30 July 2012

Serikali yaombwa kuchangia mfuko wa tiba mbadala



Na Mwandishi Wetu

SERIKALI na wadau mbalimbali, wameombwa kuchangia mfuko wa utoaji elimu kuhusu matibabu ya tiba mbadala.

Ombi hilo limetolewa Dar es Salaam jaana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Tiba Asili na Utafiti cha Boresa, Bw. Boniventura, wakati akizungumza na Majira kuhusu maadhimisho ya dawa za asili yanayotarajiwa kufanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia Agosti 27-30 mwaka huu.


Alisema  maadhimisho hayo yatawashirikisha wadau mbalimbali wa masuala ya tiba mbadala na kufanya maonesho ya dawa.

“Ili kufanikisha tiba madala isonge mbele, Serikali na wadau mbalimbali tunaomba wachangie mfuko huu ili jamii iweze kufahamu na kuthamini umuhimu wa tiba za asili.

“Wapo baadhi ya wananchi hawatambui umuhimu wa tiba hizi na kushindwa kupata matibabu kutokana na kuwa na imani potofu ambapo hivi sasa kwa kushirikiana na wadau, tumeazimia kutoa elimu katika maeneo mbalimbali nchini,” alisema.

Bw. Mwalongo alitoa wito kwa jamii kutoinyanyapaa tiba asili badala yake watoe kasoro zilizopo kwani katika baadhi ya nchi duniani zimekuwa zikinufaika na ukuaji uchumi wao kutokana na tiba za asili.

“Tulitarajia maadhimisho hayo yangekuwa na mwamko mkubwa ili jamii iachene na imani potofu kuhusu tiba asili lakini Serikali imedai haina fungu la kutosha ili kuyatangaza na kututaka tuwe na programu endelevu,” alisema Bw. Mwalongo.

Alisema uchumi wa dunia umekuwa kutokana na biashara hiyo kwa dola za Marekani bilioni 60 kutokana na tiba asili lakini Tanzania haimo katika uchangiaji biashara hiyo.


No comments:

Post a Comment