31 May 2012
TAIFA STARS YAPAA IVORY COAST LEO
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla (kushoto) akimkabidhi bendera nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja Dar es Salaam jana ajili ya kwanda nayo Ivory Coast kuipeperusha katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2014 wa pili kushoto ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe ambao ni wadhamini wa timu hiyo, Kocha Mkuu Kim Poulsen na katikati ni Mwenyekiti wa BMT, Deoniz Malinzi. Picha na Rajabu Mhamila.
January Makamba awafunda wananchi
Na Yusuph Mussa, Lushoto
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bw. January Makamba amewataka wananchi wa Tarafa ya Mgwashi mkoani Tanga kutumia fursa mbalimbali ikiwemo kufanya biashara na Halmashauri mpya ya Bumbuli badala ya kuwaachia wageni waiuzie halmashauri hiyo hadi karatasi za ofisini.
UTALII
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana, kuhusu hali ya usalama Visiwani Zanzibar baada ya Serikali kudhibiti vikundi vya watu waliosababisha vurugu na kukanusha taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari vya nje vilivyoripoti habari za kupotosha watalii. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Bw Richard Rugimbana. (Picha na Charles Lucas)
WATUHUMIWA
Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa wakati wa operesheni maalumu ya kukagua mita za LUKU za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa eneo la Tabata, Dar es Salaam jana. Hata hivyo waliachiwa baada ya kubainika kuwa si wahusika. (Picha na Prona Mumwi)
MACHINGA
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakichagua nguo na mabegi ya kuhifadhia nguo katika Soko la Karume, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala jana. Baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo wameahidi kuhamia kwenye jengo la biashara la Machinga Complex iwapo amri ya kuhama itatekelezwa ipasavyo. (Picha na Peter Twite)
Watoto watumikishwa wilayani Mbarali
Na Esther Macha, Mbeya
LICHA ya Serikali kupiga vita ajira kwa watoto hususan wanafunzi bado
tabia hiyo inaendelea kwa wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambapo kundi hilo la watoto limeshindwa kuhudhuria masomo kwa kufanya kazi katika
mashamba mbalimbali wilayani humo.
30 May 2012
POOL
Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwingi akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya St. Agustine, Jimmy Nicas baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition 2012 yaliyomalizika mkoani Iringa mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool Tanzania (TAPA) Fred Mushi. Na Michael Machella
Serikali yabainika kuchelewesha vitabu vya bajeti 2012 na 2013
Na Godfrey Ismaely, Dar es Salaam
ZIKIWA zimebakia siku chache kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingia katika vikao vya Bajeti, mwaka wa fedha 2012 na 2013 baadhi ya wanaharakati wamedai kusikitishwa na uwajibikaji mdogo wa Serikali hasa kuchelewa kutoa vitabu vya makadirio hayo.
MCHEZAJI WA MPIRA WA KIKAPU NBA
Mchezaji wa mpira wa kikapu anyechezea Ligi ya NBA ya Marekani, Hasheem Thabeet akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kliniki ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Sprite itakayofanyika katika viwanja vya Don Bosco Upanga, Dar es Salaam kuanzia keshokutwa. Na Mpigapicha Wetu
Mhasibu Lindi kortini kwa kumjeruhi mkewe kwa pasi
Na Said Hauni, Lindi
MKAZI wa Kata ya Wailes katika Manispaa ya Lindi Bw. Mwanzaga Mbowi amefikishwa Mahakama ya Mkoa wa Lindi akikabiliwa na shitaka la kumjeruhi mkewe kwa kumchoma na moto wa pasi.
Bw. Mboi ambaye ni Mhasibu katika Manispaa hiyo alipandishwa kizimbani Mei 28, mwaka huu na kusomewa shitaka lake na Mwanasheria wa Serikali, Bi. Mwahija Ahamadi.
MADAI
Viongozi wa Kamati inayofuatilia madai ya waliokuwa wafanyakazi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kuvunjika kwaka 1977, wakitoa taarifa ya kuungana katika madai yao, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (HLRC) Dar es Salaam jana. Kushoto ni Bw Ahmed Kabunga na Alfred Kinondo. (Picha na Charles Lucas)
Waziri aanika uozo wa wahisani mbalimbali
Na Pamela Mollel, Arusha
IMEELEZWA kuwa bajeti nyingi za nchi za Afrika zimekuwa tegemezi kwa wahisani jambo ambalo linachangia uwepo wa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa maslahi ya wahisani husika.
Pia Serikali imetakiwa kutumia utawala bora wa fedha kwa wananchi wake na matumizi sahihi ya mali asili ili ziweze kuwa na tija kwa vizazi vijavyo na kuitumia demokrasia katika kukuza pato la wananchi.
