27 July 2012
Mgomo wa daladala batili-SUMATRA
Na Agnes Mwaijega
BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (SUMATRA-CCC), limesema mgomo wa daladala uliotangazwa na Chama cha Wamiliki wa Daladala Mkoa wa (DARCOBOA) ni batili.
Tamko hilo limekuja siku moja baaada ya DARCOBOA, kutangaza mgomo wa kutosafirisha abiria kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa madai ya kupinga manyanyaso wanayofanyiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA).
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bw. Oscar Kikoyo, aliyasema hayo Dar es Salaam jana na kusisitiza kuwa, daladala zote ambazo zitashiriki mgomo huo wamiliki wake watashtakiwa mahakamani.
Alisema watoa huduma wote wenye mkataba na SUMATRA, hawapaswi kusikiliza maamuzi ya vyama ambavyo ambavyo havina mikataba na mamlaka hiyo.
“Tumejiandaa kikamilifu kuwashtaki wote watashiriki mgomo huu kwani kwa mujibu wa tataribu na kanuni za SUMATRA, mtoa huduma hadhibitiwi na DACOBOA, chama hiki kipo chini ya mamlaka yetu hivyo ni wazi mgomo huu ni batili,” alisema.
Aliongeza kuwa, DARCOBOA wanapaswa kufuata taratibu, kanuni na sheria za utoaji huduma kama zilizivyoanishwa na SUMATRA badala ya kuhamamsisha mgomo ambao utasababisha madhara makubwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri.
Kwa mujibu wa Bw. Kikoyo, SUMATRA-CCC imesikitishwa na madai yaliyotolewa na DARCOBOA kuwa SUMATRA inatumia walinzi shirikishi kukamata magari yao.
Alisisitiza kuwa, baraza hilo halioni kama hiyo ni hoja ya msingi inayowafanya wamiliki hao kutangaza mgomo kwani wanaamini wanaokamatwa ni wale wenye makosa.
Aliwataka watumiaji huduma ya usafili wa daladala kutokuwa na wasiwasi na mgomo uliotangazwa na kuwaomba kutoa taarifa za magari yote ambayo yatagoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment