27 July 2012

Halmashauri kutegemea wakala kukusanya kodi kikwazo serikali kuendesha shughuli kwa kujitegemea.


Na Willbroad Mathias

SERIKALI ya Tanzania ni kati ya serikali za kiafrika ambazo kwa kiasi kikubwa zinategemea kuendesha shughuli zake za maendeleo kutoka kwa wafadhili mbalimbali wa nchi za Magharibi.

Hali hii inatokana na kasumba iliyojengeka kwamba nchi nyingi za kiafrika bado hazina uwezo wa kujiendesha zenyewe bila kupata msaada kutoka nje ya nchi.


Hata hivyo ukiangalia kiundani madai hayo ya nchi za kiafrika kutokuwa na uwezo wa kujiendesha bila kutegemea msaada wa nchi za nje yanaweza kuwa siyo ya kweli kulingana na tafiti mbalimbali ambazo zimefanyika na kubaini chanzo cha tataizo hilo.

Bw.Andendekisye Mwakabalule ni Katibu Mtendaji wa kituo kisicho cha kiserikali kinachojishughulisha na utafiti na uchunguzi juu matumizi mabaya ya mali za umma (Center  For Research Fraud and Ivestigation (CRFI) cha jijini Dar es Salaam,pamoja na mambo mengine anaeleza chanzo cha serikali kushindwa kujitegemea na badala yake bajeti yake kwa asilimia kubwa kutegemea wafadhili.


Bw. Makabalula anasema kuwa pamoja na kuwa bageti ya mwaka wa fedha 2012/2013 imeshasomwa na Waziri wa Fedha Dkt.William  Mgimwa na kuridhiwa na wabunge jambo  moja kubwa lililoleta mjadala ni jinsi serikali ya Tanzania inavyojikita kwenye kupandisha kodi kwenye vinywaji na  kodi katika mishahara ya watumishi.


Anasema katika utafiti tuliofanya katika Halmashauri za Kibaha, Bagamoyo na Manispaa za Temeke, Ilala, na Kinondoni inaonesha  kitendo cha uongozi wa halmashauri hizo kushindwa kusimamia ukosanyaji kodi ndicho chanzo kikubwa kinachoifanya serikali ishindwe kuendesha shughuli zake kwajitegemea.


Katibu Mtendaji huyo wa CRFI anasema kuwa kati ya asilimia 80 ya watu waliohoji walisema kuwa kama halmashauri zingekuwa zinakusanya kodi bila ya wakala, mapato yangepatika makubwa zaidi huku asilimia 75 ya watu hao ikieleza kuwa  wengi wa wakala wanapatikana kwa njia zisizo sahii hivyo kufanya mapato mengi yaende kwenye mifuko ya watu waliowapata tenda hiyo.

"Asilimia 95 ya waliohojiwa walisema serikali inatakiwa kufanya tathmini ya jinsi ya kuboresha mapato katika halmashauri zote, maana utafifi unaonesha kwamba, kama halmashauri zingekuwa zinaachiwa vyanzo vyote vya mapato, pasingekuwa na haja ya kupata ruzuku kutoka serikali kuu wala kuomba pesa kutoka kwa wahisani,"anasema Bw.Mwakalule.


Anasema wananchi haoa wakaenda mbali kwa kutolea mfano wa nchi za wenzetu kwamba halmashauri zao zinapeleka mapato katika serikali kuu kwa sababu vyanzo vyote vya mapato katika halmashauri zinamilikiwa na halmashauri zenyewe. 


Anasema katika utafiti huo ulionesha kwamba  kwamba, halmashauri zingekuwa zinakusanya mapato zenyewe mapato yangedhibitiwa kwani mtumishi akigundulika anafuja pesa  anaweza kuchukuliwa hatua haraka kuliko wakala, maana hii inachukua mlolongo wa kusimamisha wakala na taratibu za kisheria.  



Katibu Mtendaji huyo CRFI anasema katika bajeti ya serikali, imejikita sana kwenye kupandisha kodi katika vinywaji na mishahara, lakini ingejikita sana kwenye kusimamia mapato katika halmashauri na serikali za mitaa lakini anafikiri kusingekuwepo mabishano mengi katika kupitisha bageti kuu.


"Chukulia mfano wa bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012, Manispaa ya Temeke ilipanga kutumia shilingi  bilioni 72, na bilioni 19 zilitokana na mapato ya vyanzo vya ndani ambazo kwa mtazamo ni vyanzo vidogo sana na walivuka malengo. Vyanzo vya ndani katika manispaa hii  ya Temeke ni asilimia 26,"anafafanua Bw. Mwakabalule.




Anafafanua zaidi kuwa katika Manispaa ya Kinondoni, katika mwaka wa fedha wa 2011/2012 walipanga bajeti ya shilingi bilioni 92 kati ya hizo shilingi bilioni 23 ammabzo ni sawa na asilimia 25 zilitokana na vyanzo vya ndani.

Anasema kuwa hivyo ni vyanzo vichache ukilinganisha na vyanzo ambavyo serikali kuu inakusanya. 

Anaeleza kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ilipanga bajeti ya Shilingi bilioni 37 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012 ambayo walisema kama serikali kuu isingekuwa inaingilia kati katika ukusanyaji wa  mapato ingefikia lengo bila ya kupata ruzuku kutoka serikalini.


Anatolea mfano  kwamba katika kutengenenza barabara ya Msata Bagamoyo, Moram na maeneo mengine, halmashauri hiyo isingekuwa imeingiliwa ingepata mapato ya ndani ya kiasi cha Shilingi milioni 37 kwa mwezi.


"Pia inaonyesha kwamba asilimia 98  ya wakala wanaokusanya mapato katika halmashauri zote zilizotembelewa kuwa ni wakala wa waliowapa tenda. Hii inaonyesha kwamba  mapato mengi yanaenda kwenye mifuko ya watu binafsi,"anaeleza kiongozi wa utafiti huo.


Anasema ili kuinusuru nchi na kizazi kijacho, wabunge  watunge sheria ya kudhiti mapato na kuziachia halmashauri zikusanye mapato yote bila kuingiliwa.


Bw. Mwakabalule anasema kama halmashauri zinaweza kukusanya asilimia 25  kwa vyanzo vichache walivyonavyo, hivyo wakiachiwa asilimia 100 watajitegemea kabisa na walivyosema hataweza hata kuomba pesa zingine kutoka kwa wahisani.


Anasema kuwa kwa kutumia  njia hiyop hata ukwapuaji utapungua kwa sababu watakuwa na majukumu ya kuhakikisha malengo yanatimia.


No comments:

Post a Comment