26 July 2012
Muuza nyama ajisaidia chupa 12 za mikojo buchani
Na Patrick Mabula, Kahama
MFANYABIASHARA anayeuza nyama katika bucha iliyopo mjini Kahama, mkoani Shinyanga, Bw. Said Mayala, amekamatwa baada kukutwa na mkojo chupa 12, iliyowekwa kwenye chupa za ujazo wa lita 1.5,.
Tukio hilo limetokea juzi baada ya kukutwa na Maofisa Afya wa Halmashauri ya mji huo katika Soko Kuu akiwa na chupa hizo ambazo alizitumia kujisaidia haja ndogo ndani ya bucha.
Maofisa hao walikuwa wakifanya ukaguzi wa usafi katika bucha za nyama sokoni hapo ambapo ofisa mmoja wapo, Bw. James Mwalusi, alisema mkojo huo waliukuta kwenye vibanda viwili namba 119-118 vinavyomilikiwa na Bw. Mayala.
Mwandishi wetu alishuhudia mikojo hiyo Bw. Mwalusi aliongeza kuwa, kutokana na tukio hilo wameamua kumfungia kufanya biashara ya kuuza nyama, kwenda kuzitupa na wanatarajia kumfikisha mahakamani.
Mwenyekiti wa Wafanyabishara wa Maduka ya Nyama mjini hapa, Bw. Faraji Mhamed, aliyekuwepo enbeo la tukio, alilaani kitendo hicho na kusema si ustaarabu.
Hivi karibuni, Majira liliripoti juu ya malalamiko na kero ambazo zinawakabili wafanyabishara wa soko, stendi kuu na wenye vibanda vya maduka kuwa eneo hilo halina choo cha kisasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment