30 May 2012

Wahimizwa kuzingatia lishe bora muda wote



Na Suleiman Abeid, Shinyanga

IMEELEZWA kuwa maendeleo na mafanikio ya uchumi wa nchi yoyote duniani hutokana na wananchi wake kuwa na afya bora zinazowawezesha kufanya kazi za uzalishali mali pasipo matatizo.

Hali hiyo ilibainishwa juzi na Bw. Billie Edmott ambaye ni Ofisa wa Uchumi na Uzalishaji Mali mkoani Shinyanga katika uzinduzi wa duka namba 103 la Kampuni ya TIENS inayojishughulisha na usambazaji wa virutubisho vya mwili wa binadamu.


Bw. Edmott ambaye katika uzinduzi huo alikuwa amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Ally Rufunga alisema maendeleo ya nchi yoyote ile yanaletwa na wananchi wenye afya na kwamba wakiwa na afya zenye mgogoro haitokuwa rahisi kwao kufanya kazi kwa ufanisi.

Alisema, Watanzania wengi hufanya kazi zao katika mazingira magumu, lakini hata hivyo baada ya kazi hizo huwa hawapimi afya zao ili kuweza kubaini jinsi gani viungo vyao vimetumika ili viweze kuboreshwa kwa kupatiwa virutubisho.

“Uchumi wa nchi yetu hutegemea sana kilimo na asilimia 85 ya Watanzania ni wakulima ambao wapo vijijini, kwenye maeneo ya uzalishaji wa mazao mbalimbali. Sasa ili maendeleo yapatikane inatakiwa wakulima hawa wa vijijini wapate huduma ya kupima afya zao kila wakati ili waweze kuwa na afya bora,” alisema Bw. Edmott.

No comments:

Post a Comment