29 May 2012
New Team mabingwa Copa Coca-Cola Ilala
Na Amina Athuman
MICHUANO ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ngazi ya wilaya, Kanda ya Ilala yalimalizika juzi kwa New Team FC kuifunga timu ya Sanry FC kwa mikwaju ya penalti 6-5 katika mechi ya fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao ulivuta umati mkubwa wa mashabiki kutokana na timu zote kuwa jirani, ulianza kwa kasi na ilibidi kipa wa New Team kufanya kazi ya ziada dakika 20 za kwanza kwa kuokoa mabao matatu ya wazi kutoka kwa washambuliaji wa Sanry FC, Twalib Mohammed na Hassan Kamoti.
Hata hivyo baada ya mashambulizi hayo, Sanry FC walitulia na kuanza kupeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa wapinzani wao, lakini mabeki walisimama vyema kuondoa hatari zilizoelekezwa kwao.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mashambulizi kwa zamu lakini hadi mwamuzi alipopuliza filimbi ya kumaliza mechi hiyo hakuna timu iliyoliona lango la mwenzake.
Baada timu hizo kutoka suluhu katika dakika 90 za kawaida, mwamuzi alilazimika kutumia sheria ya kupigiana mikwaju ya penalti ili kupata mshindi ndipo New Team FC ilibuika kidedea kwa mikwaju 6-5 dhidi ya wapinzani wao.
Mchezo huo ulikuwa ni hitimisho la kuchangua wachezaji watakaoungana na timu ya kombaini ya Mkoa wa Ilala kisoka, ambayo itaiwaikilisha kwenye fainali za Copa Coca-Cola zitakaoanza Juni Mwaka huu.
Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, timu ya Aggrey FC iliifunga Young Stars FC 5-4, mchezo ambao pia uliamuriwa kwa mikwaju ya penati baada ya timu zote kumaliza muda wa kawaida bila kufungana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment