24 July 2012

Pugu mabingwa kombe la Stakishari



Na Heri Shaaban

TIMU ya soka ya Kata Pugu imeibuka mabingwa wa mashindano ya Polisi Jamii katika fainali ya kugombea kombe la Stakishari Ukonga, Wilayani Ilala.

Katika fainali hiyo mshindi wa pili ni timu ya Kata Chanika na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Segerea.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam juzi,Mkuu wa Polisi Wilaya Ukonga Stakishari Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Pili Mande alisema  mashindano hayo yalianza tangu Julai 16, mwaka huu.

"Mashindano haya yalianza Julai 16, na yalishirikisha timu nane kutoka katika Jimbo la Ukonga na Segerea  lengo la mashindano haya ni kutekeleza zana ya polisi jamii katika sekta ya michezo kwa kutoa elimu na mafunzo ya mbinu ya kupambana na waarifu,"alisema Pili.

Pili alitaja timu zilizoshiriki mashindnao hayo kuwa ni Chanika,Pugu,Kipawa ,Kitunda,Kinyerezi,Ukonga na Segerea.

Alisema katika kutekeleza zana ya Polisi Jamii amefanikiwa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi Mtaa kwa Mtaa na kujenga urafiki ili waweze kushirikiana kwa pamoja.

Kwa upande wake Kanali Mstaafu Idd Kipingu aliwaomba wanamichezo waendeleze soka ili waweze kusonga mbele kwa kukuza vipaji vyao, kwani mpira ni ajira,undugu na wengi wamefanikiwa kupitia mpira.

Pia Kipingu alikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu ambapo Pugu,Chanika na Segerea zote zilikabidhiwa kila mmoja mpira mmoja na seti moja moja ya jezi.

No comments:

Post a Comment