Posta waanzisha duka la kununua, kubadilisha fedha za kigeni Dar
Na Sangalwise Abia, Dar es Salaam
SHIRIKA la Posta Tanzania limefungua biashara ya kuuza na kununua
fedha za kigeni (Bureau de change) katika ofisi zake zilizopo Posta
Mpya Mtaa wa Azikiwe jijini Dar es Salaam.
NISHANI
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishina Augustino Nanyaro kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimvisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Nne, Mkaguzi Msaidizi wa Magereza, Bi. Mariam Kamangu. wakati utoaji nishani hizo, Dar es Salaam jana. (Picha na Peter Twite)
Wanyange Miss Tanzania watakiwa kuchukua fomu
Na Mwali Ibrahim
WANYANGE wanaotaka kushiriki katika mashindano madogo ya kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kuingia katika kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 4 mwaka huu.
ALBINO
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Under The Same Sun, Bw. Peter Ash (aliyeinua kofia), akiwahimiza watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino), kuvaa kofia ili kujikinga na jua, alipotembelea kituo chao kilichoko Shule ya Msingi Jumuishi ya Buhangija, mkoani Shinyanga hivi karibuni. (picha na David John)
Polisi na mahakama Handeni lawamani
Na Mashaka Mhando, Tanga
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wamesema idara za polisi na mahakama zina wajibu mkubwa wa kumaliza tatizo la utoro na mimba shuleni badala ya kuwatupia lawama watendaji wa vijiji na kata.
Shule zajengewa uwezo wa kompyuta na vitabu
Na Eliasa Ally, Iringa
MBUNGE wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa Prof. Peter Msolla amekabidhi msaada wa kompyuta tatu na vitabu vya kiada, msaada wenye thamani ya shilingi milioni tisa uliotolewa na Kampuni ya Simu Airtel Tanzania katika shule tatu za sekondari jimboni humo.
Wahimizwa kuzingatia lishe bora muda wote
Na Suleiman Abeid, Shinyanga
IMEELEZWA kuwa maendeleo na mafanikio ya uchumi wa nchi yoyote duniani hutokana na wananchi wake kuwa na afya bora zinazowawezesha kufanya kazi za uzalishali mali pasipo matatizo.
Hali hiyo ilibainishwa juzi na Bw. Billie Edmott ambaye ni Ofisa wa Uchumi na Uzalishaji Mali mkoani Shinyanga katika uzinduzi wa duka namba 103 la Kampuni ya TIENS inayojishughulisha na usambazaji wa virutubisho vya mwili wa binadamu.
Mashujaa yakomba hadi Meneja Twanga
Na Zahoro Mlanzi
BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa, imetangaza rasmi kumnasa Meneja wa African Stars (Twanga Pepeta), Matrin Sospeter kujiunga na bendi hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa bendi hiyo, Charles Gabriel 'Chalz Baba' alisema ana furaha kuona kiongozi huyo amejiunga nao na ana imani itazidi kufanya vizuri katika anga ya muziki wa dansi.
Changamoto zawaandama wauguzi mbalimbali
Na Salma Mrisho, Geita
IMEELEZWA kuwa mazingira magumu ya kazi yanayowakabili wauguzi hususan upungufu wa watumishi wa kada hiyo na malipo kidogo ni mojawapo ya changamoto zinazowafanya kutowajibika ipasavyo katika kazi zao.
Hayo yalibainishwa hivi karibuni kwenye kongamano la siku mbili na mkutano wa 12 wa Chama cha Wauguzi (TANNA) Mkoa wa Shinyanga ulioenda sambamba na kuwaaga baadhi ya wauguzi waliohamishiwa mikoa ya Geita na Simiyu.
NCCR-Mageuzi wavuna wanachama Mtwara
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
CHAMA cha NCCR-Mageuzi mkoani Mtwara kimevuna wanachama wapya 2,517 katika Jimbo la Mtwara Mjini.
Takwimu hizo zilitolewa jana na Mjumbe wa Halmashauri ya chama hicho Bw. Danda Juju alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.
CHADEMA waishutumu CCM
Na Allan Ntana, Tabora
KATIBU Mwenezi wa CHADEMA Bw. Ali Mwakilima amewataka wananchi kutobweteka na ulaghai wa CCM pindi unapokuja uchaguzi kwa kuwahadaa kwa fulana, kofia na kanga.
Kauli hiyo aliitoa juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Kijiji cha Igunda Kata ya Ifucha, Manispaa ya Tabora ambako kulikuwa na
mkutano wa CHADEMA.
Albino wana uwezo wa kufanya kazi zote'
Na David John, Aliyekuwa Mwanza
IMEELEZWA kuwa jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Albino wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa ili kuhaakisha maendeleo.
Hayo yalielezwa hivi karibuni mkoani Mwanza na Bi.Vicky Ntetema ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Same Sun hapa nchini, baada ya kutembelea mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kujionea changamoto zinazowakabili watu hao.
Madega ajana katiba mpya Yanga
Na Suleiman Mbuguni
BAADA ya wanachama wa Yanga, kushinda vita ya kumwondoa Mwenyekiti wa klabu hiyo madarakani na kutakiwa kufanya uchaguzi mdogo Mwenyekiti aliyeondoka kabla ya uongozi huu, Imani Madega amesema ili klabu hiyo kongwe ifanikiwe ni lazima kufanyike marekebisho ya katiba.
Kocha Stars awaota Drogba, Toure
Na Zahoro Mlanzi
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen amesema uwezo binafsi wa wachezaji Didier Drogba na Yahya Toure wa Ivory Coast utawapa wakati mgumu katika mechi ya Jumamosi itakayopigwa jijini Abidjan.
29 May 2012
Watanzania washauriwa kutumia mkutano wa AfDB kujitangaza
Pamela Mollel na Jane Edward, Arusha
WATANZANIA wametakiwa kujitangaza kiuchumi kupitia mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ulioanza jijini Arusha ambao umewajumuisha marais sita wakiwemo magavana wa nchi mbalimbali za Afrika.
Tushirikiane kukomesha ukatili kwa wajawazito
WALI ilikuwa ikifikirika kuwa kazi ya uuguzi ni wito, hivyo kila anayefanyakazi hiyo ana sifa ya kuwa na ukarimu, upendo, upole na sifa zingine.
Kadri siku, miezi hadi mwaka inavyokwenda ndivyo sifa hizo zinavyotoweka.
Kutokana na ukosefu wa ajira nchini vijana wamejiamulia kujiingiza katika fani mbalimbali licha ya kutokuwa na sifa zinazostahili kuingia kwenye fani husika.
Kifukwe, Falcon, Karigo wanukia Yanga
Na Zahoro Mlanzi
SIKU 2 baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuitaka Klabu ya Yanga kufanya uchaguzi wa viongozi wapya Julai 15 mwaka huu, homa ya uchaguzi huo imeanza kupanda huku viongozi waliowahi kuiongoza klabu hiyo, Francis Kifukwe, Godson Karigo na Ahmed Falcon wakitajwa kuwania nafasi za juu.
New Team mabingwa Copa Coca-Cola Ilala
Na Amina Athuman
MICHUANO ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ngazi ya wilaya, Kanda ya Ilala yalimalizika juzi kwa New Team FC kuifunga timu ya Sanry FC kwa mikwaju ya penalti 6-5 katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mbunge aiokoa Korogwe United
Na Yusuph Mussa, Korogwe
MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Tanga, Mary Chatanda ameiokoa timu ya soka ya Korogwe United kuweza kushiriki mashindano ya Kanda, baada ya kuwasaidia sh. milioni moja za kuwapiga jeki katika michuano hiyo.
Ash aivaa Serikali mauaji ya albino
Na David John, Aliyekuwa Shinyanga
SERIKALI imeshauriwa kuwasaidia waandishi wa habari ambao wanaripoti habari za mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na siyo kuwawekea vikwazo vya kuwatisha pindi wanaporipoti habari hizo.
Mwito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Under The Same Sun Bw. Peter Ash mkoani Shinyanga baada ya kutembelea Shule ya Msingi Buhangija ambayo imefanywa kuwa moja ya kituo cha kulelea watoto wenye ulamavu wa ngozi.
NCCR-Mageuzi jino kwa jino na CCM
Na Mwandishi Wetu, Lindi
MSHAURI Mkuu wa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia, Danda Juju ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho amesema ni hatari wananchi kubadili mitazamo yao kisiasa kutokana na maisha magumu yanayowakabili.
Pamba yaondoka na matumaini kibao
Na Daud Magesa, Mwanza
MABINGWA wa zamani wa soka Tanzania Pamba ya Mwanza, imeondoka jijini hapa ikiwa na matumaini makubwa ya kufuzu fainali za Kanda ili kucheza Ligi Daraja la Kwanza.
Pamba ambao ni mabingwa wa soka Mkoa wa Mwanza, iliondoka juzi kwa basi la kukodi ikiwa na kikosi cha wachezaji wake wote chini ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ramadhan Muzzo na kuahidi ushindi.
Airtel yakabidhi vifaa vya michezo kwa DRFA
Na Elizabeth Mayemba
KAMPUNI ya simu za mikononi ya Airtel Tanzania imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu za vijana chini ya miaka 17 zitakazoshiriki mashindano ya Aitel Rising Stars, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho katika mikoa sita.
Mikoa ambayo itashiriki michuano hiyo ni Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Temeke na Kinondoni, ambapo kwa upande wa Ilala mechi zitakuwa zikichezwa Uwanja wa Airwing, Kinondoni Mwenge na Temeke mechi zitachezwa Uwanja Twalipo.
28 May 2012
VICOBA KIMANI
Diwani wa kata ya msongola ambaye pia ni Mwenyekiti wa Huduma za Uchumi za Jamii wa Manispaa ya Ilala, Bi.Angelina Malembeka (katikati) akipiga makofi pamoja na Mratibu wa Benki za Wananchi Vijijini (VICOBA) Tanzania, Bw.Aldo Mfinde, kulia na Mwenyekiti wa kikundi cha Mlimani Vicoba cha Ukonga jeshini, Bi.Shia Simba, wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho, Dar es Salaam juzi. (Picha na Charles Lucasa)
Ligi ya Taifa kuanza leo
Na Amina Athumani
LIGI ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa inaanza kutimua vumbi leo kwenye vituo vya Kigoma, Musoma na Mtwara.
Tamasha la Washindi wa Tuzo za Kili Music lafana Mtwara
Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani wakati wa shoo maalum ya Washindi wa Tuzo za Kili Music zilizofanyika juzi kwenye Uwanja wa Umoja,Mtwara.
Wananchi warudisha imani ATCL-Chizi
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Ndege nchini ATCL Bw. Paul Chizi amesema idadi ya abiria wa shirika hilo imezidi kuongezeka baada ya wananchi kuonesha uzalendo na imani kwa kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi huyo ilieleza hatua hiyo inatokana na mpango walionao wa kujizatiti ili kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri wa anga kupitia mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa shirika hilo.
Taifa Stars, Malawi zaingiza mil. 40/-
Na Mwandishi Wetu
MECHI ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames), imeingiza sh. 40,980,000 kutokana na mashabiki 9,365 walioingia uwanjani.
Mechi hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kujiandaa na mechi zao za kuwania kucheza Kombe la Dunia 2014 ambapo Stars itacheza na Ivory Coast Juni 2, mwaka huu na Malawi itaumana na Uganda.
Uchumi wa Tanzania umekua kwa asilimia 6.4 mwaka 2011'
Na Pendo Mtibuche, Dodoma
UCHUMI wa Tanzania umekua kwa asilimia 6.4 mwaka 2011 ambapo katika sekta ya usafirishaji na mawasiliano, ukuaji huo upo asilimia 11.3.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Beno Ndulu aliyasema hayo mjini Dodoma mwishoni mwa wiki wakati akitoa mada katika mafunzo elekezi yanayoshirikisha wakuu wa mikoa, wilaya na makatibu tawala wa mikoa.
KERO YA UZIO
Askari polisi akipita kando ya uzio ulioangushwa na upepo kwenye eneo la ujenzi wa Barabara ya Mtaa wa Manfierd na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo, Dar es salaam jana.Picha na Prona Mumwi.
Mbatia aeleza siri ya korosho kupanda bei
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia amesema bei ya zao la korosho imepanda kutokana na jitihada za chama chake na kuahidi kuendelea kuwapigania wakulima.
Bw. Mbatia alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti juzi mkoani Mtwara alipokuwa akifungua matawi ya chama hicho katika Jimbo la Mtwara Mjini.
Zanzibar yatwaa ubingwa wa judo Taifa
Na Amina Athumani
ZANZIBAR imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Judo katika michuano ya Taifa ya mchezo huo iliyomalizika jana katika Ukumbi wa Land Mark Hotel, Dar es Salaam.
Zanzibar ambao pia ni mabingwa wa Afrika Mashariki katika mchezo huo wamefanikiwa kutwaa ushindi wa jumla katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Chama cha Judo Tanzania Bara (JATA).
KUJITOLEA DAMU
Baadhi ya wakazi wa jiji wakijitolea damu kwa hiari katika kituo cha Huduma na Ushauri Nasaha cha FEMINA (HIP) wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMWI ya Chuo cha Mwalimu Nyerere Kigamboni, Dar es salaam juzi, ambayo huadhimishwa kila mwaka.
Sherehe Simba yafunika Dar Live *Makalla aipa mtihani
Na Speciroza Joseph
NAIBU wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Klabu ya Simba, amewataka wana-Simba kuendeleza umoja na mshikamano ili waendelee kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Viongozi wapya Yanga Julai 15 *Mwesigwa apewa 'mikoba' kwa muda
Amina Athuman na Zahoro Mlanzi
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeitaka Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Yanga, ianze mchakato wa kujaza nafasi zilizo wazi kuanzia Juni Mosi, mwaka huu na Julai 15 ifanye uchaguzi wa viongozi wapya.
