29 May 2012

Mbunge aiokoa Korogwe United


Na Yusuph Mussa, Korogwe

MBUNGE wa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Tanga, Mary Chatanda ameiokoa timu ya soka ya Korogwe United kuweza kushiriki mashindano ya Kanda, baada ya kuwasaidia sh. milioni moja za kuwapiga jeki katika michuano hiyo.

Michuano hiyo itatoa timu zitakazopanda Daraja la Kwanza msimu ujao, ambapo timu hiyo imepangiwa kituo cha Musoma,Mara.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana mjini hapa, Mkurugenzi wa Korogwe United ambayo ndiyo mabingwa wa Mkoa wa Tanga, Filbert Mpezya alisema mbunge huyo aliwaingizia fedha hizo kwenye akaunti yao, ambapo pia zitawasaidia kukodisha basi dogo aina ya Coaster kwa ajili ya kwenda Musoma kwenye mashindano hayo.

"Unajua mashindano haya ni gharama hasa ukizingatia hayana udhamini, hivyo kwa kupata msaada wa sh. milioni moja kutoka kwa Mama imetusadia sana sisi kuweza kufika kwenye kituo cha mashindano na timu yetu inacheza mchezo wa kwanza leo na timu ya Red Cross ya Dar es Salaam," alisema Mpezya.

Naye Chatanda alisema ameamua kuisaidia timu hiyo, ili iweze kufanya vizuri kwenye mashindano hayo hatimaye iungane na Coastal Union na Mgambo JKT kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Nimewaingizia sh. milioni moja kama ahadi yangu niliyoitoa kwenye sherehe zao za ubingwa wa mkoa, lakini pia nitaendelea kuisaidia timu hii kama Mbunge na mkazi wa Korogwe kuona inacheza Ligi

No comments:

Post a Comment