31 May 2012

UTALII


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Bw. Lazaro Nyalandu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana, kuhusu hali ya usalama Visiwani Zanzibar baada ya Serikali kudhibiti vikundi vya watu waliosababisha vurugu na kukanusha taarifa ya baadhi ya vyombo vya habari vya nje vilivyoripoti habari za kupotosha watalii. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa  Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Bw Richard Rugimbana. (Picha na Charles Lucas)

2 comments:

  1. jamani hebu tuacheni siasa kwenye mambo ya msingi yanayo husu inchi yetu tunasikitishwa sana na kitendo ambacho tulizani sasa tanzania itakuwa kisiwa cha amani bali kimegeuka kuwa kisiwa cha jamani shetani gani huyu.amani ni kila kitu watanzania tujifunze yaliyotokea kwa jirani zetu rwanda burundi na sehemu zingine jirani walianza hivi kama hao wachache wenye hakili chafu inayonuka yeye kujaa ubaguzi usiyokuwa na tija bali uroho wa madaraka.vijana tusitumiwe kama mataili ya gari yanayotegemea pumzi badala ya kufanya fujo tufanye kazi

    ReplyDelete
  2. TULIANZA KUCHANGANYA SIASA NA DINI TULIPOONYWA WATU WALIONA NI KUWANYIMA DEMOKRASA NA VIJANA WENGI WA DOT COM HAWAAMBILIKI WANAJUA KILA KITU WAZEE WANA MAWAZO MGANDO WANAAMINI TWITTER NA FACE BOOK YANAYOFANYIKA NIGERIA NA MISIRI WALA HAWANA HAJA YA KUFUATILIA WAZEE WAMEJITOA WAMEACHIA DUNIA IWAFUNDISHE NA INAWAFUNDISHA VIZURI TU

    ReplyDelete