25 May 2012
Kesi ya kupinga matokea zisifunguliwe kwa jazba
JANA Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,ilitoa hukumu ya kesi iliyokuwa imefikishwa mbele yake na aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bi. Hawa Ng'umbi, akipiga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Bw. John Mnyika.
Hukumu hiyo ilisomwa na jaji Bi. Upendo Msuya, na kubainisha kuwa mdai katika kesi hiyo ameshindwa kuithibitishia mahakama pasipo kuacha shaka juu ya madai aliyokuwa akiyalalamikia. Kesi ya kupinga matokea
zisifunguliwe kwa jazba
MALALE
Kaimu Mkurugenzi wa Idala ya Kinga katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Geoffrey Kiangi, akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, iliyohusu mafunzo ya uelewa wa ugonjwa wa Malale unaoambukizwa na Mbung'o. (Picha na Charles Lucas)
Elimu kwa vijana mwarobaini kupunguza umashini nchini
Na Stella Aron
NI miaka mingi sasa tangu kupata uhuru, kumekuwa na harakati mbalimbali za kuwawezesha wananchi kutambua ama kushiriki mambo mbalimbali ya kuboresha maisha ya jamii.
Serikali na asasi zisizo za kiserikali zimeshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuendesha harakati hizo.
Pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kuhamasisha wananchi, bado kuna mambo mengi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi zaidi hasa katika kipindi hiki cha utandawazi pamoja na kukabiliana na mfumo wa soko huria.
Watu wenye ulemavu wasema ya moyoni
Na Florah Temba, Kilimanjaro
JAMII imetakiwa kuondokana na mitazamo potofu juu ya watu wenye ulemavu, pamoja na kuzingatia mahitaji ya watu hao wakati wa ujenzi wa miundombinu ili kuwawezesha kupita kwa urahisi pasipo usumbufu.
Shule zilizozofanya vizuri Dar 'tiba' ya kuacha kusomesha nje
Na Reuben Kagaruki
MWAMKO wa wazazi kutambua umuhimu wa elimu unazidi kuongezeka nchini, ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Umuhimu wa elimu kwa watoto umechangia uwekezaji katika sekta hiyo kuongezeka kwa kasi ya aina yake. Jambo hili ni kati ya mambo ya kujivunia.
Waziri awakabidhi bendera Twiga Stars
Na Mwali Ibrahim
NAIBU Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makalla jana alikabidhi bendera ya taifa kwa timu ya taifa ya Wanawake ,Twiga Stars, kabla ya kuelekea Ethiopia kwa ajili ya Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC), zitakazofanyika Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea.
Kibaha wahitaji fedha kupanua sekta ya afya
Na John Gagarini, Pwani
KITUO cha Afya wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kinahitaji kiasi cha shilingi bilioni 13 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho ili kuwa hospitali ya wilaya hiyo.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jana Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Dkt. Kaniki alisema kuwa tayari ujenzi huo umeanza.
MAOMBII
Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste la LIFT HIM UP lililopo eneo la SanawariJuu mkoani Arusha Orche Mgonja (kushoto) akimuiombea mmoja wa waumini wa kanisa hilo Sabrina Masirori, wakati wa Maombi kwenye Kituo cha Maombezi maarufu Hospitali ya Rufaa juzi, aliyekuwa katika matatizo mbalimbali ya kiimani. (Picha na Richard Konga)
Watumishi wa umma kugoma Julai-TUGHE
Na Moses Mabula, Tabora
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya taifa (TUGHE) Bw. Ally Kiwenge ameitaka Serikali itekeleze kwa vitendo ahadi yake ya kupandisha mishahara kwa watumishi wa umma ifikapo Julai Mosi mwaka huu ili kuepusha mivutano baina ya pande hizo mbili.
Simba kuziba pengo la Mafisango *Wapo Santo, Kasule, Kije, Tegete naye yumo
Na Elizabeth Mayemba
SIMBA sasa imepania kufanya kweli katika usajili ambapo wanataka kuziba pengo la kiungo wao Patrick Mafisango aliyefariki katika ajali ya gari hivi karibuni, hivyo wameanza mazungumzo na viungo wanne kutoka Kenya na Uganda.
SIMBA sasa imepania kufanya kweli katika usajili ambapo wanataka kuziba pengo la kiungo wao Patrick Mafisango aliyefariki katika ajali ya gari hivi karibuni, hivyo wameanza mazungumzo na viungo wanne kutoka Kenya na Uganda.
