30 May 2012
Waziri aanika uozo wa wahisani mbalimbali
Na Pamela Mollel, Arusha
IMEELEZWA kuwa bajeti nyingi za nchi za Afrika zimekuwa tegemezi kwa wahisani jambo ambalo linachangia uwepo wa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa maslahi ya wahisani husika.
Pia Serikali imetakiwa kutumia utawala bora wa fedha kwa wananchi wake na matumizi sahihi ya mali asili ili ziweze kuwa na tija kwa vizazi vijavyo na kuitumia demokrasia katika kukuza pato la wananchi.
Changamoto hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Elimu Mafunzo ya Amali kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Juma Shamuhuna wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
"Tumekuja kujifunza suala zima la demokrasia inavyoweza kukuza uchumi wa nchi yeyote sanjari na utawala bora wa matumizi ya fedha za serikali
na kuwa tunaelekea kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2012-13 ambapo tayari tutakuwa na tumepata uzoefu," alisema Waziri huyo.
Alisema kuwa, Serikali yeyote itakayofuata mambo matatu na kuyajali kwa maslahi ya wananchi wake hususan utawala bora wa fedha, matumizi sahihi ya
demokrasia sanjari na matumizi ya mali asili zitaifanya serikali kutokuwa
tegemezi kwa wahisani.
“Mashirika haya ya fedha ulimwenguni hayatoi fedha bure, lazima watangulize maslahi yao hali inayopelekea nchi zilizofadhiliwa 'kubaka' demokrasia na wananchi wake kuendelea kuwa maskini,” alisema Bw. Shamuhuna
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

KAMA NCHI KAMA MAREKANI INAKOPA KWA WAHASIMU WAO AMBAO NI WA CHINA SIO KUTUKANA UBEPARI HIVI HATA SISI KWENYE MASUALA YA UCHUMI TUNAWEZA KUSIMAMA NA KUTOA USHAURI WOWOTE KWA NCHI ZA ULIMWENGU WA KWANZA NA WA PILI WAKATUELEWA KUWA TEGEMEZI KWA MAWAZO TUKIACHA TU UTAKUWA NDIO UKOMBOZI MKUU
ReplyDelete