30 July 2012

Azam FC: Haituumizi Ngassa kushangilia Yanga


Na Mwali Ibrahim

KLABU ya Azam imedai kutokushtushwa na kitendo cha mchezaji wao Mrisho Ngassa kushangilia bao la timu yake ya awali ya Yanga lilowapeleka fainali.

Ngassa alionekana kushangilia goli walilofunga Yanga na pia alivaa jezi ya timu hiyo na kuwashangilia ikiwa ni kuonesha mapenzi yake na timu hiyo na hata kuripotiwa kutaka kurudi katika timu hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa klabu hiyo Jafari Idd alisema kitendo cha Ngasa kuishangilia Yanga  ni mapenzi yake na timu hiyo hivyo wao haiwasumbui, kwani bado wanamtambua ni mchezaji wao.

"Kama alishangilia hilo ni juu yake na mapenzi yake na labda anajua nini kilichopo katika mkataba wake na hawawezi kumzuia kushangilia," alisema.

Akizungumzia kuhusu kuwekwa benchi kwa mchezaji huyo alisema Ngassa ni mchezaji aliyecheza mechi nyingi katika ligi zilizopita hivyo kukaa kwake benchi sio kama hana kiwango hiyo ni mipango ya kocha katika kuwaweka sawa wachezaji wake.

Aliongeza kuwa, timu yao ipo vizuri kukabiliana na Yanga katika fainali ya Kagame leo  na hakuna majeruhi hata mmoja.

No comments:

Post a Comment