24 May 2012
AJALI BUZA
Wasamalia wakimsaidia mwanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Buza, Prisca Abraham, aliyegongwa na lori Mitsubishi Fuso, wakati alipokuwa akivuka barabara eneo la Buza Kanisani, Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam jana. Wakazi wa eneo hilo wameshauri manispaa iweke matuta na alama za ' Pundamilia' zitakazowawezesha kuvuka kwa usalama. (Picha na Emanuel Godfrey)
Twiga Stars waelekea Ethiopia
Na Mwali Ibrahim
TIMU ya Taifa ya soka ya Wanawake 'Twiga Stars' inatarajia kuondoka nchini leo kuelekea Ethiopia kwa ajili ya kucheza mechi ya mchujo wa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia, mechi itachezwa Mei 27 mwaka huu, kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye jijini Dar es Salaam.
NMB MSAADA
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mbezi Juu, Bw. Pius Saye, akipeana mkono na Mkuu wa Mahusiano ya Jamii wa Benki ya NMB, Bi. Shy-Rose Bhanji, (wa pili kushoto), baada ya benki hiyo kutoa msaada wa madawati 50 yenye thamani ya Sh. Mil 5 kwa shule hiyo, Dar es Salaam jana, wengine kutoka kulia ni Meneja wa Tawi la Mlimani City, Bw. George Mwita na Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee. (Picha na Prona Mumwi)
Mama kizimbani kwa kujaribu
Na Said Hauni, Lindi
MKAZI wa Kata ya Mtanda Halmashauri ya Lindi Bi. Aluminata Alois Kimisa (38) amefikishwa mahakama ya mkoa huo akikabiliwa na shitaka la kujaribu kumuua mtoto mchanga aliyemzaa.
Mwanamke huyo alifikishwa mahakamani hapo Mei 22, mwaka huu na kusomewa shitaka lake na Mwanasheria wa Serikali Bw. Juma Maige.
SHIDA YA MAJI
Baadhi ya wafanyabiashara wa maji wakiwa kwenye foleni hali hiyo imekuwa ikiyakumba maeneo mengi kwa ukosefu wa maji na kulazimika kununua dumu moja kwa bei kati ya sh. 400 hadi 1000.(Picha kwa hisani ya mtandao).
Huduma za uhakika za maji safi bado tatizo
Na Agnes Mwaijega
PAMOJA na Maendeleo yaliyopatikana katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ,bado hazitaweza kufikia lengo la Milenia katika maji mpaka mwaka 2032.
Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo nayo bado inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa huduma za uhakika za maji safi na mazingira bora.
TFF watakiwa kutoa mafunzo kwa wataalum mashuleni
Na Mwali Ibrahim
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeombwa kutoa nafasi za mafunzo ya michezo kwa wataalamu wa michezo katika Shule za Msingi na Sekondari ili kukuza viwango vya wataalamu hao waweze kuibua vipaji zaidi.
Maombi hayo yalitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bishop Durning (Bishop Durning High School) ya Arusha Sarubare Lendisa, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi habari kuhusiana na umuhimu wa michezo shuleni.
BAJAJ
Meneja Usambazaji kwa Wateja Wakubwa wanaouza bidhaa za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Kaskazini, Bw. Fortunatus Alfred (kulia), akikabidhi kadi ya bajaj ya sh. mil 4, kwa Bi. Mary Kimario, aliyeshinda tuzo ya uwakala bora wa usambazaji na uuzaji wa bidhaa hizo, mjini Moshi, Kilimanjaro juzi. (Na Mpigapicha Wetu)
Kichocho bado tishio hapa nchini-Dkt.Njau
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WATU milioni 200 duniani wameambukizwa ugonjwa wa kichocho cha kibofu na tumbo katika nchi 76 huku wengine milioni 700 wakiwa katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.
Utafiti unaonesha kwamba kati ya watu 10 waliopimwa sita walibainika kuambukizwa ugonjwa wa kichocho cha tumbo hapa nchini ambapo kulingana na viwango vya Shirika la Afya Duniani (WHO) maambukizi hayo ni ya kiwango cha hali ya juu hivyo hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
MKATABA
Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde (kulia) akisaini mkataba wa kudhamini michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2012, huku mjumbe wa kamati ya mashindano Dar es Salaam Daudi Kanuti akishuhudia. Wengine ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano TFF Saad Kawemba.(Na Mpigapicha Wetu)
Timu ya taifa ya riadha Zanzibar yakabiliwa na ukata
Na Mwajuma Juma, Zanzibar
TIMU ya Taifa ya Riadha ya Zanzibar inayojiandaa na mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki na Kati inakabiliwa na ukata mkubwa ikiwemo vifaa vya kufanyia mazoezi.
Timu hiyo inajiandaa na mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar Es Salaam juni 7-8 mwaka huu.
