31 July 2012
Abiria afariki katika ajali ya pikipiki Dar
Neema Kalaliche na Jane Hamalosi
ABIRIA wa pikipiki yenye namba za usajili T668 BXL, aina ya Jinghen, Mwanaidi Saidi (25), amefariki dunia baada ya pikipiki hiyo kugongwa na gari ambalo halijafahamika.
Ajali hiyo imetokea eneo la Santiago, Barabara ya Msongola, Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, David Misime, alisema pikipiki hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Bw. Mudy Wambura (28), na ilikuwa ikitoka eneo ya Msongola kwenda Mbande.
Alisema pikipiki hiyo iligongwa kwa nyuma na gari isiyofahamika wala namba zake ambapo abiria huyo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Temeke.
“Mwili wake umehifadhiwa katika hospitali hiyo na jitihada za kuitafuta gari iliyosababisha kifo hicho na dereva wake zinaendelea,” alisema Kamanda Misime.
Katika tukio jingine, watu 13 baada ya kukutwa na misokoto ya bangi pamoja na pombe haramu ya gongo katika maeneo tofauti wilayani humo.
Kamanda Misime alisema polisi walifanya msako katika maeneo tofauti na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na kete 119 za bangi, puli 13 na gongo lita 11.
Aliwataja baadhi ya watuhumiwa kuwa ni Bw. Mohamedi Issa (23), Bw. Kessy Ngoma (31), Bw. Saidi Kaoneka (34), Bi. Upendo Amani (27) na Bi. Mwajuma Seleman (19), ambao wote ni wakazi wa Karakata Majoe na wengine kutoka Tungi Mji Mwema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment