16 November 2010

Mbatia wahi mahakamani-Mdee.

Na John Daniel, Dodoma

MBUNGE wa Kawe kupitia Chama cha Dermokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bi. Halima Mdee amevunja ukimya na kumtaka aliyekuwa mgombea ubunge wa
jimbo hio kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia kuharakisha kwenda mahakamani.

Akizungumza na Majira mjini hapa jana, Mbunge huyo alisema anasikitishwa na hatua ya Bw. Mbatia kudai kuwa ushindi wake si halali na kumtaka awahi mahakamani ili akamvue nguo kwa kuanika mbinu zake za kumsaliti, licha ya wote kutoka kambi ya upinzani.

"Ninachosema ni kwamba Mheshimiwa Mbatia kama anataka kwenda mahakamani awahi, kwanza atathibitisha kuwa yeye ni pandikizi aliyetumwa kunivurugia ushindi, lakini pia nitaweka hadharani mambo aliyonifanyia ambayo niliamua kukaa nayo tu ili yaishe kwa
kuwa wote ni wapinzani," alisema Bi. Mdee.

Alisema wakati wakifanya kampeni jimboni humo alisikia maneno mengi dhidi ya Bw. Mbatia kuwa anafanya kampeni za kummaliza yeye  badala ya kupambana na Chama cha Mapinduzi ambayo ndio alikuwa adui wao mkubwa katika jimbo hilo.

"Hata wewe unajua wazi kuwa adui yetu mkubwa ilikuwa ni CCM kutokana na jinsi ilivyodidimiza maisha ya Wanakawe, lakini nilishangaa mwenzangu badala ya kushirikiana nami kummaliza adui, alikuwa akitaka kunimaliza mimi, ndio maana nasema akifanya hivyo atadhitibisha kuwa yeye ni pandikizi kweli," alisisitiza.

Alisema hivi sasa anajiandaa kuanza kushughulikia kero ya Wanakawe na kusisitiza kauli yake kuhusu maeneo ya wazi yaliyoporwa na wajanja kuwa ni lazima yarejeshwe, vinginevyo wahusika wataishia mkononi mwa vyombo vya dola.

"Hivi sasa ni muda wa Wanakawe kujiandaa kunipa ushirikiano wa kutosha kushughulikia kero zao, nilidhani mwenzangu naye anajiandaa kushirikiana nami kuboresha maisha ya wananchi kumbe anataka kwenda mahakamani, basi awahi ili kuokoa muda," alisisitiza.

14 comments:

  1. Mdee nakukubali dada yangu,huyo Mbatia ana jipya wala usipoteze muda wako valuable kujibizana naye,yeye na mbunge wa TLP tunawajua vizuri,hakuna upinzani hapo,akienda mahakamani tutakuchangia hela ya wakili sisi wananchi wenye upeo kidogo sasa hivi hatumu hesabu Mbatia kwenye orodha ya wapinzani nchi hii.

    ReplyDelete
  2. Bravo Halima, nakuaminia mwanangu, achana na Mbatia hana lolote huyo, anajua kulamba viatu vya CCM tu nakujifanya anajua kila kitu. Ningewashangaa sana wananchi wa Kawe kama wangemchagua Mbatia.

    ReplyDelete
  3. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 16, 2010 at 10:41 AM

    n'kwei kabisa!

    ReplyDelete
  4. Kwani jamaa kaacha UKUTA?

    ReplyDelete
  5. Big Up Mdee, wana mvomero wanafahamu juhudi zako, maana unayo hata mafaili ya wana mtibwa ukiyafanyia kazi na umesababisha Diwani wa Mtibwa Chadema) Bi. Tusekile Dicson Mwakyoma, kushinda kwa kishindo ingawa, kura za mbunge zimechakachuliwa. tupo pamoja nawe tutakuchangia fedha ya wakili hadi ukamilifu wa dahari. si kila asemaye Bwana Bwana ni muumini wa Mungu.

    ReplyDelete
  6. Mbatia tunamfahamu vurugu zake ni chokochoko sana kaisambaratisha NCCR enzi zake kwa ajili ya madaraka, lazima tumwambie ukweli. Sasa anakuja kutuliza hasira zake kwa Mdee tulia dada muache achonge akitaka aende kugombea ubalozi wa nyumba kumi huko kwao.

    ReplyDelete
  7. Haya maajabu ya Musa,kwa nini watu hawataki kukubali kushindwa?Kwanza siku zote Mbatia haeleweki!

    ReplyDelete
  8. Dada Halima,wasikunyanyase kisa mwanamke.simama.toa a/c no,tutakuchangia wakili.wewe kijana mleta mapinduzi achana na mapandikizi.tena ashindwe,kwa jina la yesu

    ReplyDelete
  9. Naona jamaa UKUTA haachi!

    ReplyDelete
  10. Sana tu, Halima Mdee, ninyi CHADEMA, DP,na CUF ndio wapinzani wa kweli. Mbatia na vyama ni mapandikizi.Hakuna mtu asiyewajua na watajitaja punde kama sio kujionyesha wazi. Mwenzao Mrema kavunja ukimya kajitaja, Mbatia atafuata. Wapo hapo mahususi kuvuruga upinzani.Mbatia hana tofauti na Mrema. Pambana dada nasi wananchi tupo pamoja nawe.

    ReplyDelete
  11. MIMI KWANZA NAMSHANGAA MBATIA, NI MUDA MREFU ANACHONGA SANA KUHUSU KWENDA MAHAKAMANI, MBONA HATAKI KWENDA???? HATUTAKI THEORETICAL FIGURES, WE NEED PRACTICAL ISSUES, SASA HIVI HATUDANGANYIKI!!!!!!!! MBATIA KAMA VIPI JIPOTEZEE, AIBU HIYO, KWA MDEE UMEINGIA CHOO CHA KIKE ATAKUUMBUA, OOOHOO!!! MIMI SIPO

    ReplyDelete
  12. Mbatia ukitia mguu mahakamani maanake unapingana na demokrasia ya wengi majibu yake jina lako 2015 ndio kabisaa halitapata wa kuunga mkono. Stop that agenda start afresh to restore peoples trust , Mdee is Peoples Choice for now! Get head start!

    ReplyDelete
  13. Mbatia acha kutokota kama si kuchemsha!

    ReplyDelete
  14. Mbatia acha kuchonga bwana,unalalamika nini? umeshindwa basi tuliza mayanga chini endelea kukalia hapo nccr tu uhahe kama bata aliyekosa bwawa la kuogelea........mdee chapa kazi kwa maendeleo ya wanawake mama.0

    ReplyDelete