MAOMBI
Askofu, Charles Gadi wa Kanisa la Habari Njema kwa Mataifa yote, akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuhusu kanisa hilo kuandaa mkutano wa kuombea Taifa, utakaoanza Mei 24 mwezi huu na kushirikisha dini mbalimbali kwenye Viwanja vya Biafra Kinondoni. (Picha na Charles Lucas)
UPDP walaani vurugu zilizotokea Rufiji
Na Rehema Maigala, Pwani
MWENYEKITI wa Chama cha Siasa UPDP Mkoa wa Pwani Bi. Asha Chuma amelaani uzembe wa Serikali kufumbia macho mauaji na uharibifu wa mali uliotokea hivi karibuni Ikwiriri wilayani Rufiji.
Akizungumza na gazeti hili jana Bi. Chuma alisema kuwa kitendo hicho kinaonyesha wazi kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inafumbia macho watumishi waovu na wasioelewa sheria za kazi zao.
Heineken yawapa burudani mashabiki UEFA
Na Mwandishi wetu
SHAMRASHAMRA za kusherekea ubingwa wa timu ya Chelsea katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya,zimeendelea kufana katika mataifa mbalimbali ikiwamo Tanzania,baada ya Heineken Champions Planet kuwaandalia pati mashabiki wa timu hiyo.
TAIFA STARS
Wachezaji wa timu ya taifa,Taifa Stars wakifanya mazoezi katika uwanja wa Karume Dar es salaam jana kwa ajili ya kuikabili timu ya taifa ya Malawi mwishoni mwa wiki hii(katikati) mchezaji Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa nchini Kongo katika klabu ya TP Mazembe.(Picha na Rajabu Mhamila)
Milovan aipa wakati mgumu Simba
Na Zahoro Mlanzi
KOCHA Mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba, Milovan Cirkovic ameiweka katika wakati mgumu timu hiyo baada ya kutaka kuongezewa mshahara kutokana na kuipa ubingwa timu hiyo.
Kutokana na hali hiyo, jana Kamati ya Utendaji ya timu hiyo ilikuwa na kikao kizito na kocha huyo katika moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam kujadili hatma ya kocha huyo.
23 May 2012
Ikwiriri sasa amani, mwafaka wafikiwa
Na Masau Bwire, Ikwiriri
MGOGORO mkubwa uliozuka Ikwiriri, Rufiji, mkoani Pwani kati ya wakulima na wafugaji kwa siku mbili mfululizo na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali umemalizika jana.
Utulivu katika eneo la Ikwiriri, umerejea baada ya Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi nchini, SACP Simon Siro, kutumia njia za kidiplomasia kutatua mgogoro huo.
MAZUNGUMZO
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akimsikiliza Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Profesa, Mark Mwandosya, mara baada ya kumuapisha Ikulu, Dar es Salaam jana, kushoto ni mke wa waziri huyo, Bi. Lucy Mwandosya. (Picha na Charles Lucas)
Polisi wakamata bunduki 4, risasi 436
Na Thomas Dominick
JESHI la Polisi mkoani Mara, limefanikiwa kukamata bunduki nne aina ya Short Gun, SMG na risasi 436 katika kipindi cha wiki mbili baada ya kuwakamata watuhumiwa nane wanaodaiwa kufanya uhalifu na uwindaji katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Waliovamia maeneo ya wazi kuondolewa
Na Grace Ndossa
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, inaendelea kufanya ukaguzi katika maeneo yote ya wazi ili kuhakikisha waliovamia maeneo hayo wanaondolewa haraka iwezekavyo.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Bw. Goodluck Ole Medeye aliyasema hayo Dar es Salaam juzi wakati akihojiwa katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na televisheni ya ITV.
Madiwani Kishapu wamkataa Mkurugenzi
Na Suleiman Abeid, Kishapu
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, wamefikia azimio la pamoja na kumkataa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Bw. Theonas Nyamuhanga.
Mbali ya kumkataa Mkurugenzi huyo ambaye hakuwepo katika kikao hicho, pia walimuomba Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo (OCD), kuhakikisha anamtafuta Bw. Nyamuhanga na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
HUDUMA CRDB
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, akizungumza nawaandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana, kuhusu upanuzi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, kusho ni Naibu Mkururugenzi Mtendaji Uendesha na Huduma kwa Wateja, Bw. Saugata Bandyopadhyay. (Picha na Peter Twite)
Lembeli: Kumuondoa Maige haikuwa kazi rahisi
Na Patrick Mabula, Kahama
MBUNGE wa Kahama, mkoani Shinyanga, Bw. James Lembeli, amesema kazi ya kumuondoa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Ezekiel Maige katika nafasi yake, haikuwa kazi rahisi.
Bw. Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Majengo mjini hapa.
22 May 2012
UTALII
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Dkt. Aloyce Nzuki (katikati), akizungumza na Naibu Waziri wa Utalii wa Afrika Kusini, Bi. Tokozile Xasa, alipotembelea banda la Tanzania, katika maonesho ya utalii ya INDABA yaliyofanyika Durban, Afrika Kusini hivi karibuni. (Na Mpigapicha Wetu)
KAMANDA SIRO KAZINI
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania,(SACP), Simon Siro ,(kulia), akishirikiana na mwananchi wa Ikwiriri (jina halikufahamika), kuondoa mawe katika Barabara ya Kilwa, eneo la Ikwiriri, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani jana, mawe hayo yaliwekwa na wananchi wenye hasira ili kuzuia magari yanayopita wakati wa vurugu kati ya wakulima na wafugaji. (Picha na Masau Bwire)
BODI YA MISITU
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi, Khamisi Kagasheki, akiteta na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Bw. Lazaro Nyarandu, wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Huduma za Wakala wa Misitu (TFS) Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
ZIARA NHIF
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Seif Suleiman Rashid (katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF), Bw. Emmanuel Humba na Naibu Mkurugenzi wa mfuko huo, Bw. Hamis Mdee wakati wa ziara ya kuangalia utendaji na kuongea na wafanyakazi wa mfuko huo, Dar es Salaam jana. (Picha na Charles Lucas)
Taa ya chemli yaua Morogoro
MKAZI wa maeneo ya Kasanga wilayani Morogoro Mkoa wa Morogoro Bw. Lucas Robert (48) amefariki dunia mara baada ya kulipukiwa na taa ya chemli aliyokuwa akiiwasha.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Bi. Adolphina Chialo tukio hilo lilitokea Aprili 17, mwaka huu, majira ya saa 12.45 alasiri maeneo ya Kasanga na kusababisha kifo chake wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa.
TAMASHA
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Morogoro Bw. Jasson Shumbusho (kulia),
akikabidhi Hundi ya Sh Mil 5.1, kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ngoma Afrika Bw. David Kitururu (wa pilia kushoto), kwa ajili ya Tamasha la Paukwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi za Manispaa ya Morogoro, litakalofanyika Uwanja wa Jamhuri wiki hii. Jumla ya shule 20 zitashiriki. (Picha na Aziz Msuya)
AJALI
Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, akimwelekeza dereva wa gari la polisi namba PT O152 kulisogeza mbele eneo la Mchicha Barabara ya Nyerere Dar es Salaam jana, baada ya kugongwa na daladala (halipo pichani) namba T 342 AWQ, linalosafiri kati ya Gongolamboto na Mwenge. (Picha na Prona Mumwi)
Ofisa Usalama afariki dunia
Na Lilian Justice, Morogoro
MWENDESHA pikipiki anaedaiwa kuwa Ofisa Usalama Manispaa ya Morogor mkoani Mrogoro amefariki dunia baada ya kugongana na mwendesha pikipiki mwenzake huko katika maeneo ya Mizani Kihonda katika manispaa hiyo.
KUMBUKUMBU
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj, Alhad Salum, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam juzi, mara baada ya kufanyika ibada ya kumbukumbu (Hitma) ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Mtabiri wa Nyota Afrika Mashariki Shekhe Yahya Hussein. (wa pili kushoto) ni mtoto wa marehemu Bw. Hassan Yahya Hussein na kulia ni mmoja wa maofisa wa taasisi mtabiri huyo, Shekhe, Hamisi Kondo. (Picha na Charles Lucas)
UMEME
Kaimu Mkurungenzi wa Shirika la (TANESCO),Bw. Boniface Njombe(aliyeinama) akimwonesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Said Mwambungu moja ya kifaa kilichoharibika katika moja ya mashine za kuzalisha umeme na kusababisha kupungua kwa uzalishaji wa umeme katika Mji wa Songea mkoani Ruvuma juzi. Kwa sasa upatikanaji wa nishati hiyo muhimu katika mji wa huo imekua kero kubwa.Picha na kassian Nyandindi
Ndugu wakamatwa na nyara za Serikali
JESHI la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia wakazi wawili ambao ni ndugu katika maeneo ya Kihonda Kilimanjaro Manispaa ya Morogoro mkoani humo kwa kosa la kukutwa na nyara za Serikali kinyume cha sheria.
Akizungumzia tukio hilo jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Bi. Adolphina Chialo alisema lilitokea Mei 19, mwaka huu, majira ya saa 9.00
alasiri huko maeneo ya Kihonda mjini hapa.
18 May 2012
GARI LA MAFISANGO
Gari Toyota Cresta lenye namba T 387 BMZ, likiwa limepondeka baada ya ajali iliyosababisha kifo cha mchezaji soka nyota wa Kimataifa wa Timu ya Taifa ya Rwanda na Simba SC ya Tanzania, marehemu Patrick Mafisango, iliyotokea eneo la VETA, Barabara ya Chang'ombe, juzi usiku. . (Picha zote na Charles Lucas)
Subscribe to:
Posts (Atom)
