, Moshi
KAMPUNI ya vinywaji baridi ya Coca-Cola ya Bonite leo imewazawadia washindi nane wa promosheni ya Vuta Mkwanja ambao wemeweza kushinda zawadi na fedha taslimu.
Tukio la kukabidhi zawadi hizo limefanyika jana katika kiwanda cha Bonite Bottlers mjini Moshi.
Washindi hao ni Joseph Gerald ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha SAUT na Diana Thadeo, muuza duka mjini Moshi, ambao wote kila mmoja amejishindia zawadi ya sh.milioni moja.
Washindi wa sh.100,000 ni Muhidini Mushi, mfanyabiashara kutoka Maili Sita, Nicholus Eligadi ambaye ni muosha magari kutoka Merereni, Zabibu Ismail ambaye ni mwanafunzi, Eliakunda Modest mkazi wa Marangu, Aaron Michael kutoka Moshi mjini na James Mjenga ambaye ni mfanyabiashara wa Merarani.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi yake, Diana Thadeo mwenye umri wa miaka 21 alisema amefurahi kushinda zawadi hiyo.
"Ninayo furaha sana kwa siku ya leo (jana), ni kama vile ndoto imekuwa ya ukweli. Sijawahi kupata pesa yangu mwenyewe kiasi hiki, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa mmoja wa washindi, nilinunua soda ya Coca-Cola na baaada ya kuangalia chini ya kizibo nikaona nimeshinda zawadi ya milioni moja.
"Nafikiria kwa sasa nitaacha kazi ya kuuza duka na kufanya shughuli zangu binafsi, nashukuru Kampuni ya Bonite Bottlers kwa kuleta promosheni hii ambayo kwa hakika imebadili maisha yangu nawashauri wateja wengine wa Coca-Cola kwamba promosheni hii ni ya ukweli na waendelee kunywa soda za Coca-Cola na jamii yake na wanaweza kuibuka washindi kama mimi," alisema Diana.
Mshindi mwingini wa sh.milioni moja Joseph Gerald mwenye umri wa miaka 25 na mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza na mkazi wa Pazua alisema zawadi yake ya milioni moja itamsaidia katika kutatua matatizo yanayomkabili akiwa chuoni kama vile kununua vitabu na hata kusaidia wazazi wake kwa upande wa karo.
"Nilikunywa soda ya Fanta Orange na nikakuta nimeshinda zawadi hii ya Milioni moja," alisema
Mmoja ya washindi wash.100,000, Muhidin Mushi ambaye anafanya shunguli za kuosha magari Mererani, anasema amefurahi sana kuwa wa mshindi kwani fedha hiyo itamsaidia kujikimu kimaisha.
Akizungumza mjini Moshi wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa Bonite Bottlers Christopher Lourick alitoa wito kwa wateja wa Coca-Cola kuendelea kunywa soda ya Coca-Cola pamoja na jamii yake ili kuibuka washindi.
Promosheni ya Vuta Mkwanja na Coca-Cola ilizinduliwa Julai 10, mwaka huu na itaendelea hadi Septemba mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment