30 May 2012
Changamoto zawaandama wauguzi mbalimbali
Na Salma Mrisho, Geita
IMEELEZWA kuwa mazingira magumu ya kazi yanayowakabili wauguzi hususan upungufu wa watumishi wa kada hiyo na malipo kidogo ni mojawapo ya changamoto zinazowafanya kutowajibika ipasavyo katika kazi zao.
Hayo yalibainishwa hivi karibuni kwenye kongamano la siku mbili na mkutano wa 12 wa Chama cha Wauguzi (TANNA) Mkoa wa Shinyanga ulioenda sambamba na kuwaaga baadhi ya wauguzi waliohamishiwa mikoa ya Geita na Simiyu.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo Bi. Liliani Matinga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bukombe aliwaomba wauguzi hao waendelee na umoja wao pamoja na baadhi ya wilaya kugeuzwa mikoa mipya.
"Ni vyema sasa kila mmoja akafanye kazi huko anakoenda kwa kuwajibika na kuwa kitu kimoja, ili kuepusha jamii kuwalalamikia kuwa hamfanyi kazi ipasavyo ingawa changamoto ya kufanya kazi katika mazingira magumu bado ipo," alisema Bi. Matinga.
Alisema, anatambua kazi ya uuguzi kuwa ni ngumu, lakini aliwapongeza na kusema baadhi ya uharibu muonekano mzuri wa fani hiyo kwa kuwatukana wateja wao na kuomba rushwa jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa kila siku na wananchi wanoenda kupata huduma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment